Waziri Mchengerwa awahakikishia usalama wachezaji, mashabiki wa Simba wakiwa Afrika Kusini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,441
Waziri Mchengerwa.jpg
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Afrika Kusini kuishangilia Timu ya Simba katika mchezo wa raundi ya pili robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kuwa watakuwa salama.

Waziri Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 21, 2022 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na Vyombo vya Habari.

"Niseme tu kwamba sisi kama Serikali tunafuatilia kwa karibu usalama wa timu na hivi ninavyoongea nimemteua Msaidizi wangu Mkurugenzi wa Michezo ili aweze kuniwakilisha kusimamia hili" amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, Mchengerwa amesema watanzania na waafrika Kusini ni ndugu wa muda mrefu hivyo ni mategemeo kuwa hakutakuwa na jambo lolote linaloweza kuhatarisha usalama.

Ameeleza kuwa katika mechi hiyo Timu ya Simba inakwenda kushindana siyo kushiriki ili kuliwakilisha taifa ambapo amewataka wachezaji kucheza kwa weledi na ari kubwa ili ipige hatua katika hatua inayofuata hatimaye irudishe kombe nyumbani.

Akizungumzia kuhusu kuzisaidia timu za taifa, Mhe. Mchengerwa tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kufanya maandalizi kwenye makambi yote ya timu hizo.

Pia, amesema dhamira ya taifa ni kushiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na kuratibu mashindano hayo hapa hapa nchini.

Amesema tayari Serikali inafanya maandalizi hayo kwa kuandaa timu bora zitakazofuzu na kuandaa miundombinu ya michezo hiyo.

Katika hatua nyingine Mchengerwa amesema kutokana na kuendelea kufanya vizuri, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi nane Afrika ambazo kombe la dunia litapita ambapo hapa nchini linatarajia kufika mwisho wa mwazi huu.

Chanzo: Langolahabari
 
Kwani ni nani aliyewatishia usalama Simba?

Mbona kocha wa Orlando amewaambia waziwazi wao watawaonesha ukarimu Simba ili kuwafundisha uungwana? Au kingereza kigumu?
 
Atawapa ulinzi?
 
mnafanya fujo nyumbani,kesho mnatakiwa kwenda kwa wenzako unaanza kulalamika lalamika,nendeni mkanyooshwe
haaa,,tehe,,tehe pro Manara.

Simba timu pekee Tanzania na East Africa inayoshiriki michuano ya CAF,nchi zingine kama South Africa,Egypt wanatimu zaidi ya moja,kwaiyo inapaswa serikali ya Tanzania kuhakikisha inashughulikia usalama wa Simba popote pale wanapokwenda kucheza.
 
Hivi ni usalama upi mnaotaka wakati wenyeji wenu wameahidi kuwaonesha tofauti yao na nyinyi?

Wameahidi kuwaonesha utu na ukarimu, sasa mnaweweseka nini?
Mimi nahisi hawa kina Barbara kuna pesa wanapiga wanaposafiri na timu hasa mahotelini na matumizi ya timu ikiwa nje.

Hapa yanatengenezwa mazingira ya kumpiga ela Mo Dewji kukodi private security company kule Jo'burg kuilinda Simba kumbe ni kampuni ya muhindi mwenzake.

Hawa wahindi mjifunze kuishi nao kwa akili, hakuna muhindi ana mapenzi na ngozi nyeusi pasipo maslahi nyuma yake.

Mkumbuke Barbara ni muajiriwa ana make money kwa style yake.
 
akuna ubaya kutumia pesa kwaajili ya usalama wa timu.
 
Huyo demu anawapiga, mimi nawajuwa vizuri wadosi nafanya nao madili, yani anawajaza hofu ili kubariki upigaji wake.

Fanyeni financial auditing ya club yenu repoti ya CAG ina nafuu madudu mtakayokutana nayo.
 
taasisi kubwa kama serikali inapigwa kilasiku na wewe mwananchi upo CAG,TAKUKURU wapo,sembuse club za soka tena Africa huku matopeni?,acha ale pesa yule dada kwanza ni mzuri alafu smart,mchapa kazi pia.
 
Back
Top Bottom