Waziri Makamba,tekeleza ahadi yako

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Suala la bomoabomoa si suala la kisiasa. Na halipaswi kutumiwa hivyo. Wananchi walioathiriwa na zoezi hilo wanaendelea kuteseka na kusubiri Serikali kuwasaidia hata kwa kuwaambia waende wapi.

Ulaghai na uongo haupaswi kufanyika kwenye suala kama hili. Kuwalaghai wananchi hawa wa mabondeni ni kuwaongezea hasira na mateso.

Imesemwa kuwa Waziri Januari Makamba uliwaahidi wananchi hao kuwapa nauli na kodi ya pango ya miezi sita huku masuala yao yakishughulikiwa. Lakini,hadi sasa Waziri Makamba ameingia mitini. Uko wapi? Nani alikutuma kusema vile? Lengo lilikuwa nini? Si vyema kulaghai wenye hasira!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Lete ushahidi wa ahadi ya Makamba vinginezo utakuwa na Elimu ya hapa na pale!
 
Watanzania tusipokuwa tayari kutatua tatizo la ujengaji holela, basi miaka 200 ijayo bado tutakuwa tunashuhudia familia zinakufa kwa ajali ya moto eti kwasababu fire-fighters wameshimdwa kufika kwenye eneo la tukio sababu ya mipangilio mibovu ya nyumba.
Pia tuwe tayari kuona kila mwaka familia zinateketea kwa mvua za misimu na mafuriko. Pia tuwe tayari kuendelea kuona familia zinakatika kwa magonjwa-mlipuko.
Hili suala halipaswi kuwa la kisiasa!
 
Suala la bomoabomoa si suala la kisiasa. Na halipaswi kutumiwa hivyo. Wananchi walioathiriwa na zoezi hilo wanaendelea kuteseka na kusubiri Serikali kuwasaidia hata kwa kuwaambia waende wapi.

Ulaghai na uongo haupaswi kufanyika kwenye suala kama hili. Kuwalaghai wananchi hawa wa mabondeni ni kuwaongezea hasira na mateso.

Imesemwa kuwa Waziri Januari Makamba uliwaahidi wananchi hao kuwapa nauli na kodi ya pango ya miezi sita huku masuala yao yakishughulikiwa. Lakini,hadi sasa Waziri Makamba ameingia mitini. Uko wapi? Nani alikutuma kusema vile? Lengo lilikuwa nini? Si vyema kulaghai wenye hasira!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Pole alienda kuuza sura,lakini moyoni alienda kuwaambia mtaisoma number
 
Makamba peleka kodi ya pango uliyoiahidi

Mzee Tupatupa
Lakini kama uongo mbaya na hatari kama huo aliyempa ajira kaunyamazia hizo sio dalili kuwa alitumwa aseme ili kutuliza upepo?
Tupatupa pamoja na kumlaumu January unapaswa kuliangalia tukio hili kwa mapana maana limeichafua sana serikali ya chama chako na kuonyesha kuwa katika swala la Utu hawana tofauti na Makaburu wa SA wakati wa Botha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom