Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Pamoja na yoteyote binafsi ya Makamba Jr.

Naona yuko kwenye pressure sana, either kuna watu wanataka afeli au tayari mbio za Urais zimeanza kuna watu wanataka wamuharibie, maana kila kukicha linazuka jipya.

Makamba Jr kuwa mtulivu inaonekana upo kwenye vita kali, tumia akili kwenye kufanya mambo yako, hiyo wizara ni kubwa na ina mambo mengi, uko mtegoni.
Ona jinga hili
 
Makamba anadhani nchi hii yuko peke yake. Ukweli ni huo uliosemwa na Mataragio. Pamoja na bei kuwa juu, kampuni za mafuta zinapata hasara kwa miezi miwili sasa kutokana na bei elekezi kuwa chini. Jamaa wameiambia Serikali wataagiza mafuta kama watakubali kuwafidia hasara wanayopata kwa sasa.
 
Huenda Dk James Mataragio ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TPDC akafutwa kazi kwa kile kilichosemwa na Makamba ni kuupotosha umma.

James, hivi karibuni alinukuliwa akisema endapo meli ya mafuta isipotia nanga ndani ya wiki mbili Nchi itashuhudia uhaba mkubwa wa mafuta jambo ambalo limeonekana kumkwaza Makamba.
Mimi nadhani alitaka kuweka worse case scenario kwamba ikitokea meli haijafika ila alikosea sababu bulk system ndio wanajukumu hilo kuhakikisha wale walioshinda tender wanaleta kwa wakati na hii imekuwa toka 2012 sasa mkurugenzi wa TPDC hii sio kazi yake kusemea serikali nadhani ameshajuwa kuna chance TPDC wakarudishiwa wao wawe kama waagizaji pekee kitu ambacho hakitatokea wameshanusa ulaji sasa wamefufuka. Kwa kauli hii mkuregenzi wa TPDC kaingilia mamlaka sio yake kabisa maana hata yeye na kampuni yake wameshinda tender kwa kushindana na wengine hawakupewa tu kama zawadi. Waziri yuko sahihi jamaa kachemka ila naamini hakuwa na nia mbaya ila hakuliweka sawa na vile waandishi wetu hawa wanadaka moja baya tu.
 
Huenda Dk James Mataragio ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TPDC akafutwa kazi kwa kile kilichosemwa na Makamba ni kuupotosha umma.

James, hivi karibuni alinukuliwa akisema endapo meli ya mafuta isipotia nanga ndani ya wiki mbili Nchi itashuhudia uhaba mkubwa wa mafuta jambo ambalo limeonekana kumkwaza Makamba.
Mimi sioni kosa la mkurugenzi hapo.
Yeye kaeleza kitakachotokea endapo Meli itapata tatizo.

Hilo linawezekana na mfano mzuri ni Zanzibar; walipoanzisha utaratibu kama huo wa serikali kuagizamafuta ili kuwa ikitokea uhaba wa mafuta pale Meli ilipopata hitlafu ama kuchelewa. Walioko Zanzibar ni mashahidi wa hili
 
wafuasi wa Chadema kama kawaida yao na tabia zao za kigaidi za kutaka nchi iwe ktk taharuki na shida,
muda wote wao wanataka habari mbaya ziikumbe Tanzania.
kweli nimeamini wafuasi wa mboe wana chembe chembe za kihalifu.

ukiwafuatilia wafuasi wa mboe utagundua mara zote kunapokuwa na tatizo kama nchi basi huwa wao wana shangilia sana.
hawa watu ni hatari sana, mwaka 2025 hawafai hata kupata kiti kimoja cha ubunge.
 
Huyu makamba kaanza kutengeneza vitisho kwa wataalamu, tukiweka hapa CV yake na ile ya mataragio utaelewa tu ni nani anayeongea jambo lenye mantiki, Nyerere aliharibu sana hii nchi kwa kuwapa nguvu wanasiasa.......mwanasiasa mwenye elimu ya kuunga unga anaweza kukurupuka tu na kuanza kuongea maswala yanayotakiwa kutolewa ufafanuzi na wataalamu.....​
 
Naam.
Screenshot_20211112-140319.jpg
 
Back
Top Bottom