Waziri Masele asema hakuna kanuni zilizotungwa kuendesha sheria mpya ya kusitisha fao la kujitoa.

elimsu

Member
Aug 27, 2010
31
3
Jana trh 02/08/2012 SSRA walitoa tangazo kupitia gazeti la Daily news na website yao wakiuarifu umma kwamba fao la kujitoa limesitishwa kufuatia sheria iliyosainiwa na Rais mwezi June 2012. Kwa uelewa wangu nina mawazo kwamba tangazo hilo ni batili kwani mpaka sasa kwa utafiti niliyoufanya hakuna mwongozo/kanuni wa matumizi ya sheria hiyo(Regulation) kuhusu matumizi ya hiyo sheria mpya hakuna GN (Government Notice) iliyotangaza matumizi ya hiyo regulation.

Kisheria, hakuna sheria yoyote itakayoweza kufanya kazi kama hakuna mwongozo wa sheria hiyo. Mf mpaka sasa sheria inayokataza uvutaji sigara hadharani haina nguvu wala hakuna mtu hata mmoja aliyeshitakiwa kwa kosa hilo kwa sababu hakuna mwongozo wa matumizi ya sheria hiyo. kukosekana kwa mwongozo wa sheria hiyo mpya ya kusitisha fao la kujitoa imethibitishwa pia na Naibu waziri wa nishati na madini Mh. Steven Masele jana Bungeni. Namnukuu

''Katika hatua nyingine, maselealiwataka wafanyakazi wa migodi waliogoma kupinga sheria ya Mifuko ya Hifadhi za jamii kurejea kazini akifafanua kuwa, kanuni zinazoendesha sheria hizo hazijatungwa'' (source mwananchi trh 03/08/2012 at pg 2)

SSRA wapetata wapi nguvu ya kuanza kutumia sheria angali kanuni zinazoendesha sheria hiyo hazijatungwa
? SSRA walitakiwa wasubiri mpaka hapo kanuni zitakapotungwa ndipo waanze kutoa matamko. matamko yao kwa umma ni batili kama sio premature. Walichofanya SSRA sio sahihi kabisa na ni upotoshaji. Hii mifuko ya hifadhi ya jamii inaweza kuendelea na utaratibu wa awali kwani bila kujali tangazo la SSRA kwani tangazo lenyewe halina nguvu ya kisheria na halijafuata utaratibu. Labda swali la kujiuliza ni je waziri husika amechukua hatua gani kuhusu hili tangazo?


Naomba kuwakilisha
.



 
hapo ndio pazuri,SSRA Wamekurupuka sana.nafikiri wameanza vibaya na hoja wanazotoa ni ovyo kabisa.
 
Tunaviongozi basi, wapo kimaslahi zaidi na si kuwatumikia watu. Huyo Steven alikuwa wapi muda wote hadi makampuni makubwa yanaanza kula hasara na hatujui pengine kuna watu walishapoteza maisha kwa presha kutokana na uzembe wa kutokutoa ufafanuzi mdogo kama huu. Kuanzia waziri wa fedha, utumishi wa umma, utawala bora na sekta zingine sioni kama wakiguswa na hii sheria mpya. Hawana shida na wananchi, I don't know they working for whom one!!
 
Muogo huyu nia yake wafanyakazi warudi kazini, hakuna kingine.

Mbona bunge halikukataa kuwa hawajapitisha hiyo sheria na badala yake Spika akaunda tume ya kuongea na kupata maoni ya Wafanyakazi.

Nina mashaka huenda siku hii sheria wanaipitisha pale Bungeni huyu Waziri Masele hakuwepo au alikuwa

amelala usingizi Bungeni kama hawa wenzie:-


View attachment 60697
View attachment 60698
View attachment 60699

Je, mnategemea atasikiliza kinachojadiliwa Bungeni, mwisho akiamka anakuta wenzie wanapiga kura ya kukubali hoja au kukataa; na yeye anajibu "NDIOOOOOOOOOOOOOO"


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mbona ufafanuzi umeshatolewa
1. Wamesitisha kwa miezi 6 wakati wakiandaa utaratibu mpya
2. Waliojitoa kabla ya tarehe 20 julai 2012 watalipwa
my take: kwa nini wasiendelee kuandaa utaratibu mpya huku ule wa zamani ukiendelea. Kwa nini wasitishe kwanza?
 
Mbona ufafanuzi umeshatolewa
1. Wamesitisha kwa miezi 6 wakati wakiandaa utaratibu mpya
2. Waliojitoa kabla ya tarehe 20 julai 2012 watalipwa
my take: kwa nini wasiendelee kuandaa utaratibu mpya huku ule wa zamani ukiendelea. Kwa nini wasitishe kwanza?

Kwa sababu hawana hela kwa hiyo wanachangishachangisha hii miezi sita.......kama daladala lililopigwa bao na trafiki na kukosa hesabu ya bosi
 
Dhaifu....walikuwa wanajaribu kumbe waajiriwa siyo mazoba kama wanaowapigia kura....wamezoea kuwadanganya na ahadi za rais wawape kura halafu wanawatosa. Jaribuni kuleta hii sheria tuwamalize...chezea waliosoma wewe?////
 
Mbona ufafanuzi umeshatolewa
1. Wamesitisha kwa miezi 6 wakati wakiandaa utaratibu mpya
2. Waliojitoa kabla ya tarehe 20 julai 2012 watalipwa
my take: kwa nini wasiendelee kuandaa utaratibu mpya huku ule wa zamani ukiendelea. Kwa nini wasitishe kwanza?

Duh hii nayo mbona hatari? Hii taarifa umeipata wapi?
 
Back
Top Bottom