Waziri Makamba jiuzulu, siku 10 za mgao wa umeme kupisha marekebisho zilishaisha ila umeme bado unakatika

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,499
4,211
Inashangaza sana kuona kiongozi wa Wizara nyeti kiasi hiki anatangaza mgao wa siku 10 akiaminisha wananchi kwamba marekebisho yanafanyika na baada ya hapo umeme utakuwa sawa

Cha kushangaza hata baada ya muda huo bado umeme ni wa kusua sua.Je ni sahihi kusema kwamba kazi haikufanyika? Kama haikufanyika nani awajibishwe?

Tuliaminishwa marekebisho hayakufanyika awamu iliyopita na sasa marekebisho yamefanyika lakini cha kushangaza hali ya umeme sasa ni mbaya kuliko hapo awali.

Pamekuwa na visingizio vingi visivyo na tija.Mpaka helicopter ilitumika kutuhakikishia mvua zimepungua hivyo mabwawa yamepungua,Jambo lililokuja kudhihirika kwamba si kweli.Tukaambiwa hakuna crane ya kubeba tani 80 .Pia ikathibitishwa kuwa uongo.

Hali hii inasikitisha sana

Je, kwa hali iliyopo
 
Nilikuwa nasikiaga mabwawa yanachepushwa maji yapungue sasa naamini tangu hii awamu ianze sana INA hamu sana na mgao Semaa mvua ziliwaumbua
 
Nimeona kupitia Al jazeera kwamba kutakuwa na hali ya upungufu wa nishati katika maeneo mbalimbali duniani kufuatia vita ya Russia na Ukraine na vikwazo vilivyowekwa.

Tanzania iko duniani ndio nauliza hii katika katika ya umeme wiki hii ni kwa sababu ya vita?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mhe. Waziri alituaminisha kuwa utafanyika ukarabati kwa muda wa wiki mbili na umeme utarudi kama uilivyokuwa tangu zamani. Tulifurahi sana kwa kauli ya Mhe. Waziri lakini cha kushangaza mambo yamekuwa tofauti kabisa. Nitoe mfano hapa Mwanza eneo la Mwananchi. Jana umeme ulikatwa mida ya saa moja kamili za usiku na umeme ukarudi kama saa saba za usiku. Ifahamike kuwa kuanzia saa moja usiku ndiyo muda wa kutayarisha mlo wa usiku, kusali, watoto wa shule kufanya mazoezi waliopewa shuleni, n.k. sasa inakuwaje umeme unakatwa muda ambao vitu vya muhimu vinatakiwe vifanyike?. Wakati wa Hayati Mhe. Magufuli umeme ulikuwa haukatiki mbona awamu hii tunaona mambo yakiwa tofauti. Nashauri Mamlaka ya uteuzi uangalie kwa maakini nafasi ya Waziri wa Nishati na Meneja Mkuu wa Tanesco. Kwa maeneo wanapoishi wananchi wa kawaida ni vema umeme ukatwe mchana na siyo usiku.
 
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
 
Jamaa huwa Naamini uwezo wake ni Mdogo sana. Wengi tulivyokuwa tukimuamini tulipotea!
 
Yani huwaga nachoka na majibu ya huyu taneco wa jf eti upo eneo gani na namba zako za simu hivi inamaana hawajui kama umeme unakatika karibu nchi nzima
 
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
wiki 2 nzima umeme unakatika asubuhi na kurudi usiku saa 4, kila baada ya siku mbili
kuja kubaini ni kwamba mnabadili nguzo lakini hamkutoa taarifa

mbona mnakua mazuzu ivi, mnapiga kimya ili iweje ? mtoe taarifa na ratiba kabisa tujue tunajipangaje
pumbav
 
Hujajibu swali lake bwashee!
 
🐒🐒🐒
0_20220223_195313.jpg
 
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
Wacha nijibu kwa niaba yake;

Mimi naishi dar nipo wilaya ya ilala msongola namba ya simu ni 0783721337 jana kati ya majira ya saa tatu na saa nne asubuhi umeme ulikatika na kurudi saa moja kasoro usiku pia juzi mchana kati ya majira ya saa sita ulikatika na kurudi mchana kama kwenye saa nane hatukuwa na taarifa yoyote,pia maeneo yote jirani kama kivule,kitonga,mvuti na chanika kote tulikosa umeme naomba majibu ya hili tatizo lilikuwa ni nini na kwann mlituaminisha kuwa zile siku kumi mlituaminisha kuwa kukatika kwa umeme kutakuwa ni historia?!!!! TANESCO
 
Back
Top Bottom