Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,546
Picha: Mhandisi Hamad Masauni
Waziri Masauni amesema hayo baada ya kushuhudia onesho la medani za kivita lililoandaliwa na askari wanaotarajia kuhitimu kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kambi ya kivita ya Kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
"Tokea nimeingia, kuna vitu viwili vikubwa sana vinanikosesha usingizi, si mimi tu nina hakika, kwanza Amiri Jeshi Mkuu na watanzania wote walio wema, la kwanza kuna matukio ya mauaji mengi toka nimekabidhiwa hii nafasi nasikia leo mtu amechinjwa ukiuliza sababu unaambiwa ni wivu wa mapenzi mwingine sijui alikuwa amedhurumiwa, la pili kumekuwepo na askari wachache ambao wanatia doa jeshi la polisi," amesema Waziri Masauni
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi nchini limejipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo ya kutumia silaha za moto na kwamba hakuna mhalifu atakayefanikiwa kutekeleza tukio la kihalifu.
Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, kamwe Jeshi la Polisi alitomvumilia askari yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni na taratibu za Jeshi hilo.
Chanzo: EATV
Pia soma > Dkt. Mpango: Rais Samia anakerwa na mauaji yanayotokea nchini. Ameagiza Jeshi la Polisi kufanya msako kubaini wanaojiuhusisha na vitendo vya mauaji
- Waziri Masauni: Serikali haiwezi kukaa kimya wakati wananchi wanauawa. Aunda kamati kuchunguza matukio ya mauaji nchini