Waziri matatani; Sakata la upanuzi bandari - Alitaka kuwazunguka Mkulo na Dk. Kawambwa

Lazima amteme mkandarasi wa awali kwa sababu hakufanya naye mkataba hivyo hana fungu la 10% kutoka kwake inabidi aanza mchakato na mkandarasi mpya aweke 10%.hakuna kujali maslahi ya taifa, jali maslahi binafsi zaidi.wamwondoe waweke waziri mwenye kutambua wajibu wake pamoja na dhamana aliyopewa.
 
..hawa watu wananishangaza sana.

..Kenya amezindua ujenzi wa bandari ya Lamu, reli na bomba la mafuta kuelekea Sudani ya Kusini.

..Bandari ya Lamu itakuwa na gati 32. Itakuwa na refinery ya mafuta.

..wakati washindani wetu wanafanya mambo makubwa,sisi wa-Tanzania tumengangania kuongeza gati mbili[ya 13 na 14] ktk bandari yetu.

..tusipokuwa makini hii bandari ya DSM itaishia kupokea mitumbwi na majahazi, meli zote zitakuwa zinatia nanga Lamu na Mombasa.

NB:

..kitu cha kushtua zaidi ni kwamba China ambao ni maswahiba wetu kwa miaka mingi sasa wametutupa mkono wanashirikiana na Wakenya. Wameshaona kwamba ktk eneo hili wa-Tanzania hatuna maana tena.

..angalia hata Raisi wetu huko Brazil anakotembelea. Badala ya kukutana na wawekezaji anakutana na Kocha uchwara wa mpira Maximo!!
 
Naona kuna harufu ya kupakana matope watu wametibuliwa ulaji wao sasa wanapaka matope. Ni vema tuambiwe terms of loan za mkopo Exim kwanza? Mchakato wa kupatikana hiyo kampuni ya mwanzo ya ujenzi na mkandarasi zilikuwa vipi na kwanini waziri Nundu aliamua kuweka ngumu kumkataa. Inabidi uzalendo uwepo binafsi nimekosa imani na wabunge wetu ambao wanaomba rushwa hadi kwa wagombea ubunge wa East Africa. Siwaamini hata kidogo tunaomba ufafanuzi zaidi tufahamu mbichi zipi na mbivu zipi.

Nitashangaa sana kama huyu Nundu atadumu kwenye wizara hii naona kama vile amekalia kuti kavu!! Hii miradi ilianza wakati wa Kawambwa akiwa waziri wa hii wizara na Kawambwa alimleta mtu wake toka chuo kikuu ili wafanye mambo yao pamoja zikiwemo hizi projects za bandari; miradi yote hii ilikuwa ni miradi ambayo Kiwete alikuwa anaifuatilia utekelezaji wake kwa karibu sana lakini Nundu alipoingia alibadilisha muelekeo, kwanza kwa kumuondoa yule mtu wa Kawambwa halafu kuanza upya jinsi ya kutekelza hii miradi kitu ambacho mkuu wa kaya hakuwa na furaha nacho na ndio maana mpaka leo hii hata shirika landege ATCL lina acting CEO ambae ni chaguo la Nundu na sio chaguo la Mkulu na hivyo ndio maana amekaa kimya hata hajishuhulishi kuteua mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo mpaka sasa. Itakuwa miujiza kama huyu Nundu atasurvive katika wizara hiyo mara cabinet reshuffle itakapotokea.
 
Mawaziri wa serikali moja, bosi wao mmoja mkishindana si mnaenda kupata clarity kwa bosi wenu?? vikao vya baraza la mawaziri si vipo watoe msimamo wa pamoja na wa kiserikali????? kaaaaaaazi kweli kweli
 
Hutu nundu ana matatizo tanga kwnyew kuna bandar inayotarajiwa kujengwa joint na uganda mpka leo longo longo miaka mitan ni mchakato tu wanaandaa mazingira
 
Nchi yetu itajengwa na wale wanaoitakia mema. Jamani Bandari ya Dar haiwezi kupanuliwa kuongeza ufanisi zaidi ya kutumia fedha zaidi ktk Ufisadi. Kwa nini inakuwa vigumu sana kwa viongozi wetu kupeleka maendeleo sehemu nyinginezo. Tunazo Bandari za Tanga na Mtwara, hizi mbona zinakufa badala ya kuboreshwa zikaweza kuifanya kazi kubwa kwa miaka 50 ijayo?.. Bandari ya Dar ifungwe kwa kupokea mizigo ibakie bandari ndogo ya meli za watalii kama cruisership, Yatch club na mji wa kisasa wenye Ofisi na Condominium ambazo zitaongeza pato la Halmashauri kutokana na pango... Hadithi kwisha.

si umesikia kwamba taqyari bandari ya mtwara wamepewa wanaoidai atcl?
hivyo labda bandari ya tanga tena kama na yenyewe bado wenye meno hawajaigawa.
 
Hii habari imekaa kiunazi sana. Yaani madudu yote haya, na mwandishi kashindwa hata kumsumbua waziri Nundu kumtaka ajieleze kuhusu kashfa hii? Kuna kitu hapa ambacho kimejificha. I hope we will find out soon.

Hata na mimi naona kuna fitna fulani hapa ambayo imejificha. Labda ugomvi ambao hawausemi ni ile 10% inayotusumbua, maana atakaefanikisha huo mradi hiyo percent inakwenda kwake.
 
Nchi yetu itajengwa na wale wanaoitakia mema. Jamani Bandari ya Dar haiwezi kupanuliwa kuongeza ufanisi zaidi ya kutumia fedha zaidi ktk Ufisadi. Kwa nini inakuwa vigumu sana kwa viongozi wetu kupeleka maendeleo sehemu nyinginezo. Tunazo Bandari za Tanga na Mtwara, hizi mbona zinakufa badala ya kuboreshwa zikaweza kuifanya kazi kubwa kwa miaka 50 ijayo?.. Bandari ya Dar ifungwe kwa kupokea mizigo ibakie bandari ndogo ya meli za watalii kama cruisership, Yatch club na mji wa kisasa wenye Ofisi na Condominium ambazo zitaongeza pato la Halmashauri kutokana na pango... Hadithi kwisha.

Tattizo kubwa liipo ni viongozi kufanya maamuzi kwa kuzingatia miaka miwili au mitano tu ijayo na a sio miaka 10 au 20 au 30 ijayo. Na kwenye Kipindi cha utawala wa JK sijasikia badari ya Tanga au Mtwara zikingoelewa sana sana utasikia banadri mpya ya bagamoyo .

Wilaya ya bagamyo ambayo tunaweza kusema ni ya kitalii na kihistoria sasa inapewa kipumbele hata miradi ya viwanda vizito vya chuma. Kuna project nyingi sanaza kimaendeeo eo zingefanyiwa kazi bagamyoyo bila kubadilisha dhima kuu.

Kwenye jumuiya ya EU maneo yaliyochaguia kuwa ya kihistoria na Kitaii kuna badhi ya miradi hawawezi /hawaruhusiwi kufanya sababu maene hayo yamepewa kipaumbele kwenye miradi mingine

Usishangae hata mfano wakitaka kujenga chuo kingine cha kisasa cha kijeshi kushirrikiana na wa-USA nakuambiwa kuchagua kati ya kisarawe na bagmoyo kijengwe wapi kwa serikali ya sasa itachaguliwa bagamoyo.Why not kisarawe.Sababu vingozi hawafanyi mamuuzi strategically Kitaifa
 
Nitashangaa sana kama huyu Nundu atadumu kwenye wizara hii naona kama vile amekalia kuti kavu!! Hii miradi ilianza wakati wa Kawambwa akiwa waziri wa hii wizara na Kawambwa alimleta mtu wake toka chuo kikuu ili wafanye mambo yao pamoja zikiwemo hizi projects za bandari; miradi yote hii ilikuwa ni miradi ambayo Kiwete alikuwa anaifuatilia utekelezaji wake kwa karibu sana lakini Nundu alipoingia alibadilisha muelekeo, kwanza kwa kumuondoa yule mtu wa Kawambwa halafu kuanza upya jinsi ya kutekelza hii miradi kitu ambacho mkuu wa kaya hakuwa na furaha nacho na ndio maana mpaka leo hii hata shirika landege ATCL lina acting CEO ambae ni chaguo la Nundu na sio chaguo la Mkulu na hivyo ndio maana amekaa kimya hata hajishuhulishi kuteua mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo mpaka sasa. Itakuwa miujiza kama huyu Nundu atasurvive katika wizara hiyo mara cabinet reshuffle itakapotokea.

Mkuu hiyo reshufle inamuhusu nini wakati keshanunua Ghorofa Tanga la kiinua mgongo
Nani anasema siasa hailipi ?
 
Mkuu Borat, ongea mambo ambayo una uhakika nayo. Kamwe usiamini habari za kusikia. Hiyo ghorofa kama inajengwa au imenunuliwa, sio kutokana na rushwa. Huyu bwana, kama unakumbukumbu nzuri, alikuwa President wa International Civil Aviation Organization (ICAO). Mimi nadhani mshahara na marupurupu aliyokuwa anapata pale ingetosha kufanya project yoyote aitakayo au hata kuritire mapema. Tujaribu kutumia objective badala ya subjective kwenye arguments zetu, vinginevyo tutakuwa tunaendeleza chuki tu.

Ningekuwa mwandishi wa habari kama hii, ambayo inamuhusu mtu muhimu kama Bwana Nundu, ningefanya juu chini kupata japo sentensi mbili kutoka kwa Nundu mweyewe au kwa mtu aliyekaribu nae,li atleast kuonyesha contrast ya habari. Lakini haya mambo ya kumeza kama kasuku sidhani kama yana manufaa kwa taifa.
 
Leo naomba tumkumbuke aliyekuwa waziri wa Ujenzi enzi zileeeee....... NALAILA KIULA
 
Hata na mimi naona kuna fitna fulani hapa ambayo imejificha. Labda ugomvi ambao hawausemi ni ile 10% inayotusumbua, maana atakaefanikisha huo mradi hiyo percent inakwenda kwake.

Hicho kichwa cha habari tuu kinaonyesha kua mtoa mada ana agenda ya siri, haionekani kulikua na haja ya kutumia neno kumzungumka Kawambwa wakati umeshasema kwamba Kawambwa hayupo tena ktk wizara hiyo sasa nini tatizo lake.

Kinachoonekana kuna utaratibu wa kutaka kumpaka matope Nundu kwa sababu ya uchapakazi wake wakati watu wameshazoea wababaishaji. Kama mimi ni Nundu ningerudi kwenye kazi yangu kuliko kukubali kutolewa mmvi na watu wasio elewa na ambao rusha imekua kama sehemu ya maisha yao. Nundu chapa kazi
 
Fuatilia taarifa ya kamati ya bunge halafu utuambie ulichotuambia hapa (especially baada ya Nundu kujibu). Kama Nundu ndio mzalendo na mchapakazi kwa kile alichokifanya kuhusiana na huu mradi (kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya bunge) basi Mungu atuonee huruma Watanzania, maana nashindwa kupata picha ya kile kinachofanywa na utakaowakubali kuwa ni wezi!
 
Taarifa ya Kamati ipi? Ile Kamati ambayo imeongwa na watu wa TPA na mwekezaji aliyeweka cha juu usd 200 million katika mradi? Kilichokuwa kinaendelea katika hotuba ya mwenyekiti wa kamati ya bunge ni kupigia chapuo mradi wa kifisadi kwa kumkaanga waziri. Na for the record, hapajawahi kufanyika uchunguzi wowote rasmi wa kamati ya bunge kuhusu mradi huu, yanayosemwa ni zile taarifa za rasharasha ambazo kamati imezipata kutoka upande wa mafisadi wanaonufaika na mradi huo. Hivi mbona hakuna mjumbe hata mmoja aliyechangia ambaye ameshauri- mradi ule utekelezwe kwa uwazi kwa kutangaza tender makampuni yote duniani yabid? Wooote wanaishia kusema nundu asiingilie, nundu aache mradi uendelee......kuna nini ndani yake?

Afterall, we cant take seriously anything said by baadhi ya wabunge wetu kwasababu wametudhiirishia, inapokuja kwenye masuala ya pesa, hawapo objective. Hawa ndio juzi tu wameongwa kuanzia shilingi laki moja hadi milioni kuchagua watu kwenye Bunge la Afrika ya Mashariki.....wakafanya maamuzi ambayo yalikuwa na walakini. Ni hawahawa wabunge ambao walichukua mikopo ya CRDB bank recklessly, kisha wanatumia reason hiyo kudai waongezewe posho, kisa mshahara wao wote unakatwa kulipia deni la crdb...... Watu wa aina hii...akija mtu mwenye deal lenye cut ya usd 200, lazima waseme sana mpaka watokwe mapovu. Lakini ukweli unabaki pale pale......iitishwe tender, na kampuni yao ibid, tuone kama tutatozwa hizo usd 500 milioni.
 
Kitu rahisi kabisa ni hiki: Nundu atueleze his version of story, akatae kwa ushahidi kuwa hakwenda China na baadhi ya watu kwenye menejiment ya TPA - ila wakamkatalia kusaini mkataba *kumbuka nyaraka zipo zinazoshuhudia ukweli huo). Atupe faida ambazo Taifa litazipata endapo hiyo kampuni anayotaka ipewe hiyo kazi - binafsi sijawahi kumsikia Nundu akikanusha kuwa hana kampuni anayoipendekeza zaidi ya kutoa sweeping statements za "mambo yote ni uongo" lakini bila kutuonyesha ushahidi wa kupinga kinachoelezwa na kamati. Kama kamati imehongwa na inasema uongo bungeni YEYE ANASHINDWA NINI KUELEZA UKWELI BUNGENI???
 
Haujakosea hata kidogo. Kinachoonekana hapa ni genge la watu waliotibuliwa ulaji wao, sasa wanatumia loopsided article hii kumpaka matope Waziri Nundu aliyeonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yake kwa kukataa "deal" hii iliyo ghali kwa taifa. Inashangaza sana kwamba hata gazeti credible la raia mwema linatumika kupigia debe "deal" la kifisadi.

katika sakata hili yafuatayo ni mambo ya muhimu ya kuzingatia:
1) Upanuzi wa bandari ni jambo muhimu kutokana na demand ya soko na vile vile ushindani mkubwa kutoka bandari za nchi jirani hasa Bandari ya Mombasa (tunayoshindania soko la nchi za Afrika ya Mashariki) na bandari ya Walvis Bay ya Namibia (tunayoshindia soko la Zambia na DRC).

2) Financing ya Mradi wa upanuzi inatokana na mkopo (sio msaada) kutoka Exim Bank ya China. Hivyo kuchaguliwa mkandarasi wa kujenga mradi huo sio sahihi. Na sio kweli kwamba benki ya exim ya China imechagua mkandarasi, kwani hiyo sio shughuli yao na hawana utaratibu huo. Mara nyingi kampuni za ujenzi za china huwa zina lobby kazi barani afrika na kushauri nchi husika iombe mkopo kwa seriikali ya China Kupitia Exim Bank.

3)Record zinaonyesha hiyo china Exim Bank imekwishawahi kuikopesha Serikali ya Tanzania kwa ajili ya miradi mikubwa kama vile ujenzi wa mkonga wa taifa na nusu ya gharaka za ujenzi wa Uwanja mpya wa taifa na katika mkopo huo hawakutoa masharti wala ku recommend mkandarasi, badala yake utaratibu wa kawaida wa tender ulitumika ili kumpata mkandarasi mwenye sifa na mwenye kutoa value for money quotation. Hata katika miradi hiyo zilikuwepo kampuni zilizokuwa zinalobby wapewe kazi hiyo moja kwa moja kwasababu tu, wao ndio walitoa wazo la upanuzi wa mradi na kufanya feasibility study

4) Tatizo hasa ni nini? Tatizo hapa ni kwamba kampuni hii ya China inayopigiwa debe na Kamati ya Bunge, baadhi ya maafisa pale wizarani, Bodi na Menejimenti ya TPA, ime over-price mradi wenyewe kwa kudai usd 500 na ushei,jambo linalotoa hofu ya harufu ya rushwa. Pale Mombasa, wanafanya upanuzi kama huo unaotakiwa kufanyika kwenye bandari ya Dar es salaa,kwa usd 250 million. Kitendo cha kampuni hiyo ya China ku overprice mradi na wabunge na baadhi ya watendaji serikalini kushabikia, inapelekea hofu kwamba wamehongwa na kampuni ya kichina....na kwakweli sitoshangaa ukifanyika uchunguzi na ikathibitika kwamba wameongwa- maana kama wabunge wenyewe ndio hawa waliokubali kuongwa kuanzia shilingi laki moja hadi milioni ili kuchaguwa wawakilishi wa tanzania kwenye bunge la afrika ya mashariki,bila hata kujali uwezo,sifa na uzoefu wa waliowachagua, kwa deal ya aina hii inayozidi milioni 200 usd, lazima mashaka yawepo

5) Huko nyuma,niliwahi kusikia maelezo ya waziri Nundu kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV. Maelezo yake yana mantiki. Yeye anachosema kwakuwa pesa tuliyopata china ni mkopo unaokuwa guaranteed na pesa za walipa kodi, si vema kushabikia mradi kufanywa kwa zaidi ya mara mbili ya gharama halisi. Hivyo aliagiza deal ile isitishwe na tender itangazwe ili watu washindae badala ya huu utaratibu wa single sourcing uliogubikwa na mazingira ya rushwa. Bodi, memejimenti ya TPA kwakuwa ishaonja asali ya rushwa, walikaidi maagizo yake. Badala yake waka step-up lobbying kwa Kamati ya Bunge kwa kuwa induce na vijipesa, na misaada ya hapa na pale majimboni kwao- kamati nayo ikaanza kuimba nyimbo za kampuni hiyo inayopigiwa chapuo na mafisadi wa TPA.

6)Kwa maelezo ya waziri Nundu,baada ya kuona TPA hawatii agizo lake la kuitisha tender, alifanya ziara huko China, India na Dubai na kukutana na makampuni makubwa yenye uzoefu wa ku execute miradi mikubwa ya aina ile. Kwanza alitaka kupata ushauri wao kwa uzoefu waliokuwa nao mradi wa magnitude ya huu wa bongo,unaweza ku cost kiasi gani ( na wote walitoa makisio ya kati ya usd 250 hadi 340 milioni. Jambo la pili aliwakaribisha nchini wa bid kufanya kazi hiyo tender zitakapotangazwal kwa maoni ya Bw Nundu, hata kama serikali ishaingia makubaliano na china exim bank kukopa hizo milioni 500 na ushee....sawa tuzichukue,lakini mradi ule ufanywe kwa gharama halisi ambazo hazifiki milioni 500, na salio litumike kwenye miradi mingine kama vile kuendeleza bandari ya Tanga na Mtwara.

Hapo ndipo panapogomba. Watu wameingiliwa ulaji wao, sasa wanachofanya ni high-level lobbying kwa kutumia Kamati ya Bunge na supposedly credible newspaper kama Raia Mwema Ku distort ukweli halisi na kumchafua waziri nundu aondolewe pale ili deal liendelee. Hivi kama wabunge wamehongwa,media imehongwa....kimbilio la wananchi hapa litakuwa wapi? Kwakweli utamu wa chajuu kinachofikia usd 200 milions sawa na bilioni 340 za tanzania ni wizi wa mchana kabisa usiotakiwa kufumbiwa macho.

Waziri Nundu chapa kazi, usirudi nyuma.

umejitaidi kutoa mchanganuo mrefu ila wewe ndio umeongea kijazba na umeshindwa kutolea maelezo mambo yafuatayo

1. kama suala la exim na mutafuta mkandarasi lilitafutwa kwa uwazi tena chini ya waziri aliyepita na serikali ikashirikishwa na ikakubali kwa maandishi sidhan unaweza kusema wote hao waliousika ni mafisadi kwani mchakato haupingani na sheria ya manunuzi ya 2004.

2. umeshindwa kuelezea mamlaka gani ya kisheria waziri aliyokua nayo ya kutafuta mkandarasi na kuingia nae MOU hata kama hana interest yoyote na anataka kua mzalendo

3. waziri kama waziri ana utaalamu gani ktk ujenzi hadi kwenda kufata ushauri yeye mwenyewe kwa hao wakandarasi na kuja na figure ya kufikirika ambayo haijafanyiwa analysis yoyotre na yeye waziri akaichukua kama ndio credible value ya ujenzi

4. kama waziri aliyetoka alikua ana interest ange force iyo unayoiita deal ikamilike chini ya uwaziri wake mbona ameondoka na mchakato umeendelea, dela yoyote ya kifisadi inatokeaga wakat muhusika yuko madrakani na sivinginevyo!

5. haiwezekani serikali, kamati ya bunge, naibu mawazari, katibu mkuu, uongozi wa bandari wote wawe wezi eti yeye kawazri kamoja ndo kazalendo!
 
Back
Top Bottom