Waziri matatani; Sakata la upanuzi bandari - Alitaka kuwazunguka Mkulo na Dk. Kawambwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri matatani; Sakata la upanuzi bandari - Alitaka kuwazunguka Mkulo na Dk. Kawambwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 19, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sakata la upanuzi bandari


  Mwandishi Wetu


  [​IMG]


  WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu


  Wabunge wataka ang'oke, nyaraka zaanikwa
  Atofautiana na Naibu na katibu Mkuu wake
  Alitaka kuwazunguka Mkulo na Dk. Kawambwa


  WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu, sasa anasubiri huruma ya Rais Jakaya Kikwete kuendelea na uwaziri baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kupendekeza avuliwe nafasi hiyo, imefahamika.

  Kamati hiyo ya Bunge inamtuhumu Nundu kuhusika kukwamisha mradi mkubwa wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na kisha utetezi wake kushindwa kuishawishi kamati hiyo.

  Hatua hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inakuja baada ya mwishoni mwa wiki kukutana hapa na wahusika wa sakata hilo akiwamo Nundu na uongozi mzima wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Bodi yake, kufikia uamuzi wa kutaka Nundu apishe.


  Taarifa za suala hilo zinasema Kamati ilitaka maelezo kuhusiana na taarifa za kwamba Nundu amethubutu hata kukejeli maamuzi yaliyofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha, yakimhusisha Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na watendaji wengine wa Wizara ya Uchukuzi.


  "Nundu aliingia katika kikao na laptop yake bila ya kuwa na nyaraka zozote, wakati wabunge walikuwa na nyaraka na walipomhoji hakuwa na maelezo ya kuridhisha. Walimtaka aeleze ni kwa nini amefanya maamuzi kupingana na maamuzi yaliyokwisha kufanywa na Wizara yake na Wizara ya Fedha na pia walitaka kujua safari alizokwenda nje ya nchi zilikuwa na maslahi gani kwa nchi," anasema Mbunge mmoja aliyehudhuria kikao hicho.


  Katika kikao hicho, Mbunge mmoja ambaye amewahi kuwa waziri mwandamizi, alitoa mifano hai ya jinsi Serikali ilivyofanikisha miradi yake katika mtindo ambao Nundu anapingana nao, na akamuasa: "Mheshimiwa Waziri unapaswa kuangalia maslahi ya nchi kwanza."


  Awali katika kikao chao na Wabunge, Bodi na Menejimenti ya TPA ilitofautiana waziwazi na Waziri Nundu ikiorodhesha sababu nne za kumpinga Waziri Nundu pamoja na viambatanisho vinavyothibitisha sababu hizo.


  Gazeti hili limefanikiwa kuona nakala za nyaraka mbalimbali, ikiwamo viambatanisho kadhaa, kuhusu mvutano huo ambao unaonyesha kuwa Waziri Nundu ametofautiana hata na Naibu wake, Dk. Athumani Mfutakamba na Katibu Mkuu wake Omar Chambo.


  Kiini cha mvutano huo inaelezwa kuwa baada ya kuteuliwa kuwa Waziri ni kama amekuwa akivuruga mipango ya kimaendeleo iliyowekwa na Waziri aliyemtangulia, Dk. Shukuru Kawambwa, kuhusu upanuzi wa Bandari.


  Akiwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Kawambwa, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari, walitafuta mkopo kutoka Serikali ya China kupitia Benki ya Exim ya China iliyoridhia kutoa mkopo wa dola za Marekani takriban 524 ili zisaidie upanuzi wa gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam.


  Kinachogomba katika mvutano huo ni uamuzi wa Waziri Nundu kumkataa mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo ambaye, Benki ya Exim imependekeza ndiye awe mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo. Mkandarasi aliyependekezwa na Benki ya Exim ya China ili itoe mabilioni hayo kama mkopo ni kampuni ya huko huko China inayoitwa China Communications Construction Company (CCCC).


  Taarifa zinadai kwamba Waziri Nundu anadaiwa kuwa na mkandarasi wake ‘mfukoni' ambaye ni kampuni nyingine ya China inayoitwa China Merchants, ambayo aliamua kuingia nayo Mkataba wa Makubaliano (MOU), bila kuwahusisha watendaji wake na TPA. Wasaidizi wake wote waligoma kushirikiana naye na akalazimika kumfukuza mmoja wa wakurugenzi wake, ambaye sasa amehamia Wizara ya Ujenzi.


  "Waziri kwanza ameingia MOU na kampuni hiyo katika kipindi ambacho tayari Serikali imekwishakamilisha mchakato wa kupata fedha na kuanza kwa mradi. Cha kushangaza Waziri alipoulizwa alisema kampuni hiyo ilikuja Dar es Salaam na baadaye yeye kuwafuata China, lakini akashindwa kutoa maelezo ya kuhalalisha maamuzi yake," anasema Mbunge mwingine wa kamati hiyo.


  Kutokana na ‘nguvu' za kampuni hiyo inayopiganiwa dhidi ya CCCC, imeelezwa kuwa Serikali inaweza kukosa mkopo huo unaotajwa kuwa wa riba nafuu ili kampuni mpya iendeshe si ujenzi wa mradi tu, lakini baada ya mradi iendelee kumiliki utoaji huduma bandarini kwa kushirikiana na wadau wengine kwa mkataba wa miaka 45.


  Hali ilivyokuwa kabla ujio wa Nundu

  Mipango inadaiwa kuwa safi wakati wa Waziri Shukuru Kawambwa, ni wakati huo ambao TPA iliandikia Wizara ya Uchukuzi (wakati huo Wizara ya Miundombinu) kuelezea mapendekezo ya kupanua Bandari.

  Wizara iliafiki mapendekezo ya TPA na kuchukua hatua ambazo ni kuiandikia Wizara ya Fedha barua zenye zenye kumbukumbu namba CB 230/364/01/62 ya Aprili 14, 2010 na CCB 364/505/01/54 ya Julai 9, mwaka juzi (2010) ili ipate kibali cha kuomba mkopo kutoka Serikali ya watu wa China.


  Wizara ya Fedha iliunga mkono kuendeleza mchakato huo kwa kuomba mkopo Benki ya Exim ya China, kupitia barua yenye kumbukumbu namba TYC/450/2/02 ya Februari 22, mwaka jana na nyingine yenye kumbukumbu namba TYC/E/450/2/130 ya Novemba 9, mwaka jana pamoja na barua ya Januari 24, mwaka huu, yenye kumbukumbu namba TYC/E/450/2/02.


  Baada ya hapo, Wizara ya Fedha ilitaarifu Wizara ya Uchukuzi kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba TYC/E450/2/02 ya Agosti 22, 2011 kuhusu kuridhia kupatikana kwa mkopo na kushauri kuwa TPA iendelee na mchakato wa kupata mkopo husika.


  Kutokana na ‘kibali' hicho kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi ilitaarifu TPA kuendelea na mchakato wake wa kuomba mkopo kutoka Benki ya Exim.


  Sababu za kuomba mkopo

  Sababu za kuomba mkopo kwa ajili ya upanuzi huo wa gati za Bandari ya Dar es Salaam ni kwanza, mkopo utatolewa kwa Serikali ya Tanzania kwa masharti nafuu, ukiwa ni mkopo wa miaka 15 kwa riba ya asilimia mbili na kipindi cha mpito (grace period) ya miaka mitatu.

  Mkopo huo unatajwa kuwa nafuu kutokana na ukweli kwamba, mikopo kutoka vyanzo vingine ina riba isiyopungua asilimia 5.5 na muda wake wa kurejesha ni mfupi ukiwa kati ya miaka mitano hadi 10.


  Sababu ya pili ni kwamba, mkopo kutoka Serikali ya China una masharti nafuu na mradi utakuwa na faida kwa maelezo kwamba, gharama za ujenzi zimekadiriwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 12 baada ya mradi kukamilika na hivyo faida yote kubakia kwa Mamlaka ya Bandari.


  Sababu ya tatu ya kung'ang'ania mkopo huo inatajwa kuwa ni Serikali, baada ya ujenzi wa mradi itaweza kukodisha shughuli za biashara na kupata faida zaidi kutokana na TPA kuwa na uwezo wa kupanda kodi ya pango na mrabaha.


  Sababu hiyo ya tatu inapingana na matakwa ya Waziri Nundu ambaye anataka ujenzi uendeshwe na kampuni nyingine ambayo pia baada ya ujenzi kukamilika itaendesha biashara na kujifidia gharama za ujenzi kwa miaka zaidi ya 45.


  "Kama mradi huu utatekelezwa na kampuni binafsi, mwekezaji atahitaji kutumia gati kwa zaidi ya miaka 40 kabla ya kurejesha mikononi mwa Serikali. Kwa mfano, kampuni ya China Merchants imependekeza kujenga, kumiliki, kuendesha gati namba 13 na 14 kwa miaka 45.


  TPA yamuumbua Waziri mbele ya wabunge

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Menejimenti ya Bandari imewasilisha waraka kwa wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinuikieleza kutoridhishwa na Waziri Nundu kuhusu usimamizi wake katika mradi huo.

  Waraka huo unaeleza; "menejimenti imetathmini hoja za Waziri wa Uchukuzi na haikubaliani nazo zote kwa ujumla wake"


  Wanabainisha sababu za kutokukubaliana kuwa ni pamoja na; "Kampuni ya CCCC ilikuja kama mwekezaji wala si kama washauri (tofauti na anavyoeleza Waziri) na ilifanya upembuzi yakinifu kwa gharama zake na mradi huu unatakiwa kutekelezwa chini ya utaratibu wa Engineering Procurement and Construction (EPC) ambapo mwekezaji anatakiwa kufanya upembuzi yakinifu, usanifu (design) na kujenga.


  Wanaeleza pia kuwa sababu nyingine kuwa ni kampuni ‘zinazopiganiwa' na Waziri Nundu kwamba zitatekeleza mradi kwa gharama nafuu hazijathibitisha gharama halisi za mradi kwa sababu hazijafanya upembuzi yakinifu na kwamba gharama wanazotaja kuwa ni nafuu ni makisio tu.


  Wanaendelea kueleza kuwa, kinyume cha kauli ya Waziri Nundu kwamba Waziri wa Biashara wa China anaunga mkono uamuzi wake (Nundu), menejimenti haina ushahidi wa hilo na kwamba ushahidi uliopo kuhusu kampuni ya China Merchants Holdings anayoipigania Nundu waliwahi kutaka kujitoa katika mradi baada ya kubaini tayari Serikali ilianza mchakato na kampuni ya CCCC kwa kutumia fedha za Exim.


  "Pamoja na hayo, sheria ya manunuzi ya umma namba 21 ya mwaka 2004 inaelekeza chini ya kifungu cha 4 (1) cha sheria hiyo kukubaliana na masharti ya utekelezaji wa mkataba pale Serikali zinapokubaliana jinsi ya utekelezaji wa manunuzi ya mradi husika. Hivyo kukubaliana na masharti ya mkopo ulioombwa kutoka Exim hakukiuki sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004," unaeleza waraka huo.


  Mdau mmoja wa sekta ya bandari, alisema Waziri Nundu anapaswa kumpeleka mwekezaji anayemtaka kujenga bandari ya Mbegani, badala ya kulazimisha kumuingiza katika eneo la mradi ambalo tayari Serikali imekwisha kamilisha mchakato wake.


  Kwa miezi kadhaa sasa Raia Mwema limekuwa likiandika utata katika upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, suala ambalo Waziri Nundu amekuwa akilitolea ufafanuzi kwa jazba, hadi kufikia kutoa matangazo ya kutetea uamuzi wake huo na kukejeli taarifa zinazopingana naye.
   
 2. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii habari imekaa kiunazi sana. Yaani madudu yote haya, na mwandishi kashindwa hata kumsumbua waziri Nundu kumtaka ajieleze kuhusu kashfa hii? Kuna kitu hapa ambacho kimejificha. I hope we will find out soon.
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  tusubiri. kama si kweli atakanusha
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 809
  Trophy Points: 280
  Wamezidi wote watimuliwe au Rais awabadili maana Nundu alitaka Bandari ikajengwe Tanga
   
 5. s

  salaama JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 243
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Haujakosea hata kidogo. Kinachoonekana hapa ni genge la watu waliotibuliwa ulaji wao, sasa wanatumia loopsided article hii kumpaka matope Waziri Nundu aliyeonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yake kwa kukataa "deal" hii iliyo ghali kwa taifa. Inashangaza sana kwamba hata gazeti credible la raia mwema linatumika kupigia debe "deal" la kifisadi.

  katika sakata hili yafuatayo ni mambo ya muhimu ya kuzingatia:
  1) Upanuzi wa bandari ni jambo muhimu kutokana na demand ya soko na vile vile ushindani mkubwa kutoka bandari za nchi jirani hasa Bandari ya Mombasa (tunayoshindania soko la nchi za Afrika ya Mashariki) na bandari ya Walvis Bay ya Namibia (tunayoshindia soko la Zambia na DRC).

  2) Financing ya Mradi wa upanuzi inatokana na mkopo (sio msaada) kutoka Exim Bank ya China. Hivyo kuchaguliwa mkandarasi wa kujenga mradi huo sio sahihi. Na sio kweli kwamba benki ya exim ya China imechagua mkandarasi, kwani hiyo sio shughuli yao na hawana utaratibu huo. Mara nyingi kampuni za ujenzi za china huwa zina lobby kazi barani afrika na kushauri nchi husika iombe mkopo kwa seriikali ya China Kupitia Exim Bank.

  3)Record zinaonyesha hiyo china Exim Bank imekwishawahi kuikopesha Serikali ya Tanzania kwa ajili ya miradi mikubwa kama vile ujenzi wa mkonga wa taifa na nusu ya gharaka za ujenzi wa Uwanja mpya wa taifa na katika mkopo huo hawakutoa masharti wala ku recommend mkandarasi, badala yake utaratibu wa kawaida wa tender ulitumika ili kumpata mkandarasi mwenye sifa na mwenye kutoa value for money quotation. Hata katika miradi hiyo zilikuwepo kampuni zilizokuwa zinalobby wapewe kazi hiyo moja kwa moja kwasababu tu, wao ndio walitoa wazo la upanuzi wa mradi na kufanya feasibility study

  4) Tatizo hasa ni nini? Tatizo hapa ni kwamba kampuni hii ya China inayopigiwa debe na Kamati ya Bunge, baadhi ya maafisa pale wizarani, Bodi na Menejimenti ya TPA, ime over-price mradi wenyewe kwa kudai usd 500 na ushei,jambo linalotoa hofu ya harufu ya rushwa. Pale Mombasa, wanafanya upanuzi kama huo unaotakiwa kufanyika kwenye bandari ya Dar es salaa,kwa usd 250 million. Kitendo cha kampuni hiyo ya China ku overprice mradi na wabunge na baadhi ya watendaji serikalini kushabikia, inapelekea hofu kwamba wamehongwa na kampuni ya kichina....na kwakweli sitoshangaa ukifanyika uchunguzi na ikathibitika kwamba wameongwa- maana kama wabunge wenyewe ndio hawa waliokubali kuongwa kuanzia shilingi laki moja hadi milioni ili kuchaguwa wawakilishi wa tanzania kwenye bunge la afrika ya mashariki,bila hata kujali uwezo,sifa na uzoefu wa waliowachagua, kwa deal ya aina hii inayozidi milioni 200 usd, lazima mashaka yawepo


  5) Huko nyuma,niliwahi kusikia maelezo ya waziri Nundu kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV. Maelezo yake yana mantiki. Yeye anachosema kwakuwa pesa tuliyopata china ni mkopo unaokuwa guaranteed na pesa za walipa kodi, si vema kushabikia mradi kufanywa kwa zaidi ya mara mbili ya gharama halisi. Hivyo aliagiza deal ile isitishwe na tender itangazwe ili watu washindae badala ya huu utaratibu wa single sourcing uliogubikwa na mazingira ya rushwa. Bodi, memejimenti ya TPA kwakuwa ishaonja asali ya rushwa, walikaidi maagizo yake. Badala yake waka step-up lobbying kwa Kamati ya Bunge kwa kuwa induce na vijipesa, na misaada ya hapa na pale majimboni kwao- kamati nayo ikaanza kuimba nyimbo za kampuni hiyo inayopigiwa chapuo na mafisadi wa TPA.

  6)Kwa maelezo ya waziri Nundu,baada ya kuona TPA hawatii agizo lake la kuitisha tender, alifanya ziara huko China, India na Dubai na kukutana na makampuni makubwa yenye uzoefu wa ku execute miradi mikubwa ya aina ile. Kwanza alitaka kupata ushauri wao kwa uzoefu waliokuwa nao mradi wa magnitude ya huu wa bongo,unaweza ku cost kiasi gani ( na wote walitoa makisio ya kati ya usd 250 hadi 340 milioni. Jambo la pili aliwakaribisha nchini wa bid kufanya kazi hiyo tender zitakapotangazwal kwa maoni ya Bw Nundu, hata kama serikali ishaingia makubaliano na china exim bank kukopa hizo milioni 500 na ushee....sawa tuzichukue,lakini mradi ule ufanywe kwa gharama halisi ambazo hazifiki milioni 500, na salio litumike kwenye miradi mingine kama vile kuendeleza bandari ya Tanga na Mtwara.

  Hapo ndipo panapogomba. Watu wameingiliwa ulaji wao, sasa wanachofanya ni high-level lobbying kwa kutumia Kamati ya Bunge na supposedly credible newspaper kama Raia Mwema Ku distort ukweli halisi na kumchafua waziri nundu aondolewe pale ili deal liendelee. Hivi kama wabunge wamehongwa,media imehongwa....kimbilio la wananchi hapa litakuwa wapi? Kwakweli utamu wa chajuu kinachofikia usd 200 milions sawa na bilioni 340 za tanzania ni wizi wa mchana kabisa usiotakiwa kufumbiwa macho.

  Waziri Nundu chapa kazi, usirudi nyuma.
   
 6. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ndugu, habari za mida hii.

  Kuna sheria - yani maagizo ya lazima ya nini cha kufanya na usipofanya kinakukuta nini - inapotokea serikali inataka kutumia hela kuajiri mtu kufanya kazi ya serikali. Sawa?

  Sasa ni kwa nini Waziri hapa na Kamati ya Bunge na TPA na Raia Mwema na wewe mnavutana kuhusu nini cha kufanya kumpata contractor. Kwa nini? Hakuna Sheria ya Manunuzi ya Umma?
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Yaani zogo lote hilo zilizokopwa Exim Bank ya China ni chini ya dola 600 ?!

  Wahariri mpo?
   
 8. Ngatele

  Ngatele JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nafikiri bank ya ya exim haina power ya kuchagua mkandarasi isipokuwa ni kuwa financier tu. TPA walipaswa kumtafuta mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi, kufanya design na kuandaa tender document and then TPA ingetangaza tender na wazabuni watakaojitokeza wangeshindanishwa na zabuni zao kuchambuliwa na hatimaye anayestahili angepewa zabuni hiyo. OR, kama hakuna financing ya mradi, katika tender document lingewekwa sharti kuwa mzabuni atatakiwa kuonesha financing plan yake kwa kwa kusubmit bank ambayo inaweza ikatoa mkopo na kiasi cha riba pamoja na miaka ya mkopo na TPA pamoja na kuchambua vigezo vingine ingetazama hiyo financing plan kama inaunafuu kwa mradi husika.
   
 9. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Pesa za mkopo tayari watu wanaanza kutoana ngeu! Kweli TZ ni zaidi ya ninavyoifahamu.
   
 10. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  i
  Kamma namuon mzee wa kutokwa povu.natumaini atajibu hii thread coz ni member humu.
  Mytake:
   
 11. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Keshajibu
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Naona kuna harufu ya kupakana matope watu wametibuliwa ulaji wao sasa wanapaka matope. Ni vema tuambiwe terms of loan za mkopo Exim kwanza? Mchakato wa kupatikana hiyo kampuni ya mwanzo ya ujenzi na mkandarasi zilikuwa vipi na kwanini waziri Nundu aliamua kuweka ngumu kumkataa. Inabidi uzalendo uwepo binafsi nimekosa imani na wabunge wetu ambao wanaomba rushwa hadi kwa wagombea ubunge wa East Africa. Siwaamini hata kidogo tunaomba ufafanuzi zaidi tufahamu mbichi zipi na mbivu zipi.
   
 13. B

  Baba theo New Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tunahitaji ufafanuzi zaid inawezekana kila m2 kati yao anamasilai yake but nundu asililizwe then 2jue yupi mkweli na ana2penda watanzania kiasi zaidi kati yao but cjui watanzania 2taponea wapi na huuu ukisasa wao ambao ni ufisadi wa kutisha.
   
 14. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Atoe maelezo yake bungeni kama anadhani kamati ya bunge imehongwa na atupe faida tutakayopata kampuni yake ya mfukoni ikipewa hiyo kazi. By the way, wapi alishasema gharama ya mradi itapungua kampuni ayoitafuta yeye ikipewa mradi?
   
 15. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,353
  Trophy Points: 280
  Ndipo credibility ya huyu mtetezi inapo anzisha mashaka, pengine kuna ukweli kwenye maelezo yake lakini bila ya kusema hiyo kampuni inayotetewa itajenga kwa shillingi ngapi ni hadithi zilezile especially kwakua mkopo wanaoutaka ni ule ule. Kwa mwenendo wa viongozi wetu who is to stop him from embezzling the leftovers.

  Jamii imeshapoteza imani na uzalendo wa viongozi wetu. Kwa hivyo amna sababu ya kuchukua cha ziada kama kunauwezekano wa kufanya project at hand for less.Huyu bwana kesha anza usiri usiri na hasira juu inavyoonekana kuna msuguano wa maslahi kati ya wachina kwa wachina na waroho kwa waroho (viongozi wa serikali na wabandari).

  Mwisho wa siku hao contractors hanao wataka waziri wameshafanya kazi wapi maana atleast hao wengine kazi zao zipo na zinajulikana so far. Isije ikawa less money translates to poor quality.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nchi yetu itajengwa na wale wanaoitakia mema. Jamani Bandari ya Dar haiwezi kupanuliwa kuongeza ufanisi zaidi ya kutumia fedha zaidi ktk Ufisadi. Kwa nini inakuwa vigumu sana kwa viongozi wetu kupeleka maendeleo sehemu nyinginezo. Tunazo Bandari za Tanga na Mtwara, hizi mbona zinakufa badala ya kuboreshwa zikaweza kuifanya kazi kubwa kwa miaka 50 ijayo?.. Bandari ya Dar ifungwe kwa kupokea mizigo ibakie bandari ndogo ya meli za watalii kama cruisership, Yatch club na mji wa kisasa wenye Ofisi na Condominium ambazo zitaongeza pato la Halmashauri kutokana na pango... Hadithi kwisha.
   
 17. s

  salaama JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 243
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60


  Nadhani kama umesoma sawasawa nilichoandika, na sio kilichotungwa na kuwa published kwenye gazeti ku distort ukweli, ni kwamba Nundu anachotaka itangazwe tender kwa uwazi na makampuni yote duniani yawe huru ku bid kwa kazi hiyo. Ile habari ya kwamba kuna kampuni ya China Nundu anaipigia debe, ni habari ya kupikwa na lile genge la wezi lililojipanga kwa gharama yoyote ile kuhakikisha deal yao inapita.

  Mtoboa siri kwenye respi
   
 18. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Watu hawa wa upande wa pili huwa siwaamini hata kidogo kutokana na ubinafsi wao. Hivi ingekuwa ni mpango wa kupanua bandari ya Unguja, angeweka kauzibe? Atemeshwe mzigo huyo apige mbizi kurudi kwao.
   
 19. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,353
  Trophy Points: 280
  Ok ume-eleweka lakini utata unabakia palepale kwanini uombe mkopo baada ya kupata estimation na kuzikubali. Halafu baadae mnasema hawa wa sasa wanagharama kubwa embu kwanza tuweke tender hadharani, wakati huo huo mnatuamibia mkopo au ambatani na tenda. Na kwanini mambo yasingeenda the other way round kutafuta hizo tenda halafu ndio mkopo uoni utata hapa. Ina maana pengine watu walisha jua estimation halisi sasa tena wanataka kuzungukana wenyewe kwa wenyewe ndio inakuwa public issue maana hela hipo njiani sasa.
   
 20. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,646
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Kama kawa shamba la bibi hakuna lawama napita tu !
   
Loading...