Waziri Malima matatani tena, Polisi yakiri anamiliki silaha kinyume cha sheria.......

Ila magamba hawawezi kuchukulia serious,kama tukio lenyewe la hotelini walipindisha sembuse hili
 
Mi bado nashangaa kauli zinazokinzana kutoka kwa viongozi wetu.

Kama asiposhitakiwa na JMT basi na mimi nitatafuta AK-47 wakinikamata nayo na wakitaka kunishtaki nita-refer kwa malima mbona yeye hamiliki kialali na ameachiwa?
 
Huyu jamaa nimeanza kuwa na wasiwasi naye..pamoja na kuwa nasilaha ya kivita. Kwa nini alikuwa anatembea na vitu pamoja na pesa nyingi namna ile wakati kuna ATM na driver with full tank ya mafuta. Kuna haja ya kuangalia kama zile Laptop zote ni za kwake au kuna dili alikuwa analicheza sema lika buma. How can you carry three Laptop at a time. Hata kama alikuwa anafanya Research lakini bado haiingi akilini. Ndio maana morogoro kuna kuwa na matukio ya ujambazi kwa sana..
Mie mtazamo wangu ni kuwa AKM alikuwa katika DILI la KIJAMBAZI, wenzake wakamchezea KANYABOYA! Tena uhalifu huu ulihusisha matumizi ya silaha kali....time will tell
 
Mwandishi wa mada hii, usiidanganye hadhira/ wananchi. Hivi inakuwaje unaripoti habari za JULY 8 MWAKA HUU ambapo bado hatujafika? Fuatilia taarifa zako. Kwa mtindo huu wa kudanganya wananchi napata majibu kuwa hata taarifa zako za kuwa Malima anamiliki silaha ya Kijeshi, SUB-MACHINE GUN (SMG) sio sahihi. Malima si mjinga kiasi hiki asijue sheria za umiliki wa silaha hasa kwa silaha kama hilyo. Aidha, ungetakiwa ufanye utafiti wa kina kwanza kabla hujatoa taarifa zako. (out of research no right to speak). Inavyoonekana mwandishi huna taarifa za kutosha juu ya tukio la malima huko Morogoro. Kwa mantiki hii, unataka kuliambia Jeshi la Polisi Morogoro hawatambui wajibu wao. KWA MUJIBU WA UTAFITI WANGU,Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa na Wilaya ya Morogoro walikagua tukio na kuziona silaha hizo zote mbili iliwemo bastola moja (pistol) na rifle moja. Hivi ingekuwa kweli walikuta SMG, si wangechukua hatua kali za kisheria? Mtoa maada huna taarifa za kutosha juu ya jambo hili, pole sana!

mkuu una makengeza???
 
kwani yule changu aliyempora bado hajakamatwa? mnapoteza lengo kwa kuumba tukio la ujambazi wakati babaa alilamba nyonyo za mrembo zilizopakwa utamu ukamkolea hadi asubuhi na ndio maana changu hakuwa na sababu ya kujibebesha zigo la binduki. wizi mtupu!
 
Huyu jamaa nimeanza kuwa na wasiwasi naye..pamoja na kuwa nasilaha ya kivita. Kwa nini alikuwa anatembea na vitu pamoja na pesa nyingi namna ile wakati kuna ATM na driver with full tank ya mafuta. Kuna haja ya kuangalia kama zile Laptop zote ni za kwake au kuna dili alikuwa analicheza sema lika buma. How can you carry three Laptop at a time. Hata kama alikuwa anafanya Research lakini bado haiingi akilini. Ndio maana morogoro kuna kuwa na matukio ya ujambazi kwa sana..
Ndenga hili nilishaliona siku ya kwanza ya Tukio hili kuwekwa hewani, kwa mwananchi wa kawaida ukikuta unamiliki silaha hiyo (SMG) unaitwa jambazi au jangili. Nilisema ntaendelea kuamini hivyo hadi, polisi/mahakama itakavyothibitisha otherwise. Kuna kila dalili za kutuwezesha kumsuspect Malima kuwa jambazi, umiliki wa more than one laptop, ni sehemu nzuri ya kuanzia achilia mbali masms yake n.k. Malima hatakuwa kiongoz wa kwanza kuwasuspected kwa ujambaz hapa duniani so polisi endeleeni na uchunguzi wa kina.

Ila polisi pia wananipa wasiwasi maana ni juzi tu tumemsikia Mkuu wa Polisi Morogoro akitudanganya kuwa Malima hakukutwa na SMG na anamilizi bunduki zote mbili kihalali, sasa haya mengine yametokea wap tena???Mbona Polisi mnatuchanganya???huu uongo uongo unalenga kumnufaisha nani????Nani tumwamin katika jeshi la polisi???Manumba muongo, waziri muongo makamanda wa mikoa waongo leongo lenu ni nini???
 
Uhuni wa Serikali ya CCM na viongozi wake haujaanza kwa Adam Malima. Nakumbuka wakati wa Mkapa Waziri wake wa Ulinzi Maokola Majogo aliwahi kukamatwa na RISASI za AK47 uwanja wa ndege nchi moja ya mashariki ya mbali siikumbuki jina.

Maokola Majogo akajitetea kwamba hizo risasi alizi pack kwa bahati mbaya ktk begi lake mke wake. Alipoambia mbona ni risasi za AK47, akasema ndiyo ni za AK47 kwasababu yeye huko nyumbani (Tanzania) anamiliki AK47.

Jeshi la Polisi likatoa ufafanuzi kama hu huu kwamba Maokola Majogo haruhusiwi kisheria kumiliki SILAHA YA KIVITA ya AK47 ni kosa na inabidi achukuliwe hatua.

Lakini serikali haikumchukulia hatua na hatujui hiyo AK47 kama bado anaimiliki au hapana. Hutakiwa kuwa a rocket scientist kuelewa kwamba pamoja na Adam Malima kumiliki SILAHA YA KIVITA kinyume na SHERIA, hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi yake, na huenda kwenye reshuffle ya baraza la Mawaziri atapewa u full MINISTER. Mark my words, the writting is already on the wall.

SHERIA ZA TANZANIA ZINA MACHO ZIPO KWAAJILI YA WALALAHOI TU NA SIO VIGOGO!
 
Mwandishi wa mada hii, usiidanganye hadhira/ wananchi. Hivi inakuwaje unaripoti habari za JULY 8 MWAKA HUU ambapo bado hatujafika? Fuatilia taarifa zako. Kwa mtindo huu wa kudanganya wananchi napata majibu kuwa hata taarifa zako za kuwa Malima anamiliki silaha ya Kijeshi, SUB-MACHINE GUN (SMG) sio sahihi. Malima si mjinga kiasi hiki asijue sheria za umiliki wa silaha hasa kwa silaha kama hilyo. Aidha, ungetakiwa ufanye utafiti wa kina kwanza kabla hujatoa taarifa zako. (out of research no right to speak). Inavyoonekana mwandishi huna taarifa za kutosha juu ya tukio la malima huko Morogoro. Kwa mantiki hii, unataka kuliambia Jeshi la Polisi Morogoro hawatambui wajibu wao. KWA MUJIBU WA UTAFITI WANGU,Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa na Wilaya ya Morogoro walikagua tukio na kuziona silaha hizo zote mbili iliwemo bastola moja (pistol) na rifle moja. Hivi ingekuwa kweli walikuta SMG, si wangechukua hatua kali za kisheria? Mtoa maada huna taarifa za kutosha juu ya jambo hili, pole sana!

Wewe ndo hujui chochote au kwa makusudi mazima unataka tukubaliane na pumba zako. Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa na Wilaya ya Morogoro alishasema na ipo ktk magazeti kuwa Malima alikuwa na silaha hiyo ya SMG na sio kama unavyotaka kutupotosha kuwa alikuwa na Rifle
 
Laptops Tatu
SMG
Pesa Mingi.

Huyu jamaa weza kuwa ni jambazi, sema deal imehatibika tu.

Laptops tatu kwanini? Kama ni lazima kubeba nyingi angebeba mbili, Moja Windows na moja Macntosh.(Kama ni lazima sana).

SMG kwanini? huyu si analindwa na polisi? Na kama anahitaji ulinzi akiwa faragha si kabastola kadogo tu kauhalali kanamfaa??(Kama ni lazima sana).

Millions in Cash kwanini? Anatembelea mafuta ya serikali, anafanyiwa service na serikali anatibiwa na serikali. N on top of all that kuna ATMs, Gari inawekewa full tank. Cheo chake dhamana tosha hata akipata emergency. Sasa mahela ya nini?

Huyu asiponyoosha maelezo vizuri lazima atakuwa ni jambazi, tena lililokomaa.

Tunaomba Msiendeleze Kulindana kwenye hili.
 
Inawezekana alikuwa na mzigo wa madawa ya kulevya jamaa wakamzidi kete akasingizia ameibiwa laptop, maana hawa wadudu wanalipa kweli ikiwa na kilo zako 10 lazima ujilinde kisawasawa.
 
Kumbe gobole na bastola! lakini zote hizo za nini kwa wakati mmoja? Ni vyema Mheshimiwa akafunguka mwenyewe ili kuwatoa hofu watanzania. Wenzetu Nigeria imekuja kugundulika kuwa baadhi ya wanasiasa ni wafuasi wa Boko haramu isijekutokea na kwetu. Matukio haya sasa yanazidi kuongezeka mwingine alipanda nayo siraha yake kiunoni ktk kampeni na sasa huyu naye anaziweka hotelini siraha zake bila ya uangalizi.
 
malima bado ana ubrazameni wa kizamani,alipita ofisini kwetu wakati wa ziara ya bilal,alichomoa laptop,ipad na kuanza kufanya alichokuwa nafanya kwenye corridor flani,.(leo naanza kuhisi alikuwa anaangalia blue au anachat kimada)nyambaf kabisa...
 
  • Thanks
Reactions: kui
SMG.jpg
Labda alikuwa amemshikia askari anaye mlinda mhe.Adam Malima

Kwa mara nyingine tena waziri Malima anaingia matatani. Jeshi la Polisi limekaririwa kuwa waziri huyu anamiliki silaha SMG kinyume cha sheria. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini.........What next? mahakamani? au mkubwa hashtakiwi??

SMG yamponza Malima
• Polisi wamshangaa kumiliki SMG
na Dunstan Bahai


JESHI la Polisi nchini limemkana Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, likiweka bayana kuwa amevunja sheria za kijeshi kwa kitendo chake cha kumiliki bunduki aina ya SMG.

Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alisema kuwa jeshi hilo halielewi namna waziri huyo alivyofanikiwa kumiliki silaha hiyo ya kivita kwa kuwa kisheria inapaswa kuwa mikononi mwa majeshi tu, na kamwe haiwezi kumilikiwa na raia.

“SMG hairuhusiwi kumilikiwa na raia, hii ni silaha maalumu kwa majeshi yetu tu na ni kosa kubwa kisheria,” alisema na kuelekeza atafutwe msemaji wa jeshi hilo, ili kutoa maelekezo ya wapi Waziri Malima alikoipata silaha hiyo.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, hakupatikana ikidaiwa yuko katika kikao. Aidha, maofisa waandamizi wa jeshi hilo waliozungumza kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walieleza kushangazwa kwao na hatua ya Malima kumiliki silaha hiyo, lakini kubwa zaidi kutembea nayo na kuiacha hadharani.

“Hili si tukio dogo kwa mtu binafsi kumiliki silaha kubwa ya kivita kama hiyo. Sijui ni hatua gani atachukuliwa na wakubwa kwa sababu, kwa namna yoyote jambo zito kama hili lazima lichukuliwe kwa uzito mkubwa,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.

Aliongeza kuwa hatua ya naibu waziri huyo kutembea na silaha hiyo na kuiacha hotelini ambako ingeweza kuchukuliwa na mtu yeyote ni jambo lisiloweza kuvumilika na akashauri sheria ichukue mkondo wake.

“Kama wale watu waliweza kuvunja dirisha na kuiba kwa mujibu wa maelezo yake, ingekuwaje kama wangechukua silaha hiyo na kwenda kufanya uhalifu sehemu nyingine? Hii ni hatari sana,” alisema ofisa huyo.

Aidha, Naye Mkuu wa jeshi hilo, IGP Said Mwema, simu zake mbili zilipokewa na wasaidizi wake, ambao walisema kuwa silaha hiyo haiwezi kumilikiwa na raia.

Maelezo ya naibu waziri huyo kumiliki silaha hiyo yalithibitishwa pia na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tukio la Malima kuibiwa hotelini.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alipopigiwa simu zaidi ya mara mbili, alisema kuwa asingeweza kutoa maelezo yoyote kwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.

Julai 8, mwaka huu, Naibu Waziri Malima, aliibiwa vitu mbalimbali alivyokuwa navyo katika Hoteli ya Nashera ya mjini Morogoro alikofikia mara baada ya ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 23.3.

Malima alidai kuwa wezi hao pamoja na kufanikiwa kumuibia mali hizo hawakuweza kuiba silaha mbili, ikiwamo bunduki aina ya SMG pamoja na bastola, alizokuwa nazo, licha ya kwamba zilikuwa sehemu ya wazi chumbani hapo.

Waziri Malima jana kutwa nzima hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa wapi alikoipata bunduki hiyo, wala sababu za msingi za kutembea na silaha nzito kama hiyo, akijua kuwa yuko katika ziara ya kikazi. Juhudi zaidi za kumtafuta zinaendelea
 
Bado tu hajatangaza kujiuzulu......alikua anaikodisha nini kwa wazee wa issue ama magharamia ?

Bastola peke yake tu ingekutwa kwa Lema leo tungekuwa tunazungumza mengine. Lakini kwakuwa imekutwa kwa Jambazi la CCM mambo shwariiiiii mpaka basi. Hii imenikumbusha kuna kipindi Anne Kilango alipotekwa na Majambazi, wakamnyang'anya fedha, hata kitu mbaya alifanyiwa, lakini chakushangaza Tinga tinga likasema msiwakamate hao majambazi najua nitakachowafanya, kazi itamalizwa ni vijana wake. Nikajua kweli wale vijana wake kumbe walikuwa majambazi, ambapo baada ya muda mchache tukasikia yule jambazi aliyemfanya kitu mbaya mama Tingatinga ameuawa na majambazi. Kabla hawajamua JB walimfanya Ndoa kwanza. Inawezekana kabisa Malima kama siyo Jambazi basi anamiliki Majambazi.
 
Malima alikuwa na silaha mbili mojawapo ni hii ya kivita -SMG, na vinasa sauti! Huyu waziri mdogo alikuwa kwenye mission gani?
 
Back
Top Bottom