Waziri Makamba ujue siyo kila kitu ni cha kubinafisisha

Waziri wa Nishati January Makamba ajulishwe kuwa kwenye taifa siyo kila kitu ni cha kubinafisishwa kwa masilahi mapana ya taifa.
  • Umeme
  • Bandari
  • Reli
  • Viwanja vya ndege
  • Mbuga etc
Baba wa taifa Mwl Nyerere kwenye hotuba yake moja mwaka 1995 alikemea vikali akili ya kuchukua mali ya uma na kuwakabidhi watu wachache, mfano umeme ndiyo injini ya uchumi wa nchi kwa kuvutia kujengwa kwa viwanda vingi na kuzalisha bidhaa za bei ndogo zitakazoshindana kwenye soko, kamwe hatuwezi kuwapa watu wachache watufanyie biashara kwa kutuuzia umeme alafu tukategemea bidhaa zetu zishindane kwenye soko la Dunia.

Enzi za Kikwete Tanesco nusura ibinafisishwe baada ya kuwa na madeni makubwa ya kulipia capacity charges kutoka kwenye generator za kampuni la symbion.

Alipoingia Magufuli akafuta baadhi ya mikataba ya hovyo na kuliwezesha shirika kukusanya zaidi ya trillion 2 kwa mwaka hivyo likaacha kujiendesha kwa kutegemea ruzuku ya serikali na kufuta mpango wa kulibinafisisha shirika hili la uma.

Ameingia rais Samia na alipomteua waziri January Makamba tayari ameingia na mentality ileile ya enzi za Kikwete.

1. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo hawaagizi nguzo nje ya nchi kama walivyokuwaga wanafanya huko nyuma lakini bado Makamba anataka shirika libinafisishwe.

2. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo wanakusanya zaidi ya trillion mbili kwa mwaka lakini bado waziri Makamba anataka shirika libinafisishwe!

3. Pamoja na kwamba kupitia REA Tanesco imetapakaa nchi nzima lakini bado waziri anataka shirika libinafisishwe.

4. Pamoja na kwamba sasa hivi Tanzania inajenga bwawa kubwa kabisa la kufua umeme lakini bado waziri anataka Tanesco ibinafisishwe.

Hii speed ya 4G ya Makamba kutaka Tanesco ibinafisishwe inasukumwa na nini? Hivi kwa akili hii vipi huyu Makamba angeshinda urais mwaka 2015?
Hivi ni wapi makamba kasema anataka kubinafsisha tanesco?na hata kama ana huo mpango kwani ana mamlaka gani ya kufanya huo uamuzi peke yake?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kama mradi wa tanesco aliouacha mwendazake pale rufiji ukiwa na aina yoyote ya mashirikiano na mabebex tutalaanika
 
Timu gaidi meno yote nje kwa furaha kwa sababu hao boda boda na bajaji vyuma vimelegea hela zitajaa mifukoni mwao baada ya kufukuzwa mjini
 
Waziri wa Nishati January Makamba ajulishwe kuwa kwenye taifa siyo kila kitu ni cha kubinafisishwa kwa masilahi mapana ya taifa.
  • Umeme
  • Bandari
  • Reli
  • Viwanja vya ndege
  • Mbuga etc
Baba wa taifa Mwl Nyerere kwenye hotuba yake moja mwaka 1995 alikemea vikali akili ya kuchukua mali ya uma na kuwakabidhi watu wachache, mfano umeme ndiyo injini ya uchumi wa nchi kwa kuvutia kujengwa kwa viwanda vingi na kuzalisha bidhaa za bei ndogo zitakazoshindana kwenye soko, kamwe hatuwezi kuwapa watu wachache watufanyie biashara kwa kutuuzia umeme alafu tukategemea bidhaa zetu zishindane kwenye soko la Dunia.

Enzi za Kikwete Tanesco nusura ibinafisishwe baada ya kuwa na madeni makubwa ya kulipia capacity charges kutoka kwenye generator za kampuni la symbion.

Alipoingia Magufuli akafuta baadhi ya mikataba ya hovyo na kuliwezesha shirika kukusanya zaidi ya trillion 2 kwa mwaka hivyo likaacha kujiendesha kwa kutegemea ruzuku ya serikali na kufuta mpango wa kulibinafisisha shirika hili la uma.

Ameingia rais Samia na alipomteua waziri January Makamba tayari ameingia na mentality ileile ya enzi za Kikwete.

1. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo hawaagizi nguzo nje ya nchi kama walivyokuwaga wanafanya huko nyuma lakini bado Makamba anataka shirika libinafisishwe.

2. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo wanakusanya zaidi ya trillion mbili kwa mwaka lakini bado waziri Makamba anataka shirika libinafisishwe!

3. Pamoja na kwamba kupitia REA Tanesco imetapakaa nchi nzima lakini bado waziri anataka shirika libinafisishwe.

4. Pamoja na kwamba sasa hivi Tanzania inajenga bwawa kubwa kabisa la kufua umeme lakini bado waziri anataka Tanesco ibinafisishwe.

Hii speed ya 4G ya Makamba kutaka Tanesco ibinafisishwe inasukumwa na nini? Hivi kwa akili hii vipi huyu Makamba angeshinda urais mwaka 2015?
Ni ujuha tu kuwa na mali za umma.

Mataifa yaliyoendelea kiuchumi kila kitu kinachowezq kufanywa na watu binafsi ni huru kuyafanya isipokua yale wasioweza kuyafanya watu binafsi. Yote uliyoyataja nchi nyingi duniani ni ya watu binafsi.

Serikali inabaki kutunga sheria tu na kuwa "facilitators" sio waendeshaji.
 
Huu unatakiwa kuwa mjadala mpana kwa sababu kadhaa. Kwa mfano, dhana ya kubinafsisha kimsingi haina ubaya katika taifa lakini Watanzania wanao uwezo huo au vipi, na kama uwezo wao ni mdogo watawezeshwaje. Pengine, tunalo la kujifunza kutoka kwenye mfumo wa uchumi wa China ambapo serikali ni mbia Mkuu kwenye sekta zilizoainishwa na aliyeibua mhadala huu.

Waziri wa Nishati ana maoni yake. Tujadiliane hatimaye tutafikia muafaka kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Walishawezeshwa na bado wanawezeshwa. Labda huelewi tu.

Unataka kuwezeshwa kwenye lipi tukupe darsa..
 
Back
Top Bottom