Waziri Maige apambana na Barrick; ameitaka serikali kuipokonya kampuni ya Barrick leseni ya madini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Maige apambana na Barrick; ameitaka serikali kuipokonya kampuni ya Barrick leseni ya madini.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Katika hali ya kutatanisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ameitaka serikali kuipokonya kampuni ya Barrick leseni ya madini kwenye wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, na badala yake kipewe kikundi kimoja kilichoko kwenye jimbo lake la Msalala.

  Kampuni ya Mkumi Exploration iliyosaini mkataba na Barrick ni mmiliki halali wa leseni ya kutafuta madini (prospecting licence) kwenye eneo la Jomu, Mwazimba, wilayani Kahama iliyokabidhiwa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kushinda tenda mwaka 2011.

  Barrick, ambayo imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 kwenye migodi mbali mbali nchini, inalalamika kuwa eneo lake hilo limevamiwa na kikundi cha Kasi Mpya Gold Mining Corporative Society (KAGAMICO) ambacho kinaungwa mkono na Waziri Maige.

  Kikundi cha KAGAMICO kimekuwa kikichimba dhahabu kwenye eneo hilo tangu mwaka 2009 kinyume na sheria licha ya kuwa Barrick ndiyo mmiliki halali wa leseni ya eneo hilo.

  "Mimi nitafanya kazi yangu ya kuwatetea na mimi niseme niko tayari kulipa gharama yoyote itakayoendana na kusema ukweli kwenye jambo hili," Maige aliwaambia wanachama wa kikundi cha KAGAMICO katika mkutano nao hivi karibuni wilayani Kahama.

  Katika mkutano huo, Maige alitoa shutuma kwa Barrick waziwazi kutokana na mgogoro huo wa uchimbaji wa madini, huku akiishutumu kampuni hiyo kuwa haiitakii mema serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

  "Kwa haya yanayotokea sasa, mimi nasema Barrick haiipendi CCM ... wana zaidi ya leseni 200 maeneo mbalimbali. Nilikuwa kwenye kamati ya Bomani ya kupitia maeneo hayo. Hakuna kampuni ambayo ina leseni nyingi kama kampuni hii," alisema Maige huku akiitaka Barrick iachie eneo la Mwazimba kwa wachimbaji wadogo.

  "Mkiwafananisha hawa (KAGAMICO) na wale (Barrick) hawawezi, kwa hiyo watazameni (KAGAMICO) ni wenzenu wanaganga njaa," alisema waziri huyo.

  Maige alisema Barrick tayari wanachimba dhahabu ya kutosha Bulyanhulu na kuwataka waliachie eneo la Mwazimba kwa wachimbaji wadogo.

  Maige alimwandikia barua Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja Februari 8 mwaka huu kumtaka waziri huyo mwenzake kusitisha mpango wa kuwahamisha wachimbaji wadogo kwenye eneo hilo la Barrick.

  "Endapo kwa vyovyote vile itashindikana kupatiwa eneo hilo la Mwazimba, basi watengewe eneo lao na wapatiwe kabla ya kuondolewa mahali walipo sasa," anasema Maige kwenye barua hiyo yenye kumbukumbu DMNRT/288/401/01/58.

  Maige kupitia barua hiyo ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, alimtaka Ngeleja kuhakikisha katika kipindi cha mpito wakati serikali inashughulikia mgogoro kwenye eneo hilo, iwaachie wachimbaji wadogo waendelee na shuhuli zao kwenye eneo hilo la Barrick.

  Akitekeleza maombi ya Maige, Ngeleja alimwamuru Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja Bahati Matala, kusimamisha zoezi la kuwahamisha wachimbaji wadogo kwenye eneo linalomilikiwa kisheria na kampuni ya Barrick.

  "Ili kutoa nafasi ya kulishughulikia suala hili kikamilifu, nakuagiza usitishe zoezi la kuwaondoa wachimbaji wadogo katika eneo husika hadi hapo tutakapokamilisha uchunguzi wa malalamiko yaliyoletwa kwetu," alisema Ngeleja kwenye barua yake kwa DC wa Kahama.

  Katika barua hiyo ya Februari 17 mwaka huu, yenye kumbukumbu namba DA.170/264/01 ambayo nakala tunayo, Ngeleja alipeleka nakala kwa Waziri Mkuu, Maige na kikundi cha KAGAMICO. Meneja Uhusiano wa Barrick, Teweli Teweli, akizungumzia sakata hilo jana alisema Barrick imesikitishwa na kitendo cha serikali kushindwa kuwazuia wachimbaji wadogo kuvamia eneo lake wakati kampuni hiyo ikiwa ni mmiliki halali wa leseni.

  "Ni jambo ambalo linakatisha tamaa sana. Tumefuata taratibu zote za kisheria lakini bado haki zetu kama wamiliki halali wa leseni iliyotolewa na Kamishna wa Madini kwenye eneo la Jomu inaporwa," alisema Teweli.
   
 2. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Anaitaka Serikali???

  Kwani yeye ni nani???
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Anatudanganya tu, hamna kitu hapo.:panda:
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Naona ni uhasama kati yao Ngeleja - Sengerema na Maige - Msalala * Nani ni Bora???
   
 5. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Wabongo hata mkilambwa makalio hamtaridhika, mkitetewa issue wakikaa kimya issue.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Matusi yamekujaje tena?
  Hebu kuwa mstaarabu bana.
   
 7. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  @Ndibalema...Wewe Ujumbe wako hapo chini Huuoni au unaona ya wenzio tu..makalio hata wewe umeandika.......

  Maige anajindanganya na kudanyaga hao wachimbaji wasio halali..barrick wanamiliki PL toka 2007.....sasa 2009 wapi na wapi afanye home work kwanza.
   
Loading...