OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 92
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea utendaji usioridhisha wa watumishi wa afya katika maeneo ya kutolea huduma nchini kwa kuwa unaenda kinyume na maadili ya utumishi.
Maelekezo ya Mhe. Mchengerwa yametolewa kwa niaba na Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume alipotembelea kituo cha Afya Mji Mwema Manispaa ya Songea ambacho hivi karibuni taarifa zilisambaa mtandaoni zikionesha wahudumu wa Afya kutowajibika kumsaidia mama mjamzito.