Waziri Makamba: TANESCO mpya imezaliwa leo, tunataka iendeshwe kibiashara

Kabisa Mkuu Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana ameinusuru nchi yetu kwa maovu mengi ya kutisha nchini kwa kumnyakua yule dhalimu.,

To hell with this dictator. Ameharibu sana Nchi yetu, Mungu ametupenda kwa kumpeleka jehanamu mapema
 
Mkuu samahani sana kukwambia ukweli Ila kiuhalisia huelewekagi unataka nini.. ni kama mwanamke malay.a, alitokea mtu akawa na bidii ya kumaliza tatizo la umeme ukawa unashinda mitandaoni kumwombea mabaya leo hii bila aibu upo unalialia kama mtoto yatima. Nakufananisha na machinga fulani rafiki zangu ambao mwaka Jana walikuwa bize kumshangilia Lissu eti NI YEYE, mara tunataka demokrasia na Uhuru wa kujieleza huku wakikandia vitambulisho vya elfu 20. Juzi wamefulumushwa kariakoo wanaanza kulaani nikawakumbusha ndo demokrasia waliokuwa wanalilia. Kwa kumalizia nakukumbusha, hakuna kiongozi wa nchi atakayeweza kumaliza shida zote za wananchi, angalia mwenye nafuu mpe sapoti.. vinginevyo endelea kulialia mpaka uingie kaburini.
Kwani lisu ndiyo amekuwa rais kwamba ndiyo yeye anayewakimbiza huko kkoo baada ya kumchagua kwamba wamepotea njia kumchagua lisu Leo anawanyanyasa??

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.

Mhe. Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.

Aidha Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu, Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na Bw. Christopher Gachuma.

Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.

"Tunataka baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora, yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.

"Nimhakikishie Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili", " alisema Bw. Maharage Chande

Meneja Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.
Wizara ya Nishati chini ya Waziri Makamba na TANESCO yake HAWAWEZI kufanya lolote positive kwa kipindi chote Waziri Makamba na Bodi yake ya TANESCO watakapokuwa madarakani. Watakaonipinga , tusubiri 2025na baada ya muda wa Bodi kuisha tufanye tathmini.
 
Zitto wa Zambarau alisema mabadiliko wizara ya nishati ni pele limepata mkunaji!
 
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.

Mhe. Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.

Aidha Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu, Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na Bw. Christopher Gachuma.

Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.

"Tunataka baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora, yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.

"Nimhakikishie Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili", " alisema Bw. Maharage Chande

Meneja Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.
 
Kauli yake ilikua promising kwamba hatimaye sasa tumepata mwarobaini wa changamoto za kutokua na umeme wa uhakika.

Whatever happened to that.
 
Uliona wapi dili na huduma bora vinakaa chumba kimoja?
Dili akiwa jikoni
Huduma nzuri amefungiwa store.
Ila muambieni kipara, nimekuja shamba huku Kigelo Kongowe Kibaha. Pwani. nategemea kulala hukuhuku, kwamba hakuna UMEME tangu mchana saa hii Ni saa 8:43 pm
 
Pole Sana
Kumbuka wakati wa ges walisemaje na ikawaje?

Gesiwana nunua kwa wazungu ndio tunapata umeme lazima bei iwejuu sababu gas hatupati bure.

Umeme wa rufiji wakisema bei itadhuka naelewa sababu katika uzalishaji maji ni bure.
 
Kabisa Mkuu Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana ameinusuru nchi yetu kwa maovu mengi ya kutisha nchini kwa kumnyakua yule dhalimu.,

Punguza mahasira ndugu utakuwa kichaa bila kujijua.
 
Hii Wizara bora angepewa tu Prof Muhongo, Huyu ndiyo alianzisha Sera ya umeme kutokatika ovyo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom