Waziri Malima matatani tena, Polisi yakiri anamiliki silaha kinyume cha sheria....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Malima matatani tena, Polisi yakiri anamiliki silaha kinyume cha sheria.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Mar 15, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kwa mara nyingine tena waziri Malima anaingia matatani. Jeshi la Polisi limekaririwa kuwa waziri huyu anamiliki silaha SMG kinyume cha sheria. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini.........What next? mahakamani? au mkubwa hashtakiwi??

  SMG yamponza Malima
  • Polisi wamshangaa kumiliki SMG
  na Dunstan Bahai


  JESHI la Polisi nchini limemkana Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, likiweka bayana kuwa amevunja sheria za kijeshi kwa kitendo chake cha kumiliki bunduki aina ya SMG.

  Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alisema kuwa jeshi hilo halielewi namna waziri huyo alivyofanikiwa kumiliki silaha hiyo ya kivita kwa kuwa kisheria inapaswa kuwa mikononi mwa majeshi tu, na kamwe haiwezi kumilikiwa na raia.

  “SMG hairuhusiwi kumilikiwa na raia, hii ni silaha maalumu kwa majeshi yetu tu na ni kosa kubwa kisheria,” alisema na kuelekeza atafutwe msemaji wa jeshi hilo, ili kutoa maelekezo ya wapi Waziri Malima alikoipata silaha hiyo.

  Hata hivyo, msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, hakupatikana ikidaiwa yuko katika kikao. Aidha, maofisa waandamizi wa jeshi hilo waliozungumza kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walieleza kushangazwa kwao na hatua ya Malima kumiliki silaha hiyo, lakini kubwa zaidi kutembea nayo na kuiacha hadharani.

  “Hili si tukio dogo kwa mtu binafsi kumiliki silaha kubwa ya kivita kama hiyo. Sijui ni hatua gani atachukuliwa na wakubwa kwa sababu, kwa namna yoyote jambo zito kama hili lazima lichukuliwe kwa uzito mkubwa,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.

  Aliongeza kuwa hatua ya naibu waziri huyo kutembea na silaha hiyo na kuiacha hotelini ambako ingeweza kuchukuliwa na mtu yeyote ni jambo lisiloweza kuvumilika na akashauri sheria ichukue mkondo wake.

  “Kama wale watu waliweza kuvunja dirisha na kuiba kwa mujibu wa maelezo yake, ingekuwaje kama wangechukua silaha hiyo na kwenda kufanya uhalifu sehemu nyingine? Hii ni hatari sana,” alisema ofisa huyo.

  Aidha, Naye Mkuu wa jeshi hilo, IGP Said Mwema, simu zake mbili zilipokewa na wasaidizi wake, ambao walisema kuwa silaha hiyo haiwezi kumilikiwa na raia.

  Maelezo ya naibu waziri huyo kumiliki silaha hiyo yalithibitishwa pia na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tukio la Malima kuibiwa hotelini.

  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alipopigiwa simu zaidi ya mara mbili, alisema kuwa asingeweza kutoa maelezo yoyote kwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.

  Julai 8, mwaka huu, Naibu Waziri Malima, aliibiwa vitu mbalimbali alivyokuwa navyo katika Hoteli ya Nashera ya mjini Morogoro alikofikia mara baada ya ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 23.3.

  Malima alidai kuwa wezi hao pamoja na kufanikiwa kumuibia mali hizo hawakuweza kuiba silaha mbili, ikiwamo bunduki aina ya SMG pamoja na bastola, alizokuwa nazo, licha ya kwamba zilikuwa sehemu ya wazi chumbani hapo.

  Waziri Malima jana kutwa nzima hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa wapi alikoipata bunduki hiyo, wala sababu za msingi za kutembea na silaha nzito kama hiyo, akijua kuwa yuko katika ziara ya kikazi. Juhudi zaidi za kumtafuta zinaendelea
   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  manumba haaminiki anatumika kisiasa!
   
 3. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa nimeanza kuwa na wasiwasi naye..pamoja na kuwa nasilaha ya kivita. Kwa nini alikuwa anatembea na vitu pamoja na pesa nyingi namna ile wakati kuna ATM na driver with full tank ya mafuta. Kuna haja ya kuangalia kama zile Laptop zote ni za kwake au kuna dili alikuwa analicheza sema lika buma. How can you carry three Laptop at a time. Hata kama alikuwa anafanya Research lakini bado haiingi akilini. Ndio maana morogoro kuna kuwa na matukio ya ujambazi kwa sana..
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wamekirie? Sasa tunasubiri hukumu ya kosa hilo.
   
 5. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Manumba na Tendwa ni watu ambao jamii ya Watanzania haitakiwi kuwaamini. wako kimaslahi zaidi..Nakumbuka ile kesi ya Chenge Manumba alikuwa anatakuipangua ikashindikana!!!
   
 6. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bado tu hajatangaza kujiuzulu......alikua anaikodisha nini kwa wazee wa issue ama magharamia ?
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Episode ya ngapi hii? Parental guidence Advised
   
 8. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  nahisi kitu kama hiki mkuu huenda alikuwa anaikodisha kwa wazee wa kazi na kisha wanamlipa kwa dola. na alikuwa ametoka kuchukua hesabu kisha machine akaifanyie service halafu awaletee tena. Hesabu yenyewe ndo ile dola 4,000. Na ndio maana alishangaa kuona 'mwizi' wake aliziacha na akasema ni mtaji tosha zile machine, anajua zinavyomuingizia
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dah! Hili saga hili!
   
 10. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  "Serikali ya wahuni wahuni,lazima itangozwa kihuni kihuni" - J .k.Nyerere (R.I.P)
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Labda sio Manumba na magamba, Ingekkuwa amekutwa nazo Mnyika ama Zitto basi kesho tu angepandishwa kwa pilato
   
 12. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hii ni Bongoland, yataisha kimyakimya. Angekua kakutwa nayo "kajambanani" saa hii angekuwa jela na ushahidi wote umekamilika na hukumu juu. Samaki mkubwa ni mkubwa tu. Umesikia wapi Papa mkubwa kamezwa na papa mwenziwe?
   
 13. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizo ni zana za kijambazi huwezi jua watu wanafanya kazi nyingi kujiongezea kipato
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Labda ni spy fulani....
   
 15. a

  arinaswi Senior Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mmm kigeugeu hawa polisi, mara hakuwa na silaha aina ya smg mara tena kakutwa nayo na kaiacha hadharani!! tuamini lipi? na sasa tunataka sheria imuwajibishe huyu mkuu kikamilifu na angejiuzulu kupisha uchunguzi au mashitaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.
   
 16. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Gangstar?
   
 17. kandidus

  kandidus Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwandishi wa mada hii, usiidanganye hadhira/ wananchi. Hivi inakuwaje unaripoti habari za JULY 8 MWAKA HUU ambapo bado hatujafika? Fuatilia taarifa zako. Kwa mtindo huu wa kudanganya wananchi napata majibu kuwa hata taarifa zako za kuwa Malima anamiliki silaha ya Kijeshi, SUB-MACHINE GUN (SMG) sio sahihi. Malima si mjinga kiasi hiki asijue sheria za umiliki wa silaha hasa kwa silaha kama hilyo. Aidha, ungetakiwa ufanye utafiti wa kina kwanza kabla hujatoa taarifa zako. (out of research no right to speak). Inavyoonekana mwandishi huna taarifa za kutosha juu ya tukio la malima huko Morogoro. Kwa mantiki hii, unataka kuliambia Jeshi la Polisi Morogoro hawatambui wajibu wao. KWA MUJIBU WA UTAFITI WANGU,Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa na Wilaya ya Morogoro walikagua tukio na kuziona silaha hizo zote mbili iliwemo bastola moja (pistol) na rifle moja. Hivi ingekuwa kweli walikuta SMG, si wangechukua hatua kali za kisheria? Mtoa maada huna taarifa za kutosha juu ya jambo hili, pole sana!
   
 18. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli kabisa!
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nafasi zao ni za kisiasa zaidi.
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  s01e02::::::pg18
   
Loading...