Waziri Malima abariki upandaji holela wa bei za chakula

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,477
17,675
Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima, ameruhusu upandaji holela wa bei za chakula, hasa wakati wa sikukuu za Idi na Krismas. Akiongea na Radio One leo asubuhi kwenye kipindi cha Kumepambazuka, Malima alisema kwamba biashara ya chakula ni huria, hivyo serikali haiwezi kuwazuia wafanyabiashara kuongeza bei kadri watakavyoona inafaa.

Malima alifafanua kwamba upandaji wa bei za chakula hutegemea upatikanaji na uhitaji (demand and supply). Kwamba upatikanaji ukiwa chini na mahitaji yakawa juu, lazima bei ipande automatically.

Alipoulizwa kwa nini bei zipande wakati wa sikukuu tu, alijibu kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao huficha chakula kwa makusudi ili kulazimisha bei ipande. Katika ufafanuzi wa kwanini serikali isiwachukulie hatua za kisheria wale wafanyabiashara wanaoficha chakula, alidai kwamba serikali haiwezi kuingilia mambo binafsi ya wafanyabiashara. "Hatuwezi kuwaingilia wafanyabiashara wanaofanya biashara halali ambao wamelipa leseni na wanaoiingizia serikali kodi", alisema.

Alisisitiza kwamba sio lazima kila mtu ale kuku na pilau wakati wa sikukuu; asiyekuwa na uwezo ale ugali na maharage. Alisema kwamba tatizo la watanzania ni kupenda kuishi maisha wasiyoyamudu kwa kulazimisha kula na kuvaa vizuri wakati uwezo huo hawana.

Source: Radio One.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom