Waziri Mchengerwa: Nafungua milango ya fursa kwa Watumishi wa Umma kwenda nje ya nchi kupata mafunzo na ujuzi

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,183
2,000
Ni rasmi sasa watumishi wa serikali wamepewa ruhusa ya kwenda safari za nje ambazo zilisitishwa na hayati Magufuli.

========


1620394043853.png

Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mchengerwa amesema kuwa anawaagiza wakuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma kujipanga kwa ajili ya kutoa mafunzo ili kuongeza weledi kwa watumishi wa umma.

Amesema haiwezekani mtumishi afanye kazi kwa miaka mitano bila kupewa mafunzo yoyote ya kuongeza ujuzi kwa kile anachokifanya lazima atafanya kazi kwa mazoea pia wanataka watu wapewe weledi na ufahamu wa kufanya kazi kwa uweledi ili kazi ambayo walikuwa wanaifanya kwa masaa sita basi ifanyike kwa masaa 2 au saa 1 ila kiuweledi zaidi. Amesema wakuu wa Chuo cha Utumishi wa umma waandae semina, warsha kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo kwa watumishi.

Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi wahakikishe wanatumia fursa ya chuo hiki katika kupata mafunzo kama kuwapeleka China au popote duniani basi fursa hizo anazifungua na hakuna sababu ya kufunga milango kwani kuna wafadhili wengine wanakuwa wapo tayari kuwasaidia bila gharama, lakini katika kutekeleza hilo kutumike uzalendo na uataifa.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,909
2,000
Wacha watu wasafiri waingize hela katika mzunguko mradi tu ziwe safari zenye tija.

Sasa mtu safari anagharamiwa na wafadhili tena kwa shughuli za kiserikali(kikazi), halafu bado unamuwekea urasimu. Kama huo sio wivu, uduwanzi na kukomoana, ni nini?
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,119
2,000
Safi sana.
Safari ni fursa, ni exposure, ni kupanua fikra, ni kuona wengine wanaishije

Mambo ya kufungiana ndani utadhani nguo kwenye kabati ni mambo ya ajabuajabu.

Let people have freedom of movement
Safi kabisa hata kama mm siwezi kwenda wataoenda wataleta mambo mazuri.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,085
2,000
Wacha watu wasafiri waingize hela katika mzunguko mradi tu ziwe safari zenye tija.

Sasa mtu safari anagharamiwa na wafadhili tena kwa shughuli za kiserikali(kikazi) alafu bado unamuwekea urasimu kama sio wivu, uduwanzi na kukomoana ni nini?
As long as ni hiari yake mwache aende hata Kama Safari haina tija na ni gharama zake.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,433
2,000
Wasisahu tu ofisi za umma zinawahitaji kwa ajili ya kutoa huduma. Yasirudi yale maisha ya mtu wa kusaini kasafiri urudi mwezi ujao.
Hapa ndipo wanaposema uhuru lazima uwe na mipaka, uhuru bila mipaka ni vurugu, naamini wataweka utaratibu mzuri watu wasijisahau wanaposafiri nje.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom