Waziri Mchengerwa: Nafungua milango ya fursa kwa Watumishi wa Umma kwenda nje ya nchi kupata mafunzo na ujuzi

Nakusalimu Mh. Rais kwa Jina la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Hongera mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wako ambao utawafaa sana mulipo katika utumishi wa Umma.

Hata hivyo nadhani itabidi maelezo ya ziada yatolewe kuhusu kama utaratibu wa awali wa kupewa kibali cha kusafiri toka kwa Katibu mkuu kiongozi unaendelea au la.

Hongereni watumishi na Kazi iendelee.
 
Juzi pale Nairobi jopo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Ughaibuni walikuwa na furaha sana huku wengine wakitafuna Mirungi na Vinywaji mbalimbali baada futari nzito nikajisemea moyoni kuwa... "Nyota njema huonekana Asubuhi"
 
Jamaa kweli aliharibu, halafu wanatudanganya uchumi wa kati.
Hawakudanganya kuhusu uchumi wa wakati. Maana Jiwe na wafuasi wake walikuwa uchumi wa kati na pengine wa juu kabisa, kupitia pesa walizokuwa wanaiba kwa mgongo wa maendeleo.
 
Safi sana.
Safari ni fursa, ni exposure, ni kupanua fikra, ni kuona wengine wanaishije

Mambo ya kufungiana ndani utadhani nguo kwenye kabati ni mambo ya ajabuajabu.

Let people have freedom of movement
Halafu siyo kwamba labda mnafungiana ndani kuna jambo la maana mnafanya. Hakuna

Mnafungiana ndani halafu, kazi inabaki ni:

Kila ukiamka unawaza ukamteke nani?

Ukamuue nani!

Unaanza kusikiliza simu za watu: Ummy Mwalimu anagombana na mashoga zake kwenye simu.

Kigwangalla haelewani na katibu wake,

January Makamba, Kinana, na Nape wanakuteta wanasema wewe ni mshamba🤣

Membe anakuteta na Mwenyekiti wa kijiji huko Rondo.

Mara umekosa kazi za kufanya, unavunja Jiji la Dar!!

Yaani hii ni sawa na baba wa familia huna cha kufanya unaanza kuhesabu vipande vya nyama kwenye sufuria au kufuatilia mke wa jirani yako anatembea na muuza mboga.
 
Back
Top Bottom