Waziri, Mbunge, Dr, Eng. John Pombe Mgufuli na Barabara za kukodi

Mokerema

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
235
123
Katika hatua ya kuhitimisha ufisadi , baada yakurejeshewa Wizara nyeti ya Miundombinu jana nimesikia John akisema wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ya kwamba Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameridhia ujenzi wa Barabara za kukodi na itaanza na Barabara ya Ubungo- Chalinze ambayo itapanuliwa kuwa na njia nne.
Utaratibu wa kujenga Barabara kwa mikataba ya BOT( Build Operate and Transfer) uliwahi kufanyika huko Amerika ya Kusini na umewaacha na matatizo lukuki. Maana yake ni kwamba anajitokeza mwekezaji na mara nyingi ni watu wenye pesa chafu. Anajenga Barabara kwa gharama zake na kuingia mkataba na Serikali ya kwamba atakusanya pesa kwa njia ya kuwatoza watumia barabara road toll na vinawekwa vituo vya kulipia (kama mnakumbuka serikali ya Kipindi cha kwanza cha Mzee Ruksa walijaribu kukusanya road toll na sote tunjua walivyokwama mpaka marehemu Kibona alipobuni kuondoa road toll posts na ikaingizwa kwenye mafuta) ili arejeshe gharama zake kwa kipindi cha mkataba.

Katika hali ya kawaida huo mkataba unakuwa wa miaka isiyopungua 20. Kinschojiri ni kwamba huyo mwekezaji/ tapeli anafanya kazi zote kuanzia usanifu hadi ujenzi ikiwa ni pamoja na usimmizi hapo ndipo penye kasheshe! Barabara huharibika kabla ya miaka kumi na ndipo tuaachia vizazi vijavyo madeni?
Kwa kifupi Magufuli na TANROADS yake wameshindwa kusimamia Barabara ya Kilwa fupi tu na ikabomoka baada ya miezi sita! Tena msaada wa Japan na Mfugale angeweza kwenda kwa miguu kusimamia. Sasa hiyo kilometa 100 itakuwaje. Najua atasema huko DRC wanafanya kachunguze hiyo rate ya road toll ni laana tupu.:A S 465: Pia ujue ni ufisadi per se anaanza na Barabara muhimu kweli ili wakamue kiulaini. Mkapa alikataa ushauri huo wa kipuuzi na akaamua Barabara zijengwe kwa fedha za ndani sasa hiyo U turn tena sidhani kama imepelekwa Bungeni ila huyu Mtusi ni balaa. Alimdanganya Mkapa wakajiuzia nyumba za Serikali sasa anamdanganya Jakaya Kikwete huyu ****** mpole kubinafsisha Barabara huu ni zaidi ya uhaini. Hivi kwa nini bado yuko hai?
 
Punguza Jazba, kasome andiko lao la huo mradi. Kama road toll itahamishwa kutoka kwenye mafuta na kukusanywa cash, itapunguza gharama za wakulima maana matrekta yaliyo mashambani nayo hulipa road toll kupitia dizeli, gharama za kuendesha vijenereta n.k
 
Mie naona poa tu ila hiyo BOT itumike kwa barabara za ndani ya Dar es salaam kwa maana wananchi wa Dar wengine wana hela kuliko serikali.Hii Ingesaidia kupunguza hii mifoleni.
 
mbona mimi naona sawa tu! mtoa mada inaonekana hutaki maendeleo maana naona unemzungumzia magufuli utadhani barabara zake bwana. Mbona kila kitu siku ni ubinafisishaji kwani tatizo liko wapi? wabongo bwana! kama kitu anaona hapati marupu rupu anakikandaia kinoma!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jamani mimi naona huu mkataba usitishwe mpaka tupate katiba mpya itakayoruhusu mikataba yote kupitia bungeni,
serikali hii haijawahi kusaini mkataba kwa maslahi ya nchi.hiyo ni janja ya ccm kuiibia nchi.
 
Katika hali ya kawaida huo mkataba unakuwa wa miaka isiyopungua 20. Kinschojiri ni kwamba huyo mwekezaji/ tapeli anafanya kazi zote kuanzia usanifu hadi ujenzi ikiwa ni pamoja na usimmizi hapo ndipo penye kasheshe! Barabara huharibika kabla ya miaka kumi na ndipo tuaachia vizazi vijavyo madeni?

Kwenye red: Kama mkataba ni wa miaka 20, ina maana matengenezo/road maintance kipindi cha mkataba itakuwa jukumu la serikali au huyo mwekezaji?

Kwa kifupi Magufuli na TANROADS yake wameshindwa kusimamia Barabara ya Kilwa fupi tu na ikabomoka baada ya miezi sita!
Hivi hii barabara sio ndio Magufuli kawazalimisha wa-japan kurudia ujenzi? tena kwa gharama zao wenyewe wa-japan? Na nani aliingia mkataba wa awali na hawa wa-japan? nahisi ni Kawambwa!

Alimdanganya Mkapa wakajiuzia nyumba za Serikali sasa anamdanganya Jakaya Kikwete huyu ****** mpole kubinafsisha Barabara huu ni zaidi ya uhaini. Hivi kwa nini bado yuko hai?

Uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulikuwa wa baraza la mawaziri. Hivyo yeyote angekuwa ndio waziri wa wizara hii kipindi hicho angetakiwa kufanya alichofanya Magufuli maana ndio uamuzi wa cabinet. Na hapa ndio naona tunapotea kwa kum-target mtu mmoja mmoja wakati wenye nyumba wanatucheka. Mfumo wa uongozi hapa Tanzania bado ni 'chama kushika hatamu'. Rais ndiye pia mwenyekiti wa ccm - chama tawala. Hivyo kama kama mwenyekiti wa ccm ambaye pia ni rais aliongoza kikao kilichoridhia/agiza nyumba za serikali ziuzwe ina maana CCM-wote wameridhia. Narudia CCM wote wameridhia maana hakuna mahali popote iliporepotiwa kuwa ccm wamekaa na kutoa tamko la kutoridhia uuzwaji wa nyumba za serikali. Kuendelea kumkaba Magufuli koo - we are missing the point.
 
Ninavo fahamu msongamano mkubwa uko ndani ya jiji, kuanzia Mbezi kuingia kati ya jiji. Sasa hii ya kuweka njia nne mpaka Chalinze si niufisadi!! Ingawa itasaidia kwa hapo badae na kuponguza ajali za uso kwa uso, kwanini wasiziongezee upana njia za Pugu road a.k.a Nyerere road, Kilwa road, Bagamoyo road a.ka A. H Mwinyi, Bandari road a.k.a Mandela na nyingine zinazojengwa sasa hivi Kama za kigogo bila kusahau uhuru na msimbazi
 
Katika hali ya kawaida huo mkataba unakuwa wa miaka isiyopungua 20. Kinschojiri ni kwamba huyo mwekezaji/ tapeli anafanya kazi zote kuanzia usanifu hadi ujenzi ikiwa ni pamoja na usimmizi hapo ndipo penye kasheshe! Barabara huharibika kabla ya miaka kumi na ndipo tuaachia vizazi vijavyo madeni?

Kwenye red: Kama mkataba ni wa miaka 20, ina maana matengenezo/road maintance kipindi cha mkataba itakuwa jukumu la serikali au huyo mwekezaji?

Kwa kifupi Magufuli na TANROADS yake wameshindwa kusimamia Barabara ya Kilwa fupi tu na ikabomoka baada ya miezi sita!
Hivi hii barabara sio ndio Magufuli kawazalimisha wa-japan kurudia ujenzi? tena kwa gharama zao wenyewe wa-japan? Na nani aliingia mkataba wa awali na hawa wa-japan? nahisi ni Kawambwa!

Alimdanganya Mkapa wakajiuzia nyumba za Serikali sasa anamdanganya Jakaya Kikwete huyu ****** mpole kubinafsisha Barabara huu ni zaidi ya uhaini. Hivi kwa nini bado yuko hai?

Uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulikuwa wa baraza la mawaziri. Hivyo yeyote angekuwa ndio waziri wa wizara hii kipindi hicho angetakiwa kufanya alichofanya Magufuli maana ndio uamuzi wa cabinet. Na hapa ndio naona tunapotea kwa kum-target mtu mmoja mmoja wakati wenye nyumba wanatucheka. Mfumo wa uongozi hapa Tanzania bado ni 'chama kushika hatamu'. Rais ndiye pia mwenyekiti wa ccm - chama tawala. Hivyo kama kama mwenyekiti wa ccm ambaye pia ni rais aliongoza kikao kilichoridhia/agiza nyumba za serikali ziuzwe ina maana CCM-wote wameridhia. Narudia CCM wote wameridhia maana hakuna mahali popote iliporepotiwa kuwa ccm wamekaa na kutoa tamko la kutoridhia uuzwaji wa nyumba za serikali. Kuendelea kumkaba Magufuli koo - we are missing the point.

Si Magufuli wala Kawambwa wanoingia mikataba ya ujenzi wa barabara bali TANROAD ila Magufulia nachofanya ni kufanya kazi na vyombo vya habari ili kujitafutia sifa. Nakumbuka alipoingia tu katika wizara hiyo alikuta akina Kawambwa wameshakamata watu waliozdisha fedha za fidia yey akawa wa kwanza kutangaz akatika vypombo vya habari ili apate sifa.

Iweje sifa nzuri zinzotokana na maamuzi ya Cabinet kama ujenzi wa barabara ziende kwa Magufuli peke yake badala ya Serikali nzima ila sifa mbaya kama kuuza nyumba za Serikali lawama ziende kwa Cabinet. maamuzi mangapi ya Cabinet yasiyo na maslahi kwa taifa huwa yanabaki katika mafaili tuu? Kashafa hii ya uuzwaji wa nyumba za Serikali ni ya Magufuli hata mfanyeje tena akajinufaisha yeye, ndugu zake na mahawara wasio kuwa watumishi wa Serikali
 
Kweli Magufuli week hii ameandikwa sana kutokana na mabo ya Kigamboni! Na pengone ataendelea kuandikwa kwa majuma kadhaa. Ameandikwa kwa mambo ya kweli na kwa mambo yasiyo kweli, mfano huyu bwana ni Msukuma leo anaitwa Mtusi. Huyu bwana ni Mkemia leo anaitwa Eng (maana yake Mhandisi). Great thinkers 'jaribuni kufanya utafiti kabla ya kuandika taarifa zinazosomwa na watu pengine wenye ufahamu kama wa waandaaji wa threads au zaidi.
 
3
Comments

More On : Al Wasl, ALnasr, Juan Mercier

36037hp2.jpg

Diego Maradona's UAE club Al Wasl have revealed they have signed three-time Argentina international Juan Ignacio Mercier from Saudi Arabian outfit Al Nasr.

The 31-year-old midfielder, who was given his international debut by Maradona, had been linked with Al Wasl for the past few weeks.

And while Al Wasl haven't officially confirmed his acquisition, a club spokesperson told Sport360 he had been signed.
 
Kwa kifupi Magufuli na TANROADS yake wameshindwa kusimamia Barabara ya Kilwa fupi tu na ikabomoka baada ya miezi sita!
Good point!
Wahandisi wa Ujenzi kazi yao kuu ni kuhakikisha kuwa ujenzi unaoendelea unakidhi viwango. Siyo kusubiri mwishoni ili kupata sifa ya kukataa barabara. Walikuwa wapi wakati inajengwa chini ya kiwango?
KUBWA ZAIDI; KWA NINI BARABARA YA BAGAMOYO INAJENGWA KWA UTARATIBU ULE ULE WA KILWA ROAD WAKATI IMESHATHIBITISHWA KUWA UJENZI HUO WA KUWEKA LAMI JUU YA KIFUSI BADALA YA JUU YA KOKOTO HAUFAI?
Dr. (wa Kemia, siyo Uhandisi) J. Pombe Magufuli anasubiri Bagamoyo Road imalizike kisha aikatae?
 
pombe sio mkemia bwn ni mhandisi,jaribu kujikip updated na mambo
 
pombe sio mkemia bwn ni mhandisi,jaribu kujikip updated na mambo

We ndio umekosea. Magufuli ana Ph.D ya Kemia (ni mkemia) na sio uhandisi. Fuatilia habari kwa makini, utaona ukweli wake
 
Jamani mimi naona huu mkataba usitishwe mpaka tupate katiba mpya itakayoruhusu mikataba yote kupitia bungeni,
serikali hii haijawahi kusaini mkataba kwa maslahi ya nchi.hiyo ni janja ya ccm kuiibia nchi.

Hiyo kitu lazima itekelezwe mkuu, na wewe kama hutoweza kulipa road toll basi hamna option nyingine zaidi ya KUPIGA MBIZI
 
pombe sio mkemia bwn ni mhandisi,jaribu kujikip updated na mambo
Mh alikuwa mwalimu wa Chemistry na Physics lakini haimzuii yeye kujiendeleza na akawa Mhandisi. Mhandisi si lazima awe wa barabara tu kuna umeme, maji, simu, magari,marine, agro, kompyuta, etc etc. nakuunga mkono.
 
As of now, Magufuli hana shahada ama stashada ya juu yoyote ya uhandisi ili aweze kuitwa mhandisi a.k.a engineer!

Dr. Magufuli ni mwalimu wa sayansi. Hiyo Ph.d aliyonayo kaipata kwenye chemistry na kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa mwalimu sengerema secondary akifundisha physics na chemistry.

Kama una taarifa za yeye kusomea uhandisi tufahamishe alisoma lini na wapi.
 
Back
Top Bottom