Waziri Masha afichua siri


BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,436
Likes
117,316
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,436 117,316 280
Waziri Masha afichua siri

na Peter Nyanje
Tanzania Daima


RIPOTI ya Kamati ya Kupitia Mikataba ya Madili iliyoongozwa na aliyepata kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Lawrence Masha, imeanika udhaifu wa Kitengo cha Madini katika wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika kusimamia na kuratibu sekta ya madini nchini.

Ripoti ya Kamati ya Masha inasema ushahidi uliotolewa na Alex Stewart (Assayers) Government Corporation, unaonyesha dhahiri kuwa uwezo wa TRA ni mdogo katika masuala ya madini kwa kuwa haina wafanyakazi wa kutosha na wenye ujuzi mpana wa kunyambulisha taarifa za fedha za kampuni za madini.

Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ambayo Tanzania Daima imeiona, suala la udhaifu wa Kitengo cha Madini katika wizara, lilishabainishwa katika ripoti ya Kamati ya Dk. Kipokola.

Kamati ya Dk. Kipokola iliainisha udhaifu wa kitengo hicho katika masuala ya muundo wake, uwezo, uratibu na mawasiliano na idara nyingine za serikali.

"Ripoti ya Dk. Kipokola inabainisha kuwa muundo wa kitengo cha madini uliopitishwa mwaka 2001 hauendani na matakwa ya sekta hii ambayo inakuwa kwa kasi," inasema sehemu ya ripoti ya Kamati ya Masha, ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ripoti hiyo inarejea uzoefu ulioonekana katika nchi za Botswana na Ghana na kueleza mathani kuwa nchini Botswana, kuna Kitengo cha Uchumi wa Madini, ambacho jukumu lake kubwa ni kulinda maslahi ya nchi kwa kuratibu kwa karibu shughuli za uchimbaji madini.

"Nchini Ghana, kipo kitengo ambacho kazi yake kubwa ni kufuatilia kwa karibu gharama za miradi mikubwa ya uchimbaji madini," inasema ripoti hiyo.

Kutokana na masomo hayo, tayari mapendekezo yalishafikishwa serikalini kuhusiana na umuhimu wa kukifanyia kitengo hicho mabadiliko, lakini kwa mujibu wa ripoti ya Kamati ya Masha, utekelezaji wa mapendekezo hayo unategemea sana mafunzo kutoka Botswana.

Kuhusu TRA, ripoti hiyo inasema kuwa ripoti iliyoandaliwa na Alex Stewart (Assayers) Government Corporation, manunuzi kutoka nje yaliyofanywa na kampuni za madini hayakuchunguzwa ipasavyo na Idara ya Ushuru wa Forodha kuhusu idadi, aina na thamani ya vifaa vilivyoagizwa ambavyo vinastahili kusamehewa ushuru.

Inabainishwa pia katika ripoti hiyo kuwa, ukaguzi wa kina katika maeneo ya machimbo ulifanyika mara chache sana kabla masuala ya kampuni za madini hayajahamishwa kutoka Idaya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Mapato na kupelekwa Idara ya Walipoa Kodi Wakubwa.

"Kodi zilikadiriwa kutokana na ukaguzi uliofanyika ofisini tu. Ziara ya maeneo ya machimbo zilifanywa kwa ajili ya marejesho ya VAT na kodi ya zuio," inabainisha ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasema kuwa Alex Stewart ilibaini kuwepo kwa uwezo mdogo katika ngazi mbalimbali ndani ya TRA kuratibu shughuli za kampuni za kuchimba madini.

"Kwanza TRA ilitakiwa iwe na udadisi wa hali ya juu kuhusu biashara na taarifa za fedha zinazowasilishwa na kampuni za madini… kuna uwezekano kuwa TRA haina watu wenye maarifa maalum kunyambulisha shughuli za kampuni za madini," inasema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa, kuna masuala ambayo TRA ilitakiwa iyabaini mapema kama vile muendelezo wa kukosekana kwa nyaraka kadhaa.

"Kuna ushahidi wa dhahiri wa dhamira ya kupotosha pale wadau wawili katika mradi wanapotoa taarifa mbili tofauti za fedha kuhusu shehena moja ya dhahabu iliyosafirishwa nje," inasema ripoti hiyo.

Ikiweka wazi, ripoti inataja tukio ambalo kampuni mbili zilizoungana katika mradi mmoja wa madini, zilidanganya kuhusu mapato ya mauzo ya dhahabu kwa pungufu ya dola za Marekani 2,340,000 kati ya mwaka 2001 na 2003.
 
M

Morani75

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2007
Messages
619
Likes
2
Points
0
M

Morani75

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2007
619 2 0
Salaam.... Hii kazi nimekuwa naifuatilia haswa baada ya kusikiliza muziki aliotuletea Invisible juma lililopita... Sasa ninavyojaribu kuweka mambo sawasawa nagundu kwamba kijana mwenzetu Mhe Masha alikuwa sawa toka mwanzo lakini kulinda maslahi ilibidi apelekwe kuhesabu "Pasipoti" asichafulie wazee mamboz yao.... Duh, hii ni kazi kwelikweli....

Kwa wale wamjuao Masha tulipata wasiwasi manake mengi yalisemwa kumbe jamaa alikuwa msemakweli.... Bravo Laurance Masha - Keep up the Good work of keeping us the YOUTH of Tanzania "New Blood" PROUD!!!
 
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
249
Likes
4
Points
0
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
249 4 0
Kwa wataalam wa kuangalia nyuso za wanadamu unaweza kukiri kuwa huyu kijana mwenzetu Laurent wa Masha ni muungwana fulani,hajatawaliwa na mapompo ya mafanikio ya maisha yake wala wale waliomzunguka.

He is somebody for Tz;
Kama unatembelea humu naomba uyasome maneno ya mkongwe huyu naiwe ndiyo dira yako ktk maisha ya siasa"Every gun that is made, every warship that is launched, every rocket fired signifies in the final sense a theft from those who hunger and are not fed, those who are cold and not clothed" – Eisenhower

Keep it up Hon Masha
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
61
Points
145
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 61 145
Ukisoma hizo reports iko clear tatizo liko kwenye kodi ingawaje watanzania wengi tumeng'ang'ania kwenye sheria mbaya za madini.

Sheria zetu nyingi za kukusanya kodi ni mbaya, pia hakuna wataalamu wengi wenye uwezo na mbinu mbalimbali za kuwanasa wakwepa kodi.

Hata tuje na sheria gani, kwa utaratibu wa sasa wa TRA hakuna kitu.

Ma Engineers tunasema garbage in garbage out, sasa kama hao TRA
wanachojua ni kupambana na biashara za Machingas, kweny hawa mafia wa dunia hawawezi kitu.
 
K

KakindoMaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2006
Messages
1,351
Likes
58
Points
145
K

KakindoMaster

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2006
1,351 58 145
Ukisoma hizo reports iko clear tatizo liko kwenye kodi ingawaje watanzania wengi tumeng'ang'ania kwenye sheria mbaya za madini.

Sheria zetu nyingi za kukusanya kodi ni mbaya, pia hakuna wataalamu wengi wenye uwezo na mbinu mbalimbali za kuwanasa wakwepa kodi.

Hata tuje na sheria gani, kwa utaratibu wa sasa wa TRA hakuna kitu.

Ma Engineers tunasema garbage in garbage out, sasa kama hao TRA
wanachojua ni kupambana na biashara za Machingas, kweny hawa mafia wa dunia hawawezi kitu.
Mzee hivi kweli hatuna wataalamu au hao TRA pesa za kujenga majumba yao zinatoka wapi?

Je siyo kwamba ni Rushwa ndio inatuangusha? Juzi juzi nilisikia kuwa kuna watu TRA wanaweza kujenga golofa hata Tano kwa mpigo. Je hizo pesa ni mishahara au ni nini? Je siyo pesa wanazoachia na kuzunguka mbuyu?
 
M

Morani75

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2007
Messages
619
Likes
2
Points
0
M

Morani75

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2007
619 2 0
KakindoMaster, ukweli kwa nijuavyo mimi, pamoja na rushwa lazima tukubali kwamba pale TRA kidogo pana "Hitilafu" especially kwenye "Qualifications".... Nimeshaona siku moja kuna jamaa tulikuwa tunapambana maswala ya "Taxation - VAT". Basi bwana yule Assessor alipata shida sana kuona "Provissional Sum" kwenye bid document and kutushupalia kwamba lazima tulipie "Tax".... Aligoma kuelewa kwamba "PS" wakati wa tendering can be billions but in actual life ni kidogo tu inaweza tumika au istumike kabisa.... Hapo sasa fikiria ndugu yangu huo ni mfano mmoja kwangu sijui mengine mengi kwa wengine......
Sisemi hawajui lakini nasema "KUNA MUSHKELI MAHALA PALE - PROFESSIONALLY, degree is the difference!!!"

Naomba kuwakilisha.....
 
Bowbow

Bowbow

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2007
Messages
545
Likes
12
Points
0
Bowbow

Bowbow

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2007
545 12 0
Sidhani kama TRA hakuna utalaam, Rushwa, Rushwa, na kisheria tax avoidance is legal, but tax avation is ilegal.

Ila kama kweli TRA hakuna hao wataalam haina maana hawapo Tanzania ni kwa sababu ya Rushwa na undugunazation ndio maana watu competent hawaajiri.

TRA ni ofisi inahitaji reshufle kubwa kuliko hata wizarani.
Pamoja na kuwa na sera mbaya za kodi bado pia kuna sheria mbaya za madini so zote zinahaitaji kurekebishwa
 
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2006
Messages
6,613
Likes
883
Points
280
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2006
6,613 883 280
TRA inao wataalamu wa kutosha, tatizo tulilonalo ni wanasiasa. Mfano rahisi sana ni huu wa kutumia sheria mbili tofauti za kodi ya mapato. Ile iliyokwisha futwa (Income tax act 1973) kwa baadhi ya hawa wanaoitwa wawekezaji na sheria halali (Income tax act 2004) kwa kundi lingine. TRA wanajua kuwa kuendelea kutumia sheria ambayo haipo ni ukiukwaji wa utawala wa kisheria, wanajua pia kuwa ukiukwaji huu haukutokea kwa bahati mabaya. Ni mpango wa wakubwa ambao ni vigumu kuwaaminisha TRA kuwa haukutokana na rushwa. Sasa TRA wanapokuwa kuwa na convincing reasons kuwa wakubwa wamevuta wewe unataraji wao wafanyeje ? Hii misamaha ya kodi ya mafuta kwenye migodi isiyo na ukomo inatoa picha gani kwa ndugu zetu wa TRA! Ukiweza kudhibiti juu, chini kazi inakuwa nyepesi sana.
 
Mkereketwa

Mkereketwa

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2007
Messages
202
Likes
1
Points
0
Mkereketwa

Mkereketwa

JF-Expert Member
Joined May 19, 2007
202 1 0
Hapo hakuna cha TRA wala sheria mbovu za madini. Tanzania nikichwa cha mwendawazimu tu hata tungefanya nini, hakuna suruhisho.

Yaani hapa naongea kwa hasira hata point zimetoweka
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
61
Points
135
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 61 135
Naamini kuwa Masha na wengine walijua toka mwanzo. Lakini naona hali kama hiyo kuachwa kama ilivyo ni kama makusudi, kuna watu wananufaika na hali hiyo, kama ikirekebishwa taifa litanufaika zaidi kuliko wao, na hawapendi ndio maana wakaona wampeleke jamaa kuhesabu Pasipoti!
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
61
Points
145
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 61 145
Sidhani kama TRA hakuna utalaam, Rushwa, Rushwa, na kisheria tax avoidance is legal, but tax avation is ilegal.

Ila kama kweli TRA hakuna hao wataalam haina maana hawapo Tanzania ni kwa sababu ya Rushwa na undugunazation ndio maana watu competent hawaajiri.

TRA ni ofisi inahitaji reshufle kubwa kuliko hata wizarani.
Pamoja na kuwa na sera mbaya za kodi bado pia kuna sheria mbaya za madini so zote zinahaitaji kurekebishwa
Unafikiri TRA wanakula rushwa kwa hao wazungu? Labda akina Karamangi, TRA wanawezana na sisi Wadanganyika au akina Mohamed Enterprises. Kwa hao Wacanada, TRA kigugumiza kinaingia.

Mnaweza msikubali lakini ndio ukweli, wana elimu ya kutosha general lakini sio ambayo inatakiwa kwenye uchambuzi wa miradi kama hiyo ya madini.

Si unajua hata huku majuu, hawa watu nwa kodi wanachemsha inapokuja kuwabana mashirika makubwa? Ila huku wajanja kila siku wanagundua mianya na kuziba, hapo TZ inachukua miaka kugundua tatizo na miaka kulirekebisha wakati huo tayari mgodi unafilisika.

Hata kwa sheria hizo hizo zilizopo, ilitakiwa tuweze kukusanya kodi ya maana lakini ndio hiyo, hata hao Wazungu wakaguzi wamegundua kitu ambacho baadhi ya watu wanasema muda mrefu. Tofauti tu ni kwamba hao wazungu wamelipwa mamilioni kutayarisha hiyo report ambayo hakuna kilichofanyika kuifanyia kazi.
 
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Messages
11,377
Likes
3,099
Points
280
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2007
11,377 3,099 280
Sawasawa, tushagundua shida ilipo!
Tufanye nini sasa?
 
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2007
Messages
2,941
Likes
286
Points
180
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2007
2,941 286 180
Salaam.... Hii kazi nimekuwa naifuatilia haswa baada ya kusikiliza muziki aliotuletea Invisible juma lililopita... Sasa ninavyojaribu kuweka mambo sawasawa nagundu kwamba kijana mwenzetu Mhe Masha alikuwa sawa toka mwanzo lakini kulinda maslahi ilibidi apelekwe kuhesabu "Pasipoti" asichafulie wazee mamboz yao.... Duh, hii ni kazi kwelikweli....

Kwa wale wamjuao Masha tulipata wasiwasi manake mengi yalisemwa kumbe jamaa alikuwa msemakweli.... Bravo Laurance Masha - Keep up the Good work of keeping us the YOUTH of Tanzania "New Blood" PROUD!!!
..jamaa bado ni kijana,hivyo ana ngwe ndefu mbele,akiharibu sasa,hatofika mbali!

..it's in his own interest!
 
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2007
Messages
2,941
Likes
286
Points
180
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2007
2,941 286 180
Ukisoma hizo reports iko clear tatizo liko kwenye kodi ingawaje watanzania wengi tumeng'ang'ania kwenye sheria mbaya za madini.

Sheria zetu nyingi za kukusanya kodi ni mbaya, pia hakuna wataalamu wengi wenye uwezo na mbinu mbalimbali za kuwanasa wakwepa kodi.

Hata tuje na sheria gani, kwa utaratibu wa sasa wa TRA hakuna kitu.

Ma Engineers tunasema garbage in garbage out, sasa kama hao TRA
wanachojua ni kupambana na biashara za Machingas, kweny hawa mafia wa dunia hawawezi kitu.
..akili ya kukusanya kodi vizuri,tutaipata pale tutakapoacha kutegemea misaada ya fedha kwenye bajeti yetu!

..it's this simple kuwa,kama unapewa chakula kidogo na mtu,kwanini uhangaike kulima sana!chakula si kinatosha,angalau kukufanya uishi!
 
Halisi

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Messages
2,812
Likes
98
Points
145
Halisi

Halisi

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2007
2,812 98 145
Kwa hii ripoti nampongeza sana Masha, ameonyesha kwamba akipewa nafasi anaweza... na si yeye tu, vijana wengi wakipewa nafasi wanaweza... Pamoja na kuwa huko IMMA alikokua kuna mambo yanahitaji mjadala zaidi
 
Invisible

Invisible

Admin
Joined
Feb 11, 2006
Messages
9,104
Likes
602
Points
280
Invisible

Invisible

Admin
Joined Feb 11, 2006
9,104 602 280
Kwa hii ripoti nampongeza sana Masha, ameonyesha kwamba akipewa nafasi anaweza... na si yeye tu, vijana wengi wakipewa nafasi wanaweza... Pamoja na kuwa huko IMMA alikokua kuna mambo yanahitaji mjadala zaidi
Miaka miwili imepita...
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,349
Likes
8,708
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,349 8,708 280
..Masha anawa-quote Alex Stewart kana kwamba walifanya kazi ya maana.

..wakati huohuo serikali inawashitaki Basil Mramba na Daniel Yona kwa kuitia hasara serikali kutokana na uamuzi wao wa kuwaajiri Alex Stewart.
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
92
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 92 0
- Unajua nilishituka kweli nilipoona hii topic, kumbe ni ya Mwaka 2007! Duh!

Respect.

FMEs!
 

Forum statistics

Threads 1,235,878
Members 474,779
Posts 29,239,300