Waziri Makamba: Serikali ya Rais Samia haina mpango wa kukodi mitambo ya umeme wa mafuta

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,863
3,190
Akiongea baada ya kuzuru bwawa la Mtera Januari Makamba, Waziri wa Nishati ametoa ufafanuzi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita haina mpango wa kukodi mitambo ya kuzalisha umeme wa mafuta.

Amefafanua kuwa hii imetokana na historia mbaya ya mitambo hiyo ambayo huko nyuma kumekuwepo na mivutano kati ya Serikali na wamiliki wa mitambo hiyo.

January Makamba amefafanua kuwa Serikali ya Rais Samia imedhamiria kuongeza nguvu kwenye uzalishaji wa umeme wa bei nafuu tofauti na umeme wa mafuta ambao ni gharama kubwa ili kudhibiti tatizo la umeme. Nguvu zaidi zinatarajiwa kuongezwa kwenye umeme wa upepo, gesi na maji katika mabwawa yote ya uzalishaji wa umeme.
 
Bado anatuchota akili aone tuta panic kiasi gani ,anatupitishia ajenda ya umeme wa upepo mdogo mdogo
 
Back
Top Bottom