Waziri Mchengerwa anena kuhusu watumishi wazuri

Waziri wa Utumishi wa Umma, Mhe. Mchengerwa amesema watumishi wengi wenye uwezo mzuri wa kiutendaji wana fanyiwa mizengwe na majungu ya kuharibiwa kazi, na mbaya zaidi mabosi wao wanakuwa ni sehemu ya kuwaharibia...
Nimemuelewa sana huyu mwamba......kauli yake ni nzito na inabidi ichukuliwe kwa uzito wake.

Watumishi wamekuwa wakinyanyasika sana......kisa weledi wao katika Utendaji.
 
Nimemuelewa sana huyu mwamba......kauli yake ni nzito na inabidi ichukuliwe kwa uzito wake.

Watumishi wamekuwa wakinyanyasika sana......kisa weledi wao katika Utendaji.
Kwakweli wakipatikana Mawaziri mfano wa huyu Mchengerwa Mambo yatabadilika.
na wtumishi watafanya kazi zao furaha na amani.

kwanza huyu mhe. nimemgundua ni mtu mwenye Hofu ya Mungu.

Kiongozi mwenye hofu ya Mungu ndiye anaye weza kuwatendea Haki watu.

Enyi Viongozi/watendaji mlio pewa dhamana ya kuwasimamia wengine acheni uonevu, acheni kuwaonea watu wenu, tendeni Haki.
Hizi nafasi mlizo pewa ni za muda tu, mtaziacha, hamuwezi kufa nazo, acheni kuwanyanyasa wengine.
 
Hilo suala ni kweli kabisa kuna ukandamizaji na ubabaishaji mwingi sana humo serikalini!

Kuna jamaa yangu yuko halmashauri moja huko mkoani, anasema tangu aanze kazi amepata misiba zaidi ya mara 7, hakuna msiba hata mmoja boss wake wa kitengo aliwahi kuhudhuria au hata kutoa mchango!

Yeye misiba anayoitambua nufiwa na baba,mama mzazi au mtoto lakini akifiwa hata na dada au kaka wa damu hiyo kwake haimuhusu!
Kwa mtindo huo ni ngumu hata kuhamasisha wengine kuhudhuria au hata kutoa mchango!

Wakati hayo yakiendelea humo idara nyingine hakuna msiba wa mwana kitengo unaopita bila mchango! Waziri anaweza kumaliza matatizo ya watumishi katika idara za serikali iwapo tu ataweka utaratibu wa kuwasiliana nao au njia ya kumfikishia taarifa moja kwa moja!
 
mfumo wwnyewe kaka,ukiona unazubgushwa ni kuwa ishu uumeileta,mkuu wa idara hawez kusema lastly mpaka murugenz aseme.so na unakuta barua yako mpk iende masjala ishubyako ishushwe kwetu,unakuta mkui yupo kikao cha cmt inabid urud kesho tu hakuna namna
Umeandika kindezi sana. Edit urudi tena.
 
That was my boss, ameletwa ofisini Ila kila kazi ananiita nimuelekeze hajui kitu maana ana miaka mingi kazini Ila sekta aliyokuwa anaitumikia ipo tofauti na yetu kule ni wizara huku ni corporate body, Kuna vikao vya bodi na Mambo tofauti hata namna ya kurespond hoja za bodi na Mambo mengine ya kuitawala...
 
That was my boss, ameletwa ofisini Ila kila kazi ananiita nimuelekeze hajui kitu maana ana miaka mingi kazini Ila sekta aliyokuwa anaitumikia ipo tofauti na yetu kule ni wizara huku ni corporate body, Kuna vikao vya bodi na Mambo tofauti hata namna ya kurespond hoja za bodi na Mambo mengine ya kuitawala...
Kuna ukweli fulani ingawa wengine hawataamini. Inaonekana mpaka Mhe. Waziri kutamka hilo, amelifanyia kazi na kupata ukweli.
 
Hilo suala ni kweli kabisa kuna ukandamizaji na ubabaishaji mwingi sana humo serikalini!
Kuna jamaa yangu yuko halmashauri moja huko mkoani, anasema tangu aanze kazi amepata misiba zaidi ya mara 7, hakuna msiba hata mmoja boss wake wa kitengo aliwahi kuhudhuria au hata kutoa mchango...
nufiwa ## mfiwa. Soma Standing Order vizuri ili ujue kuhusu michango kwa watumishi wanaofiwa.
 
Siasa Siasani, Mwana Siasa Asiaminiwe Popote Pale
Kwa Kauli Zake, Isipokuwa Labda Kwa Mbaali Vitendo
 
Haya Mambo ya kawaida sana serikalini namaanisha it's normal yamezoeleka kabisa.
ni kweli yamezoeleka na kuota mizizi, mbaya zaidi yanafanywa na viongozi watendaji.
matendo hayo ya majungu na fitina makazini, sio tu yanaondoa ufanisi makazini lkn pia yanaondoa ari ya kazi kwa wale wanao onewa na kunyanyaswa na viongozi wao wenye mamlaka.
ifike wakati sasa Waziri na wasaidizi wake walete mabadiliko ili kuondoa hali hii.
 
Fanya kazi
Subiri mshahara wako
Mambo yasiwe mengi Sana sote tunakufa na watu wanabadilika kila mara
 
Shida pia itakuja na kwenye hzo tume maana hao watakao pewa dhamana ni binadamu walewale pengine wenye sudi au hulka hyo hyo ya unyanyasaji.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Utumishi wa Umma, Mhe. Mchengerwa amesema watumishi wengi wenye uwezo mzuri wa kiutendaji wana fanyiwa mizengwe na majungu ya kuharibiwa kazi, na mbaya zaidi mabosi wao wanakuwa ni sehemu ya kuwaharibia.

Waziri Mchengerwa amedhamiria kuondoa hali hiyo katika idara zote za Serikali ameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa ni kama kansa ktk utumishi wa umma.

Kwa maneno hayo ya Mhe. Waziri inaonekana kuna tatizo kubwa sana tena sana. Viongozi wa juu yaani mabosi wana waonea sana watumishi wa chini, ukionekana mwerevu tu unapigwa nyundo ya kichwa. Kuna baadhi ya watendaji wenye dhamana wanajiona wao ni miungu watu

Ushauri:
kama kweli Waziri Mchengerwa amedhamiria kuwafuta machozi wanao nyanyaswa basi aunde tume maalumu itakayo fuatilia kero za watumishi ktk kila idara za Serikali nchi nzima.

Uchunguzi ufanyike kila idara, kuna uonevu mkubwa sana, watu wanaonewa na viongozi wao bila sababu za msingi, watu wanalia hakuna wa kuwasikia.

wapo watumishi wa umma wanatamani hata kuacha kazi kutokana na uonevu wanao fanyiwa na viongozi wao wa juu, wanachafuliwa kwa maksudi ili wasisonge mbele.
Hali hii ni hatari sana endapo itaachiliwa iendelee, lazima jambo lifanyike;
kwanza kubaini matatizo hayo ktk Idara zote za Serikali, lkn pia kuwaondoa viongozi watendaji ambao wamekuwa na tabia za uonevu kwa walio chini.


Wizara ya Elimu na Taasisi zake imekithiri sana kwa hili. Mh Waziri anza nayo. Ushahidi ni kesi zilizo Tume ya Utumishi wa Umma na kwingineko. Mungu amuongoze Mh Waziri aikomeshe kansa hii kwenye utumishi wa umma.
 
Shida pia itakuja na kwenye hzo tume maana hao watakao pewa dhamana ni binadamu walewale pengine wenye sudi au hulka hyo hyo ya unyanyasaji.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Pamoja na ubinadamu kuna watu wenye hofu ya Mungu hivyo watafanya haki. Mfano kwa sasa wote waliotumia madaraka vibaya wanapelekwa mbele ya vyombo vya sheria. Hata walitaka kuifanyia ugaidi nchi yetu wako kwenye vyombo vya sheria.
 
Ni jambo la kushukuru angalau Kwa mara ya kwanza WAZIRI Mwenye dhamana amebaini hilo tatizo la kupigwa nyundo watumishi wasio na godfather.

Angalau matumaini Kwa wanyonge yanaonekana.

Pongezi nyingi Kwa MHE WAZIRI Mungu azidi kumpa maarifa Na akili nyingi ZA kupambana Na waovu bila woga
Hongera sana Mh Waziri kwa kubaini uozo huu serikalini. Waweke watu makini kwenye uchunguzi wako utapata mengi sana ya kushangaza. Watumishi wanaohoji ubathirifu kwa ofisi za serikali hupotezwa kwa namna yoyote.
 
Ni ukweli usio fichika kuwa kuna tatizo kubwa la watumishi wazuri kiutendaji kuonewa na viongozi wao wa juu, uonevu ni mkubwa sana, watu wana umizwa sana, kuna viongozi miungu watu KAZI yao ni kuwa vunja moyo watendjibwazuri.

Kuna uonevu na fitina kubwa kati ya viongozi wenye dhmana na watumishi wa kawaida, kuna Majungu na fitina hatari!

Aanze na Mhimili wa Mahakama.
Kweli kabisa tatizo hili ni kubwa serikalini na linasorotesha sana ufanisi serikalini. Wizara ya Elimu na taasisi zake imekithiri sana kwa tatizo hili. Kuna kulindana iliyopitiliza na kutembeza bahasha ili kumdidimiza Mtu fulani iliyopiliza. Uchunguzi huru wa suala hili utabaini mengi sana ya ajabu na kusikitisha.
 
Huyu waziri anania njema sana, lakin kuna mambo yatambana, mojawapo bajeti.

Lakin bado anao uwezo wa kufanya yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake.

1. Kupamdisha watumishi vyei
2. Kulipa watumishi walio kaimu kwa muda mrefu bila kuthibitishwa.
3. Kurudisha kazini watumishi walio achishwa kazi bila taratibu za kiutumishi. etc etc
Mh waziri akiamua ataweza kwa kuwa serikali inataka ufanisi na si kufuga watu wanaolindana kwa sifa isiyojitosheleza. Imefika mahali hata Mh Rais wetu Mpendwa Mama Samia Hassan anaaminishwa kuwa kesi zilizoshindwa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma naye arithie kumbe mtandao ni uleule. Mh Waziri Mungu amekupa uwezo wa kugundua uozo huu uufanyie kazi.
 
Sijui amepanga kulimaliza vipi ilhali kuanzia Rais Wa Nchi mpaka mfagiaji wote wanachukia watu smart kichwani.

Hii nchi ili upande vyeo lazima uwe mlamba viatu.
Mimi naamini Mh Rais anawapenda watu smart sema walio karibu naye ndio wanamlisha uongo sasa kupitia kwa huyu Mh Waziri atapata ukweli.
 
Back
Top Bottom