Waziri Majaliwa apiga marufuku kilimo cha mkataba asema kinawanyonya wakulima

ibra blogger

Member
Jan 19, 2018
13
22
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa sababu kinawanyonya wakulima.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya Hunyari wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.

“Ni marufuku kwa wanunuzi wa pamba kulima pamoja na wakulima kwa sababu wakulima wanakosa uamuzi wa kupanga bei. Kuanzia sasa zao hilo litauzwa kwa njia ya mnada.”amesema Majaliwa

Amesema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeamua kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba, pembejeo hadi masoko.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo katika wilaya hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu itakayowawezesha kulima kwa kufuata njia bora za kisasa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo lao
 
Ningekuwa mimi ndo nafanya maamuzi ningeweka mazingira rafiki kwa wakulima na wafanyabiashara ili kusiwepo kunyonyana. Mfano kama mkulima amewekeza nguvu zake na ardhi na mfanya biashara akaleta utaalam wake na vitendea kazi kama tractors kwanini hii joint venture isiwe isikubaliwe.

Kama kilimo kiboreka hadi kwenye kilimo cha kisasa yaani cha umwagiliaji nahisi ingekuwa bora zaid. Serikali ingezibana pande zote mbili kwa influence iliyonayo kupelekea makubaliano yenye tija hata kama makubaliano ya awali hayakuwa hivyo.

Swala la kuchagua uuze wapi au usiuze wapi ni jambo ambalo si la muhimu sana kama mkulima ananufaika na kilimo cha mkataba kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima amekifanya miaka 50 bila mafanikio ya kimaslahi. Mapinduzi ya kilimo.yananza na wakulima wenyewe.
 
Huku nilipo serikal imekaza kwe nye klmo cha pamba . Ukilima bila mistari jela.
 
watafanya mnada kama kwenye korosho?

wafanye sarakasi zote ila bei tu ya kununulia iwe kubwa kuliko ya msimu uliopita
 
Ningekuwa mimi ndo nafanya maamuzi ningeweka mazingira rafiki kwa wakulima na wafanyabiashara ili kusiwepo kunyonyana. Mfano kama mkulima amewekeza nguvu zake na ardhi na mfanya biashara akaleta utaalam wake na vitendea kazi kama tractors kwanini hii joint venture isiwe isikubaliwe.

Kama kilimo kiboreka hadi kwenye kilimo cha kisasa yaani cha umwagiliaji nahisi ingekuwa bora zaid. Serikali ingezibana pande zote mbili kwa influence iliyonayo kupelekea makubaliano yenye tija hata kama makubaliano ya awali hayakuwa hivyo.

Swala la kuchagua uuze wapi au usiuze wapi ni jambo ambalo si la muhimu sana kama mkulima ananufaika na kilimo cha mkataba kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima amekifanya miaka 50 bila mafanikio ya kimaslahi. Mapinduzi ya kilimo.yananza na wakulima wenyewe.
Na wakulima wengine wanaingia ubia kwa kuwa hawana zana na pesa za kuhudumia zao, wakati wafanya biashara wana pesa ila hawana Ardhi.
 
Serikali isiwaingilie Wakulima. Km ni hivyo wawape na mikopo na kuwatafutia Masoko. Mwaka uliopita watu wamekula hasara kwenye Mahindi sababu ni Serikali kuwaingilia Wakulima eti wasiuzie nje mahindi. Ah !!,Wanatuboa Kweli Kweli.
 
Ningekuwa mimi ndo nafanya maamuzi ningeweka mazingira rafiki kwa wakulima na wafanyabiashara ili kusiwepo kunyonyana. Mfano kama mkulima amewekeza nguvu zake na ardhi na mfanya biashara akaleta utaalam wake na vitendea kazi kama tractors kwanini hii joint venture isiwe isikubaliwe.

Kama kilimo kiboreka hadi kwenye kilimo cha kisasa yaani cha umwagiliaji nahisi ingekuwa bora zaid. Serikali ingezibana pande zote mbili kwa influence iliyonayo kupelekea makubaliano yenye tija hata kama makubaliano ya awali hayakuwa hivyo.

Swala la kuchagua uuze wapi au usiuze wapi ni jambo ambalo si la muhimu sana kama mkulima ananufaika na kilimo cha mkataba kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima amekifanya miaka 50 bila mafanikio ya kimaslahi. Mapinduzi ya kilimo.yananza na wakulima wenyewe.
Ni mawazo mazuri ukiwa umejikita negativity, lakini jiulize kati ya mwenye ardhi na alietia gharama kwa maana ya yule anaejiita mwekezaji ni nani ana mandate ya kupanga na kujua gharama za uendeshaji? Kiukweli kwa mfumo huu ni rahisi sana kwa mwekezaji kimpiga mkulima kwa kupandisha gharama za uendeshaji kidanganyifu hivyo mkulima huyu bandia ni rahisi kupewa mgao kiduchu bila kugomea kwani gharama hazijui.

Hivyo tunaposhauri kwenye mambo ya msingi kama haya lazima wakweli na timamu wa mawazo pasi na chembe yeyote ya ubinafsi.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa sababu kinawanyonya wakulima.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya Hunyari wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.

“Ni marufuku kwa wanunuzi wa pamba kulima pamoja na wakulima kwa sababu wakulima wanakosa uamuzi wa kupanga bei. Kuanzia sasa zao hilo litauzwa kwa njia ya mnada.”amesema Majaliwa

Amesema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeamua kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba, pembejeo hadi masoko.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo katika wilaya hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu itakayowawezesha kulima kwa kufuata njia bora za kisasa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo lao

Je Serekali imeshafanya utafiti wa kutosha..ni jinsi gani wakulima walikuwa wananufaika na kilimo cha mkataba?

1. Wenye makampuni walikuwa wanawapa wakulima kuanzia
a) Mbegu
b) Madawa
c) Pembejeo nyingine

Na bado wakulima walikuwa wanawapiga wenye makampuni kwa kutokulipa madeni haya...na walikuwa wanauzia pamba makampuni mengine tofauti na yule aliye mfadhili mbegu na madawa. Kuna madeni kibao mpaka sasa wenye makampuni hawajalipwa kwa miaka.
Hapa itakula kwa wakulima..kwa maana unafika msimu wa kilimo mkulima hana hata pesa ya kununua mbegu na pembejeo nyingine

Swali je ni serekali sasa itatoa ruzuku kwa wakulima kwa kazi ambayo ilikuwa inafanywa na makampuni binafsi? Kama serekali haitafanya haya hakuna la maana litakalo fanyika zaidi sana wenye makampuni watakuwa wamepunguziwa mzigo wa madeni ambayo kila baada ya msimu wa pamba kwisha ilikuwa ni lazima yawepo na mengine hayajalipika kwa miaka sasa
 
Back
Top Bottom