Waziri Makamba: Iwe Mjini au Kijijini Gharama wanayatumia Tanesco kumuingizia mtu umeme ni Tsh 800,000

KWa iyo leo nikitaka unganishiwa umeme inakua sh ngapi, ?
Waziri wa Nishati January Makamba amemshukuru Rais Samia kwa kuwapa tsh 500bil kwa ajili ya ukarabati wa Miundo mbinu ya Umeme, jumla ya Fedha inayohitajika ni zaidi ya tsh trillion 1

Makamba amesema iwe Mjini au Kijijini Gharama za kuunganisha Umeme wanazotumia Tanesco ni tsh 800,000

Source ITV Dakika 45
 
Waziri wa Nishati January Makamba amemshukuru Rais Samia kwa kuwapa tsh 500bil kwa ajili ya ukarabati wa Miundo mbinu ya Umeme, jumla ya Fedha inayohitajika ni zaidi ya tsh trillion 1

Makamba amesema iwe Mjini au Kijijini Gharama za kuunganisha Umeme wanazotumia Tanesco ni tsh 800,000

Source ITV Dakika 45
Mpendwa Mteja !

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 320,960/=,

Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,

Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=

Aidha, gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,

Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,

umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
 
Naiomba serikali itunge sheria kuruhusu wananchi kutengeneza umeme wao binafsi.

Maana huu wa tanesco sasa haufai tena.

Hapa ni kung'oa mita na nyaya zao tu.

Mtu unaendelea na mambo yako.
 
Huyu jamaa vipi ??

Mbona BICHWA lake limejaa upaa na Tope tu.

Yaan Umeme wa REA, nao kumuunganishia Mwananchi Kijijini Unamtoza LAKI NANE ???.


Huyu Jamaa kumbe ni kenge namna hii

Yaan Mtu wa Mjini mwenye Mjengo wa zaidi ya Milion 200+ .

Na wakijijin mwenye Kajumba lake ka Milion mbili na tofali kafyatua mwenyewe , naye Umeme atumie LAKI NANE .


.
 
Huyo Makamba huonekana yupo smart akiwa amekaa kimya tu.

Akiongea ni pumba au upupu au vyote!

Haiwekani gharama ikawa ileile kwa kila mteja ilhali wengine hawahitaji hata nguzo huku wengine ni three phase.

Hii wizara inahitaji mtu makini siyo sampuli ya Makamba.
 
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi makini Mungu wa mbinguni awabariki

Mods naomba pandisha huu ufafanuzi pale juu kwa faida ya wote
Okay Haina shida muda siyo mrefu nitaupandisha huu ufafanuz hapo juu kwa faida ya wote. Msalimie profesa mgaya
 
Back
Top Bottom