WAZIRI MASELE ananikosha.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WAZIRI MASELE ananikosha..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theHAVARD_product, Jul 14, 2012.

 1. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa huyu jamaa ,na siku hadi siku anzidi kuonesha Kile kitu ambacho hakijafanywa miaka mini cheki hii ya KARIBUNI.


  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele ameiamuru kampuni ya TanzaniteOne kuacha kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


  Akizungumza jana na uongozi wa kampuni hiyo,Masele ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia madini aligeuka na kuwa mkali mithili ya mbogo wakati akizungumzia suala hilo kwa viongozi wa kampuni hiyo.​  Naibu waziri alitoa amri hiyo baada ya kuelezwa na wachimbaji wadogo alipofanya ziara ya kutembelea migodi yao kuwa kampuni hiyo inawamwagia maji mgodini na alipotoa amri hiyo gari lake lilisukumwa na wachimbaji hao.


  “Sawa ninyi ni wawekezaji lakini Serikali haipo tayari kuona wachimbaji wadogo wananyanyaswa katika nchi yao hivyo niwaamuru kusitisha mara moja kumwaga maji hayo kwenye migodi ya wachimbaji wadogo,” alisema Masele.
  Hata hivyo,Mwenyekiti wa kampuni ya TanzaniteOne,Ammi Mpungwe alimthibitishia Masele kuwa kampuni yake haimwagi maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ila maji hayo yanatoka yenyewe kwenye mgodi wa TanzaniteOne.


  Mpungwe alisema maji hayo hutoka nyenyewe kutokana na jiolojia ya miamba ilivyo kwenye mgodi wao wa Bravo ambao haufanyiwi kazi lakini kampuni hiyo haijawahi kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo.


  “Mheshimiwa waziri mimi nilikuwa balozi na nikastaafu kwa heshima zote,sasa siwezi kwenda jela leo kwa kosa la kukiuka sheria za nchi,mimi ni mzalendo sitakubali kuruhusu kampuni yetu imwage maji migodini,” alisema Mpungwe.


  Pia,Naibu Waziri huyo aliitaka kampuni hiyo kusaidia huduma za jamii kama madawati shuleni,afya na maji kwenye kata zote nne za tarafa ya Moipo zilizopo pembezoni mwa migodi hiyo kuliko kuisaidia kata moja ya Naisinyai.


  “Watanzania hawatatuelewa ikiwa kampuni hii inachimba madini ya Tanzanite yenye utajiri mkubwa wakati kata za jirani wanafunzi wanakaa sakafuni,huduma za afya duni na barabara ya Kia-Mirerani ni ya vumbi,” alisema Masele.  Akizungumzia kuhusu hilo,Mpungwe alisema watajipanga kulitekeleza ila alisikitishwa na kitendo cha viongozi wa kilichokuwa kijiji cha Mirerani kukataa msaada wa zaidi ya sh12 milioni walizotoa kama msaada wa maendeleo mwaka 2000.
   

  Attached Files:

 2. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mshaurini kuhusu mirabaha na mikata hizi peanut tokens hazina tija bana..............though may be a good start
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  My foot!!!!!!!
   
 4. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  mkuu nini tena?!!!:redface:
   
 5. NguoYaSikuKuu

  NguoYaSikuKuu JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2014
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 273
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ni waziri mzuri sana. Anajitambua
   
 6. ngorope

  ngorope JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2014
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanachukua tanzanite kwa kuchangia madawati shuleni maskini tanzania shamba la bibi
   
 7. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2014
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,634
  Likes Received: 25,567
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu mipango yake ya kulipua chopa ?
   
 8. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2014
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,634
  Likes Received: 25,567
  Trophy Points: 280
  unauliza majibu ?
   
 9. l

  lupe JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2014
  Joined: Apr 1, 2013
  Messages: 5,659
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magamba kwishney
   
 10. M

  Mwanzo Kwanza JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2014
  Joined: May 4, 2014
  Messages: 1,465
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Masele huyu aliyetaka kulipua ndege ya doctor slaa au ni mwingine.
   
 11. R

  RockSpider JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2014
  Joined: Feb 16, 2014
  Messages: 6,875
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tanzanite ni Madini Pekee yanayopatikana Tanzania tu!!! Kuna haja Gani ya kuwashirikisha Wazungu?... Of all the People unamzungumzia Massele? ameifanyia nini Taifa hili? Muulize Petradiamond wataanza lini kulipa stahili za Watanzania? Kwenye Dhahabu mrabaha wa 1.2% unakaguliwa na nani?..
   
 12. NYANYADO

  NYANYADO JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2014
  Joined: Jan 8, 2013
  Messages: 2,751
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 280
  Mleta mada. Yaani wewe ni bonge LA mzembe. Anachofanya Masele ni kutimiza wajibu wake, sasa nashangaa anachokukoshea sijui nini. Wewe ni kama wale walioukataa utumwa , wakajikuta hawana uhuru
   
 13. Ibusai

  Ibusai Member

  #13
  Aug 11, 2014
  Joined: Apr 25, 2014
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Acha ushabiki wew, hayo ni majukumu yake ni si swala gen alilofanya na isitoshe hata utekelezaji haujafanyika unaanza kutokwa na bofuu. Hayo ni maneno ya kujikosha aonekana ni mtu mwema kwa wanaume ila hapo kinachofanyika ni kiin macho maana bahasha ina mhusu na hata hana muda wa kufanya ufuatiliaji tena!!!
   
Loading...