Waziri Mbarawa aitaka TPA kujenga gati

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
8 (1).JPG

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuanza ujenzi wa maegesho ya meli katika bandari ambazo meli mbili mpya zinazojengwa na Mamlaka hiyo katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela, zitatoa huduma ya usafiri baada ya kukamilika.

Waziri Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo alipokagua bandari ya Mbambabay iliyopo Wilayani Nyasa ambayo ni miongoni mwa bandari ambazo meli hizo zitatoa huduma na kubaini kuwa bado bandari hiyo haina maegesho kwa ajili ya meli hizo.

"Nataka kuona maegesho ya meli yanakamilika haraka ili kuwezesha meli mpya kupakua na kupakia mizigo katika bandari hii", amesema Waziri Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa meli hizo mbili za mizigo ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Agosti na Oktoba zitaongeza kasi ya utoaji wa huduma katika bandari hiyo na kuwa chachu ya maendeleo hususan katika shughuli za biashara na kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na nchi jirani.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemtaka Meneja wa Bandari ya Kyela kuisimamia kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boart Yard inayojenga meli hizo ili zijengwe kwa ubora na viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zinatokana na kodi za wananchi.

Katika Hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara ya Mbinga- Mbambabay yenye urefu wa Km 66 ambayo Serikali iko katika hatua ya kumtafuta mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaimarisha huduma ya bandari ya Mbambabay na kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa Ruvuma Eng. Lazeck Alinanuswe amesema kuwa kwa sasa wakala unakamilisha zoezi la kulipa fidia kwa wananchi waliopo katika hifadhi ya barabara wakati hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa zinakamilishwa.

Naye Meneja wa Bandari ya Kyela Percival Salama amemueleza Waziri kuwa pamoja na changamoto ya kukosa wa chombo cha usafiri majini kinachotoa huduma katika bandari hiyo pia ameomba kuboresha huduma za miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami ili kuwezesha ufanisi wa bandari.

"Kuimarika kwa barabara ya mbinga-mbambabay na barabara nyingine za maingiliano katika bandari hii kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza fursa za uwekezaji na biashara na Mkoa na nchi jirani", Waziri Prof. akame Mbarawa, yuko katika ziara ya Kikazi Mkoani Ruvuma kukagua miradi ya Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Meneja wa Bandari ya Kyela, Percival Salama (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) ya namna shughuli za biashara ya makaa ya Mawe zinavyoweza kuongeza pato kwa bandari ya Bambabay Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akisalimiana na baadhi ya Madereva wa Malori wanaosafirisha makaa ya mawe Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, Mkoani Ruvuma.
 
Tenda hiyo ya ujenzi wa gati ifuate taratibu zote halali za kiserikali maana huko ndiyo kwenye kichaka cha ufisadi
 
Uwezo wa kujenga gati upo nje na uwezo wa tawi hilo la TPA.Pia usimamizi wa ujenzi wa meli kwa huyo meneja na wasaidizi wake its beyond their capability.Ujenzi wa meli husimamiwa na Marine Surveyor wa Classification society itakayo sajili meli hiyo tokea michoro hadi kukamilika.Profesa fanya homework,otherwise utageuka kichekesho.
 
Back
Top Bottom