Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Mimi naishauri Mamlaka ya uteuzi kuwa Waziri yeyote anayeteuliwa katika Baraza lake basi huyo Waziri awe na fani inayohusika na Wizara aliyoteuliwa. Mfano Waziri wa Nishati ni vyema akiwa na degree ya umeme au uhandisi katika fani hiyo, Afya lazima awe Daktrari, Ujenzi awe mhandisi, Elimu awe mwalimu. Mhe. Waziri wa Nishati ana fani gani?.
 
... nyeti za kuku zi wazi! Umeme kukatika pindi manyunyu yanapoanza imekuwa jambo la kawaida nchi hii; sio jana tu; ni tatizo la miaka na miaka. How long does it take kuzivalisha hizo nyaya nguo ili kuondokana na tatizo? CCM ni wapuuzi sana; imefika mahali wamehalalisha upuuzi wao uonekane kawaida maisha yanaendelea.
Eti wanasema nalo ni tatizo la legacy? Nonsense...sisi tunataka watu wanaotoa majawabu ya changamoto zetu sio story.
Ilikuwa rahisi kuandika twitter...amepewa mzigo anaanza kupiga hadithi badala ya kufanya kazi
 
Waziri Makamba umeonyesha kiwango kidogo cha ukomavu, kwa kusema wabunge wanakubana kwa sababu ya uwaziri wako.

Hii ni kauli inayopaswa kutolewa na mtu ambae sio msomi, hakuna wabunge wenye shida na uwaziri wako bali wanachofanya ni wajibu wao kwa maana wanawakilisha wananchi.

Wabunge wanarudi majimboni wanaulizwa kuhusu umeme kwa kuwa unaathiri shughuli zao, wao ndio wanakuja bungeni kueleza kero hiyo. Wewe hutaki uulizwe.

Pia waziri unapaswa kufahamu sio wewe tu ambae unabanwa kwenye utendaji hasa Jambo fulani likienda vibaya. Ni mawaziri wote hubanwa hivyo, waziri wa afya amekuwa akibanwa kuhusu vituo vya afya.

Waziri wa maji juma aweso amekuwa akibanwa sana bungeni kuhusu upatikanaji wa maji, waziri wa ujenzi amekua akibanwa kuhusu ubovu wa miundombinu Ila wote hao hawakuwahi kusema tatizo ni uwaziri wao.

Majibu yako mh.makamba ni ya kushangaza, sasa unasema waya kwenye substation ya ubungo zipo uchi hivyo upepo ukipuliza tu umeme unakatika.

Kwa majibu ya namna hiyo unategemea watu wataacha kukuuliza maswali?

Kamati ya nishati ya bunge ni haki yao kuhoji na wamesema hakuna sababu za msingi za umeme kukatwa.

Makamba maswali ya kuhusu wizara ya nishati unataka aulizwe nani? Mbona mawaziri wengine wanaulizwa maswali kuhusu wizara zao na wanajibu bila shida, kwa nini wewe uone unaonewa wivu? Hutaki watu/wabunge waulize kuhusu wizara ya nishati?

Wajibu maswali yao kiuweledi na sio kusingizia uwaziri wako.
January kaongea ukweli sio tuu wanambana bali Wana chuki binafsi ,huo ndio ukweli.

Kamati Ya nishati ina fursa zote za kuhoji yeyote ikiwemo kumuita mtendaji mkuu.
 
KULIKONI UJENZI WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE KUSUASUA?!

1) Tunaishukuru Serikali kwa Taarifa zake mbalimbali kupitia Waziri wa Nishati Mheshimiwa January Makamba (Twitter Account yake na Bungeni) na huyu Mhandisi Christopher Bitesigirwe (ambaye sina uhakika iwapo alichosambaza Mitandaoni ni Tamko lake binafsi au Tamko Rasmi kwa niaba ya Serikali).

2) Niharakishe kushauri kwamba haya Matamko yawe yanatolewa kwa Utaratibu Maalum maana, wakati mwingine, yanaweza kuwa na Contractual Implications.

3) Maswali ya Awali ya BJC!

Kwa Msingi wa Matamko haya, ningependa kujua:

a) Ni kwa sababu gani hasa Serikali imeruhusu kutokea lolote lililotokea kusababisha Bwawa la Mwalimu Nyerere lisianze kujazwa maji kesho tarehe 15.11.2021 kama alivyoahidi Bungeni Waziri wa zamani wa Nishati, Mheshimiwa Medard Kalemani?!
b) Ujenzi wa Mradi umechelewa kwa muda gani?! Izingatiwe kwamba Ucheleweshaji wa Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere umeripotiwa kwa mara ya kwanza Bungeni (juzikati) na Waziri mpya wa Nishati, Mheshimiwa January Makamba.
c) Na tunajuaje kiuhakika Urefu wa Ucheleweshaji wa Ujenzi kimkataba iwapo Mkandarasi hajaomba na kupewa EoT (Extension of Time) ya muda huo?! Kwa Mkataba huu EoT inaweza kuombwa lini hasa (katikati ya Mkataba au karibu na mwisho wa Mkataba)?! Au labda Serikali imeishakubaliana na Mkandarasi kwa Maandishi ya Kimkataba kuhusu Ucheleweshaji huu?!
d) Nani aliyesababisha Ucheleweshaji huu?! Ni Serikali au Mkandarasi?! Kivipi?! Nani hasa atakayegharimia Ucheleweshaji huu na kwa kiasi gani?!
e) Kuna Ucheleweshaji wowote ambao umewahi kusababishwa na Mkandarasi (na Mkandarasi hana ubishi)?! Mkandarasi atagharimia kiasi gani?!
f) Kuna muda wowote (toka Mradi uanze) ambapo Ujenzi uliwahi kusimama?! Iwapo jibu ni ndiyo, ulisimama kwa muda gani (toka tarehe ngapi hadi tarehe ngapi) na kwa sababu gani?!
g) Kuna muda wowote ule wa Ucheleweshaji wa Ujenzi ambao ulisababishwa na Serikali kushindwa kumlipa Mkandarasi?! Iwapo jibu ni ndiyo, Malipo yalicheleweshwa kwa muda gani na kwa sababu gani?! Uhusiano wa muda wa kuchelewesha Malipo na Muda wa Ucheleweshaji wa Ujenzi ukoje kimkataba?!
h) Mkandarasi alilipwa Advance Payment kiasi gani na kwa Matumizi gani exactly?! Alilipwa tarehe ngapi?!
i) Mkandarasi alipanga kuagiza Mitambo na Mashine lini?! Je, aliagiza mapema au alichelewa kuagiza?!
j) Mkataba kati ya Serikali na Mkandarasi ulisainiwa tarehe ngapi?!
k) Mradi ulitakiwa ukamilike tarehe ngapi?!
l) Mobilization Period ni muda gani?!
m) Site Handing Over!
Hivi Mkandarasi alikabidhiwa Saiti tarehe ngapi?!
n) Je, Timu ya Usimamizi wa Mradi ina Mamlaka kamili na Muda wa kutosha kimkataba kucheki na ku-approve Michoro ya Mradi, Nyaraka za Mradi na Specifications za Mradi zinazoandaliwa na Mkandarasi kabla ya kutumika kujengea au kufanya uagizaji?!

4) Nikiwa nimeishaandika niliyoandika hapo juu, nimekutana na hii Taarifa Rasmi ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti!

Haina sahihi wala Jina la Mwandishi (sijauona ukurasa wa mwisho!) lakini inaelekea iliandaliwa kwa ajili ya Kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oktoba 2021.

5) Baada ya kuisoma na kuikagua vizuri Taarifa hii nimegundua kwamba kumbe si Taarifa kamili, bali ni baadhi tu ya kurasa au sehemu za kurasa. Ni Extracts kama ifuatavyo:

a) Karatasi inayosomeka kama Ukurasa wa Kwanza wenye Kipengele 1.0. Kuna Aya 3 za Utangulizi.
b) Karatasi isiyoonyesha Namba ya Ukurasa yenye Kipengele 2.0 (titled Maendeleo ya Mradi) na Kipengele 2.1 (titled Taarifa ya Fedha za Mradi). Kuna Aya 3.
c) Karatasi yenye Kipengele 5.0 (Changamoto).
d) Karatasi yenye Kipengele 6.0 (Hatua Zinazochukuliwa na Mwajiri).

6) Disclaimer!

a) Vipengele kuanzia 2.2; 3.0 na 4.0 vimerukwa. Sijaviona na kwa hiyo si sehemu ya Makala yangu hii.
b) Sijaona wala kusoma Vipengele kuanzia Ukurasa wa 9. Kipengele cha mwisho kinachoonekana ni Kipengele Na.6(i) na Na.6(ii).

7) Sasa naomba niendelee kujadili Mada nikijielekeza kwenye hii Taarifa ya Wizara ya Nishati.

8) Taarifa za Mkataba!

Taarifa zilizomo kwenye Utangulizi wa Taarifa hii ni pamoja na hizi:

a) Mnamo tarehe 12 Disemba, 2018 TANESCO kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) iliingia Mkataba na Kampuni mbili za nchini Misri zilizoingia ubia (Kampuni za Arab Contractor na Elsewedy Electric (JV AC - EE) kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project kwa thamani ya Shilingi 6,558,579,983,500.28.
b) Mradi unafadhiliwa na Serikali ya JMT kwa asilimia 100.
c) Wigo wa kazi (za Mkandarasi - nyongeza yangu) unahusu Usanifu, Ununuzi, Usimikaji, Majaribio na Kukabidhi kituo kilichokamilika chenye uwezo wa kufua MW 2115 ambazo ni sawa na Umeme wa Saa za Gigawati (GWh) 6,307 kwa mwaka.
d) Muda wa Mkataba ni miezi 42 ikiwemo miezi 6 ya Kazi za Maandalizi ya Awali.

9) Ni wazi:

a) Mkataba huu ni wa Design-and-Build.
b) Serikali ya JMT itakuwa na Timu yake ya Wataalam Wanaosimamia Mradi ikiongozwa na Msimamizi Mkuu wa Mradi.

10) Kwa kawaida, Majukumu ya Timu ya Usimamizi wa Mradi ni pamoja na:

a) Kusimamia Utekelezaji wa Mkataba.
b) Kumsimamia Mkandarasi na kuhakikisha wakati wote anafanya kazi zake kama inavyotakiwa kimkataba.
c) Kutoa Site Instructions kwa Mkandarasi kila inapobidi.
d) Kutoa Hati za Malipo kwa Mkandarasi kwa mujibu wa Mkataba. Kwa lugha nyepesi ni Kuthibitisha Malipo ya Mkandarasi kabla hajalipwa.
e) Kushiriki na kuendesha Site Meetings.
f) Kushiriki na kuongoza Ukaguzi wa Site (Site Inspections).
g) Kutoa Taarifa kwa TANESCO/Serikali kuhusu Maendeleo ya Mradi.
h) Kutoa Ushauri wa kitaalam kwa TANESCO/Serikali kuhusiana na Mradi/Mkataba.
i) Kulinda Maslahi ya Serikali ndani na nje ya Mkataba.

11) Hili Suala la Serikali Kumshauri Mkandarasi limenistua kiasi naomba nianze nalo!

a) Nimestuka na kushangaa sana kusikia kwamba Serikali/TANESCO (Mwajiri) imetoa Ushauri kwa Mkandarasi.
b) Naomba nikisema "Serikali" iwe ni sawa tu na kusema "TANESCO", "Mwajiri" au "Timu ya Usimamizi wa Mradi".

Tafadhali rejea Kipengele Na.6 cha Taarifa ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

12) Naomba ninukuu:

Serikali (Mwajiri) inaendelea kumshauri Mkandarasi mambo yafuatayo:

a) Mkandarasi aongeze kasi ya utekelezaji wa Ujenzi kwa kuajiri Wataalam wenye uzoefu na ujuzi au kutafuta Kampuni bobezi zotakazofanya kazi ya Ujenzi wa Jengo la Mitambo.
b) Mkandarasi amtumie Mtengenezaji wa Mitambo kusimika Mitambo hiyo ili kuhakikisha ubora wa kazi na kuepuka Changamoto zinazoweza kutokea katika kipindi cha maangalizi na uendeshaji.

13) Nimebaki najiuliza:

a) Serikali imemshauri Mkandarasi kwa kutumia Kipengele kipi cha Mkataba?! Hivi kweli kwenye Mkataba wa Ujenzi wa Bwawa hili kuna Kipengele kinachotamka kwamba moja ya Majukumu ya Serikali ni kumshauri Mkandarasi?! Mbona hii ina-sound kama utani fulani hivi, if not gross incompetence!
b) Kwani Serikali ya JMT ni Mshauri Elekezi wa Mkandarasi?! Hivi hata hii Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti haikustuka kuona jambo hili kwenye Taarifa Rasmi ya Wizara ya Nishati kwao?!
c) Kwani si ni kazi ya Washauri Elekezi wa Mkandarasi kumshauri Mkandarasi?!
d) Nani huyo aliyeiingiza Serikali mkenge ifanye makosa ya kujigeuza Mshauri Elekezi wa Mkandarasi?!
e) Hili si jambo dogo na linaweza kuigharimu Serikali yetu Billions (if not Trillions) of Shillings. Maana mbele ya safari unaweza kuja kumbana Mkandarasi kwa suala fulani, akachomoa kilaini kwa kusema, na kuonyesha Ushahidi, kwamba yeye amefanya alichoshauriwa na Serikali yenyewe.
f) Huu ni mfano mzuri si tu wa matumizi mabaya ya Madaraka, bali pia athari za Wanasiasa kujigeuza Wataalam wa Ujenzi. Kuweka mkokoteni mbele ya punda! Punda ni sisi Wataalam wa Ujenzi na mkokoteni ni Viongozi wetu (wa kisiasa)! Ashakum si matusi!

14) Ukisoma kwa makini huu Ushauri wa Serikali kwa Mkandarasi utapata picha kwamba:

a) Kasi ya Ujenzi ya Mkandarasi iko chini.
b) Ubora wa Kazi ya Usimikaji Mitambo unatia shaka.

15) Sasa iwapo hivi ndivyo, ufumbuzi wa Changamoto hii si Serikali "kuendelea kumshauri Mkandarasi", bali Serikali, kwa kupitia Msimamizi Mkuu wa Mradi, kumpa Mkandarasi Site Instruction inayomuagiza Mkandarasi:

a) Kuongeza Kasi ya Ujenzi kwa sababu Kasi iko chini sana na hili halikubaliki maana linaathiri overall Progress of the Works.
b) Kuongeza Ubora wa Kazi ya Usimikaji wa Mitambo kwa sababu Kiwango cha Kazi hiyo hakiridhishi wala kukubalika.

16) Narudia! Site Instruction si Ushauri.

17) Taarifa ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inasema:

"Mradi kwa ujumla una viashiria vya kuchelewa katika maeneo ya Ujenzi wa Tuta Kuu (Main Dam), Jengo la Mitambo (Power House), Njia za Maji pamoja na Kingo za Maji (Saddle Dams). Mkandarasi amewasilisha sababu zifuatazo zilizosababisha kuchelewa kwa Mradi kwa siku 477":

a) Mafuriko!
Mvua kubwa zilizonyesha nchini katika kipindi cha Desemba 2019 mpaka Juni 2020 zilisababisha uharibifu wa miundo mbinu na hivyo kupelekea kusimama kwa ujenzi wa njia ya kuchepusha maji ya Mto Rufiji.
b) Sababu za Kimazingira!
Kujitoa kwa Makampuni watengenezaji wa Mitambo kutoka Nchi za Ulaya kwa sababu za kimazingira na kupelekea kuchelewa kuanza kwa utengenezaji wa Mitambo.
c) Mlipuko wa Ugonjwa wa Uviko 19!
Kutokana na Nchi mbalimbali Duniani kuweka zuio la safari, ilipelekea Wataalam wa Mkandarasi kushindwa kusafiri.

Tafadhali rejea Vipengele Na.5(i), Na.5(ii) na Na.5(iii) vya Taarifa ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

18) Taarifa ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inaonyesha wazi kwamba:

a) Mkandarasi ndiye aliyesababisha Ucheleweshaji wa Ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere. Taarifa ya Wizara ya Nishati inasema kwamba: "Hata hivyo, Mwajiri amebaini sababu ya msingi iliyosababisha Mradi kuchelewa ni Mkandarasi kujenga Handaki moja la njia ya kuchepusha maji ya mto badala ya Mahandaki mawili hivyo kusababisha maji ya mto kupita eneo la Ujenzi wa Tuta Kuu wakati wa masika."
Tafadhali rejea Kipengele Na.5.
b) Hii ni Hoja nzuri sana. Naipongeza Serikali kwa kumstukia Mkandarasi ambaye amefanya kosa kubwa sana la kiufundi lililochangia Ujenzi wa Bwawa kuchelewa na halafu kusema uongo kwa kusingizia Mvua na Mafuriko na mambo mengine wakati makosa ni ya kwake! Maswali: Je, Serikali imechukua hatua gani za kimkataba kulinda Maslahi ya Serikali (Mwajiri) na kuiepusha Serikali na Hasara?! Je, Timu ya Usimamizi wa Mradi ilichukua hatua gani baada ya kuona Mkandarasi anajenga kinyume na Michoro ya Ujenzi?! Kuna Site Instructions zozote ambazo Msimamizi Mkuu wa Ujenzi alimpa Mkandarasi kumwambia ajenge Handaki la pili na Mkandarasi akakaidi?! Kwangu hiki ndio kipimo cha umakini wa Timu ya Usimamizi wa Ujenzi wa Bwawa hili.
c) "Sababu za Kimazingira"! Maswali! Hii Lugha ya Mafumbo inakujaje tena?! Neno "mazingira" linatumika kwa maana gani hapa?!
d) Tunaambiwa kuna Makampuni ya Ulaya ya Watengeneza Mitambo walijitoa. Kwa maoni yangu, hili halimchomoi Mkandarasi kwenye uwajibikaji kwa Ucheleweshaji wa Ujenzi. Kwa sababu Mkataba huu ni Design-and-Build na hao waliojitoa ni sehemu ya Timu ya Mkandarasi, Mkandarasi hawezi kabisa kutumia kujitoa kwako kukwepa kuwajibika kwa Ucheleweshaji wa Mradi. Maswali: Kwanza hayo Makampuni yalijitoa lini exactly?! Mbona hili halijawekwa wazi kwenye Taarifa ya Wizara ya Nishati (kama lilivyowekwa wazi Suala la Handaki)?! Namaanisha ukweli kwamba kujitoa kwa Makampuni haya hakumuondolei Mkandarasi uwajibikaji kwa Ucheleweshaji wa Mradi.
e) Mradi umechelewa kwa siku 477!! Mbona sielewi! Maswali: Hivi hii Ripoti ya Wizara ya Nishati imekosewa au ndiyo ukweli kwamba Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere umechelewa kwa mwaka mmoja na miezi karibu 4?! Nashangaa maana huu ni Ucheleweshaji mkubwa sana. Aidha, nashangaa kwa nini Wananchi hatukuambiwa mapema?! Hivi Waziri Kalemani wakati analitaarifu Bunge kuhusu Mradi huu, na kutangaza siku ya kuanza kujaza Bwawa maji kuwa ni kesho tarehe 15.11.2021, alikuwa anajua au hajui nini kuhusu Ucheleweshaji huu?! Nani alimuongopea nani?! Kwa nini Wananchi tusielezwe ukweli?! Kwa nini Bunge halihoji inavyostahili?!
f) Nimeshangaa jinsi Wizara ya Madini inavyotoa Taarifa nzito kama hii bila kujali umuhimu wa kutumia maneno kama "eti", "anadai", "anazodai zilisababisha", n.k. kuonyesha Serikali haikubaliani. Tafadhali rejea Kipengele 5.0.
g) Nimeshangaa pia jinsi Taarifa ya Wizara ya Nishati inavyoita Ucheleweshaji wa Ujenzi kwa siku 477, "Mradi una viashiria vya kuchelewa." Kwangu, hii inasomeka kama juhudi za kufanya Ucheleweshaji wa Mradi kwa siku 477 kitu kidogo sana! Maswali: Nimebaki najiuliza "Ni nini nisichoelewa hapa...?!" Ina maana Wizara ya Nishati haina uhakika kwamba Mradi umechelewa au...?!

19) Force Majoure!

a) Ni matumaini yangu Serikali haitafanya makosa ya kumruhusu Mkandarasi atulaghai na kutumia visivyo Clause ya Force Majoure kusingizia Mvua na Mafuriko kama sababu za kuchelewesha Ujenzi. After all, Tanzania mvua haijawahi kunyesha kwa mwaka mmoja na miezi 4.
b) Kwa kawaida Tender ya Mkandarasi huwa inajumuisha (it takes into account) ukweli kwamba kuna Msimu wa Mvua. Hivyo Mvua za Msimu haziwezi kugeuzwa sababu for invoking Force Majeure.
c) Tusikubali kugeuzwa mafala na kuibiwa sababu ya Uzembe, Siasa na/au Ufisadi.

20) COVID-19!

a) Hapa ndio tunahitaji kuwa makini sana sana.
b) Najua COVID-19 itakuwa imeegemezwa kwenye Force Majoure (which is right) kwa kadri Mkataba unavyoruhusu na Nyaraka za Mradi (Project Documentation) zinavyothibitisha.
c) Lakini tusikubali tu kila kitu kwa mgongo wa COVID-19. Ni lazima Kipengele cha Force Majoure kisomwe kwa makini sana, tena bila huruma, na kulinganishwa na Project Documentation ili kuona nini ni haki kwao na nini si haki.
d) Kumbukeni hapa tunaongelea Ucheleweshaji mkubwa ambao ni sawa na Malipo makubwa sana ya ziada.

21) Taarifa ya Wizara ya Nishati kwamba hadi Desemba 2020 Serikali ilikuwa haijawahi ku-default kwenye Malipo. Naomba ninukuu:

"Kutokana na Serikali kuendelea kutimiza wajibu wake wa kumlipa Mkandarasi kwa wakati, mwezi Desemba 2020 Serikali ilifanikiwa kutimiza miezi 24 ya kumlipa Mkandarasi bila kuchelewa."

a) Maswali: Kwani baada ya Desemba 2020 Serikali ilianza kuchelewesha Malipo ya Mkandarasi?! Kwa nini?!
b) Kama hadi Novemba/Desemba 2020 Mkandarasi alikuwa anawasilisha Maombi ya Malipo (through Valuation Applications), bila kuonyesha kwamba kuna Ucheleweshaji wowote. Na Serikali ikawa ina-certify Malipo na kumlipa, sasa mbona hapo ndipo ilipojificha Hoja kwamba Madai ya Mkandarasi kuhusu sababu za Ujenzi kuchelewa zina utata mkubwa sana. Hapo ndipo kwenye Hoja za ziada za kumbana Mkandarasi kwa kuficha Ucheleweshaji wa Ujenzi.
c) Maswali: Je, Msimamuzi Mkuu wa Mradi aligundua kupitia Interim Payment Certificates (na mbinu zingine) kwamba Mkandarasi amepunguza Kasi ya Ujenzi?! Je, alichukua hatua gani za kimkataba kulinda Maslahi ya Serikali?! Je, kuna Site Instructions zozote alizomwandikia Mkandarasi kuhusiana na hili?!

22) Site Meetings!

a) Site Meetings ni Mikutano ya Saiti ambayo kwa kawaida hufanyika kila baada ya wiki 4 ikijumuisha pande zote za Mkataba. Pande hizi ni Serikali na Timu yake ya Wasimamizi na Mkandarasi na Timu yake nzima.
b) Minutes hutayarishwa baada ya kila Site Meeting na pande zote huthibitisha Minutes hizi.
c) Kila Site Meeting Mkandarasi huwasilisha Detailed Contractor's Progress Report akionyesha Maendeleo ya Mradi against the Programme of Works.
d) Swali! Ningependa kujua ni lini kwa mara ya kwanza (tarehe) Mkandarasi alianza kutoa Taarifa na kuonyesha kwamba Mradi utachelewa (warning) na kwamba sasa Mradi umeishaanza kuchelewa (reality)?! Nataka kujua Minutes of Site Meetings zinaonyesha nini kuhusu hilo. Hii ni Hoja muhimu sana unapotaka kumbana Mkandarasi kwa kutumia Project Documentation. Ushahidi toka kwenye Nyaraka za Mradi.
e) Maswali! Hivi ni lini, kwa mara ya kwanza, Mkandarasi aliitaarifu rasmi Serikali kuhusu Mradi kuchelewa?! Mkandarasi alitoa sababu zipi na alisema Mradi umechelewa kwa kiasi gani?! Mkandarasi aliahidi kuchukua hatua gani kuzuia Ucheleweshaji huo usiendelee?! Serikali ilijibu nini?!

23) Site Instructions!

a) Namna nyingine ya kumbana Mkandarasi kwa Ushahidi wa Nyaraka za Mkataba kwamba yeye ndiye aliyechelewesha Ujenzi ni kwa kutumia Site Instructions.
b) Kama Timu ya Usimamizi wa Mradi inafanya kazi yake vizuri na kwa mujibu wa Mkataba, basi itakuwa iligundua mapema sana mara Ujenzi ulipoanza kusuasua. Na ilichofanya itakuwa ni kumpa Site Instructions Mkandarasi ili aongeze kasi. Sasa huu ndio Ushahidi unaoondoa ubishi. Swali: Je, nakala ya hizo Site Instructions zipo?!
c) Tafadhali rejea pia nilichoshauri hapo juu kuhusiana na kilichoitwa "Ushauri wa Serikali".

24) Siasa!

a) Siasa ziwekwe pembeni. Mara nyingi "Siasa" ndio Sumu inayoharibu baadhi ya Miradi ya Ujenzi Nchini, hasa hii mikubwa. Ashakum si matusi.
b) Tatizo la Wanasiasa kujigeuza Wasemaji wa Miradi ni kwamba, pamoja na mambo mengine, wakiisharopoka mambo ambayo si sahihi kitaalam/kimkataba, wengi wao kuwa na tabia ya kutaka ukweli huu usijulikane at whatever cost. "Whatever cost" ni pamoja na "kuwalazimisha" au kusababisha Wataalam/Wahandisi wa Mradi waseme uongo na kupindisha Ripoti zao ili kuwalinda.
c) Mfano hili Suala la Cranes...! Swali: Hivi Serikali inahusika vipi hadi Waziri Makamba kujigeuza Msemaji wa Mkandarasi wakati ni wazi Mkandarasi kachemsha kwa labda kuchelewa kuagiza Mitambo na Vifaa (Plants and Equipment)?! Jamani huu sio Mradi wa Force Account ambapo Mwalimu Mkuu na Mkuu wa Wilaya wananunua materials and equipment... simenti na milango! Nimekumbuka video clip ya Mheshimiwa fulani!

25) Umoja ni Nguvu!

a) Ni matumaini yangu Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ataona umuhimu wa kujumisha Nguvu, Utaalam, Maarifa na Ushauri wa Mawaziri wapya na Mawaziri wa zamani wa Ujenzi na wa Nishati ili kuepuka maamuzi ya kukurupuka kuhusu Mradi huu.
b) Hakika Umoja ni Nguvu.

26) Vinginevyo, kwa picha nayoipata, Nchi inaweza kupata hasara kubwa sana ambayo ingeweza kuepukika kwa kupitia Umoja na Ushirikiano wa Kitaalam baina ya Viongozi wetu wanaoujua vizuri Mradi. Continuity ni kitu muhimu sana kwenye Mradi mkubwa kama huu, hasa unapoanza kusuasua.

27) Tusisahau kwamba bado Siasa, Ufisadi na Uzembe ni matatizo sugu Nchini, na hasa kwenye Miradi mikubwa.

28) Hitimisho!

a) Nimekutana na Kipeperushi cha UVCCM ambacho kina picha nzuri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na nukuu ya maneno yake yafuatayo:
"Uzalishaji (nadhani anamaanisha Ujenzi - nyongeza yangu) wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere unaendelea vizuri na umefikia asilimia 55.6 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 996.76 zimetumika kwenye Mradi huo katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Septemba, 2021." Kipeperushi kinaonyesha kwamba Rais Samia alitamka maneno haya Oktoba 10, 2021.
b) Kwa kuzingatia kauli ya Waziri wa Nishati (Mheshimiwa January Makamba) Bungeni na hii Taarifa ya Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ya Oktoba 2021, inaelekea Mheshimiwa Rais Samia hakuwa na Taarifa Sahihi (aliongopewa?!) kuhusu Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere!
c) Maswali: Hii ajali imetokeaje?! Nani aliyemuongopea Mama Samia kwa kumwambia "Mradi unaendelea vizuri" wakati kuna matatizo lukuki ikiwamo Ucheleweshaji wa Ujenzi kwa mwaka mmoja na miezi karibu minne?! Siku 477!! Au, labda, hakukuwa na co-ordination kati ya Ikulu na Wizara ya Nishati?! Kwa kweli nashindwa kuelewa!
d) Ni matumaini yangu kwamba Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan atachukua hatua atakazoona zinafaa kwa haraka sana ili kuulinda Mradi huu na kuilinda Serikali na Nchi tusipate hasara kubwa zaidi bila ulazima.
e) Bado naendelea kujiuliza, iwapo kweli Mradi umechelewa kwa siku 477 (mwaka mmoja na miezi kama 4), mbona badala ya Bwawa kujazwa maji kesho tarehe 15.11.2021 (kama alivyoabidi Mheshimiwa Waziri Kalemani), Mheshimiwa Waziri Makamba anasema litajazwa maji mwezi Machi 2022, kama miezi 3 na nusu tu baadae?! Najiuliza tu kwa sauti!
f) Nimetumia Makala yangu hii kujadili Mradi huu na kutoa Ushauri wangu wa kitaalam ili kuisaidia Nchi yangu na Viongozi wetu kwa nia njema. Samahani sana iwapo sehemu yoyote nimetoa Ushauri au Hoja zisizostahili kutokana na kutoujua Mradi kwa undani (au kwa sababu ya Taarifa za Waziri/Wizara kutokuwa sahihi)!
g) Nashindwa kujizuia kutamka kwamba Mpambano unaoendelea kufuka moshi kati ya Awamu ya 6 na Awamu ya 5 hauna maana na unaiumiza Nchi. Na unaweza kusababisha hasara kubwa sana. Sijui Mama Samia atasaidiaje kuweka mambo sawa?!

29) Ahsante.

30) MUNGU IBARIKI TANZANIA!

BJC. DSM. 14.11.2021. 1915hrs.

Reposted on 15.11.2021 (1930hrs) with some minor corrections.

Reposted on 16.02.2022. 0432hrs.
 
Waziri anasema eti bei ya mafuta imepanda kwenye soko la Dunia kwakua kuna tension ya vita kule Russia na Russia ni mmoja ya nchi inayouza mafuta kwa wingi.

Toka lini sisi tunanunua mafuta toka Urusi??

Na je hiyo tension ya vita imeathiri vipi production ya oil duniani??

Angezungumzia vita Iraq, Saudi Arabia na nchi nyingine za kiarabu ambazo ni major producers wa oil ningemuelewa ila sio kutudanganya na Urusi.
Bwana Stroke (Naamini wewe ni Me) inapotokea tension kwenye nchi yoyote inayozalisha mafuta, Kuna hatari ya Bei ya mafuta kupanda au kushuka. Russia ni mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani, ikitokea lolote linaloweza kusababisha kuongeza au kupunguza uzalishaji wa mafuta, tegemea athari zake zitaonekana sokon la Dunia na hii hata hapa Tz Bei itabadlika, HATA KAMA TANZANIA HAINUNUI MAFUTA KUTOKA RUSSIA.
Bei ya mafuta inazidi kupanda sokoni.
Screenshot_20220216-210056.jpg
 
Bwana Stroke (Naamini wewe ni Me) inapotokea tension kwenye nchi yoyote inayozalisha mafuta, Kuna hatari ya Bei ya mafuta kupanda au kushuka. Russia ni mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani, ikitokea lolote linaloweza kusababisha kuongeza au kupunguza uzalishaji wa mafuta, tegemea athari zake zitaonekana sokon la Dunia na hii hata hapa Tz Bei itabadlika, HATA KAMA TANZANIA HAINUNUI MAFUTA KUTOKA RUSSIA.
Bei ya mafuta inazidi kupanda sokoni.View attachment 2121381
Russia Ukraine tensions sio reason ya kupanda kwa bei ya mafuta soko la dunia.

Bei ilikua imeathirika kabla hata ya kuanza kwa huo mgogoro

Hivyo Bwn. Waziri hapo katoa taarifa ambayo si sahihi.
 
January kaongea ukweli sio tuu wanambana bali Wana chuki binafsi ,huo ndio ukweli.

Kamati Ya nishati ina fursa zote za kuhoji yeyote ikiwemo kumuita mtendaji mkuu.
Kwa hiyo wizara yake haitakiwi kuulizwa maswali bungeni?
Basi wafute kipindi Cha maswali na majibu.
Empty kabisa huyo
 
Mkuu wababayangu!

Kuhusu makamba kukagua vina vya mito na mabwawa ya maji kwa kutumia HELIKOPTA!

Mimi binafsi niliwahi kujiuliza sana bila majibu.

Utawezaje kujua kina cha maji ukiwa Angani.
Mbaya zaidi kila siku anabadili majibu ya tatizo la kukatika kwa umeme

Kwa kipindi chote cha JPM maintenance ya mitambo haikufanyika kwa sababu ya watumishi kuogopa kutumbuliwa

Mabwaya yamekauka maji

Juzi kaja na mpya kuwa nyaya za umeme zinagawa umeme kwa distance ndefu kinyume na inavyotakiwa kitaalam.

Jinga sana huyu mtu. Hii kupeana madaraka makubwa ili kumridhisha mtu tutakuwa tunaenda hatua 3 mbele tunarudi hatua 5 nyuma
 
Back
Top Bottom