Waziri Mbarawa afungua kundi la Whatsap la watumishi wa Muwsa

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema atafungua Group la mtandao wa kijamii wa Whatsap maalum kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi(Muwsa).

Amesema lengo ni kuimarisha mawasiliano uwazi na uwajibikaji kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo. Pia amewaonya wafanyakazi hao kutotumia mtandao huo kumwomba michango ya harusi wala kutuma majungu,fitina na uchochezi dhidi ya utawala kwa mambo wasiyokuwa na uhakika nayo. Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo Agosti 2, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.

Amesema atafungua kundi hilo yeye mwenyewe ili asiwepo anayeweza kumtoa. "Nafungua Group la Whatsap leo mimi mwenyewe na nitaliita Muwsa,tutaweza kupeana taarifa mbalimbali za mamlaka na utendaji kazi wetu na kwa hali hiyo tutaweza kubadilika"amesema Mbarawa.

Amesema Group hilo litaanzishwa kwa maslahi ya mamlaka hiyo na wafanyakazi. Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii, uwazi na uadilifu ili kuboresha utoaji wa huduma. "Kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wanashirikiana na vishoka kuiba maji, wengine wanadiriki kuwaunganishia watu maji kiujanjaujanja, sasa naomba uwazi,uwajibikaji na uadilifu,"amesema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Muwsa Profesa Faustine Bee amesema mamlaka hiyo itaendelea kujipanga ili kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi.
 
afungue na la wakazi wa moshi ambao ni wadau wakuu wa huduma ya/za maji; au ndio amesema hataki kero...
 
Mwambieni arifungue Jumapiri iri niende nikarizindue, nimemisi kuzindua zindua.

Na nyinyi ma-DC hakikisheni una magurupu si chini ya kumi maana hayo yatanitosha kufanya uzinduzi mwaka mzima.

Mbishi nitarara naye mbere

Makofi pwaa pwaa pwaa
 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema atafungua Group la mtandao wa kijamii wa Whatsap maalum kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi(Muwsa).

Amesema lengo ni kuimarisha mawasiliano uwazi na uwajibikaji kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo. Pia amewaonya wafanyakazi hao kutotumia mtandao huo kumwomba michango ya harusi wala kutuma majungu,fitina na uchochezi dhidi ya utawala kwa mambo wasiyokuwa na uhakika nayo. Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo Agosti 2, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.

Amesema atafungua kundi hilo yeye mwenyewe ili asiwepo anayeweza kumtoa. "Nafungua Group la Whatsap leo mimi mwenyewe na nitaliita Muwsa,tutaweza kupeana taarifa mbalimbali za mamlaka na utendaji kazi wetu na kwa hali hiyo tutaweza kubadilika"amesema Mbarawa.

Amesema Group hilo litaanzishwa kwa maslahi ya mamlaka hiyo na wafanyakazi. Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii, uwazi na uadilifu ili kuboresha utoaji wa huduma. "Kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wanashirikiana na vishoka kuiba maji, wengine wanadiriki kuwaunganishia watu maji kiujanjaujanja, sasa naomba uwazi,uwajibikaji na uadilifu,"amesema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Muwsa Profesa Faustine Bee amesema mamlaka hiyo itaendelea kujipanga ili kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi.
Ni hatua nzuri
 
Back
Top Bottom