Waziri Maiga,Umejipangaje safari yako UN?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Boss wako Raisi Magufuli ni mtu Wa misimamo chanya na hivi anapenda pia kuhamasika anapokutana na watu wenye fikra na misimamo chanya.Ukitaka kufahamu namuongelea mtu Wa namna gani rejea siku Boss wa kampuni ya Barrick Gold Mines, BGM alipokuja nchini kuonana na naye kufanya mazungumzo baada ya makanikia yao kupigwa "pin".


Raisi Magufuli alimsifu sana yule wajina wake kwa kusema ni "mwanaume" kweli. Sifa ile haikuwa ya "uanaume" Wa kawaida tuujuao na hakumaanishi chochote zaidi ya kwamba BGM ni watu kweli wanaoweza kukabiliana hata na hali ngumu katika maisha.Kwamba ni watu wanaoweza kuona fursa katika changamoto.Kwamba BGM ni watu wanaoweza kuona wema katika ubaya.Na kwamba ni watu walio tayari kugeuza matatizo na vikwazo kuwa daraja la kuvukia kusonga hatua nyingine kibiashara.


Na kwa kweli Magufuli hakuwa amekurupuka kuwaita BGM kuwa ni "wanaume" maana hadi leo wako hapa wanakomaa na mazungumzo licha ya kwamba ushahidi hauwapi fursa ya "kutoboa".

Dunia haijawahi kuwa rafiki kwa watu legelege.Dunia siku zote ni rafiki kwa wale wanaotia juhudi.Dunia inawa-favour wale wanaoweza kugangamala nayo hata pale inapowaburuza. Mifano iko mingi. Yesu mwenyewe "alikomaa" na msalaba na ndiyo maana leo watu tuna matumaini kwamba Mbingu tutaiona maana baada ya mateso yale alirejea Mbinguni na kufungua geti la Uzima wa Milele na kilichobaki kwetu ni suala la kila mmoja kufika tu pale getini na kugusisha " Smart ID" yako( ili 'system iweke record ya particulars za mtu aliyeingia' na kisha kuingia ndani.Geti liko wazi miaka 2000 iliyopita.


Kwa mkitadha Wa mada, hii naomba nitoe mfano mwingine.Nchi ya Korea Kaskazini. Kwa wale wanaongalia mambo kwa kushirikisha na jicho la tatu wataungana nami kwamba NK imetoka mbali kufika hapo ilipo Leo. Imesota sana. Watu wake hawakuogopa changamoto wala vikwazo.Maendeleo ya Kitekinolojia,mintarafu katika dhana za kijeshi na Kiusalama hayatokana na sala za Albadiri au maombi ya watu wake kulia kulia kwa kugalagala.Ni matokeo ya watu Wa NK kuelewa kuwa dunia haidandiwi kwa mbele inapojizungusha. Ni matokeo ya kuelewa kwamba matatizo,changamoto na vikwazo ndio mtaji Wa kwanza kabisa katika binadamu kuiboresha dunia iwe pahali pa kupendeza.


Waziri Mahiga, kwa nafasi yako ya Uwaziri Wa mambo ya kigeni na taaluma yako ya " udukuzi" unafahamu mambo mengi sana juu ya uwezo Wa NK kuliko mimi.Leo katika kuthibitisha kuwa wao nao kwa sasa ni "wanaume" nimesikia kupitia vyombo vya habari kuwa NK wamesisitiza na kukumbusha mission yao kuwa wanataka kuwa sawa na Marekani kiulinzi na kitekinolojia. Wanataka kuwa na Nuke.Raisi wao Kim amesisitiza hataki kusikia jambo jingine zaidi ya kuwa nchi yake inakuwa na nguvu sawa na Marekani.Hiyo ndio ndoto yao. Na kweli wanasonga sana mbele kuelekea ndoto hiyo.Sio tena ndoto ya mchana bali ni vitu vinaonekana sasa.


Katika kufikia hapo, NK ilichagua kufanya biashara na nchi nyingine na hivi kuachana na Marekani na washirika wake wengine ambao wote walionekana kuwa na wivu wa kijinga dhidi ya NK. Ndio wivu wa kijinga tu. Wanadamu wote tumeamuriwa kuitiisha dunia tena kila mtu kwa nafasi,rasilimali na uwezo Wa kiakili aliojaliwa nao na Mungu.


NK katika kufanya biashara na wale iliowaona ni wanaendana inasemekana na sisi Tanzania tumo.Na kweli Kama tumefanya nao biashara mimi naomba tuwe "wanaume" tu. Tuiambie dunia kuwa tumefanya nao NK biashara. Tusimung'unye maneno hata kidogo.Tuiambie UN kuwa tumewapa NK walichohitaji na ambacho tulikuwa nacho na wao wakatupatia kile tulichokihitaji na ambacho walikuwa nacho.


Tuiambie dunia kuwa sisi hatujauziana mirungi,bangi au aina nyingineyo ya madawa ya kulevya na Wakorea hao. Tuiambie dunia kuwa tumefanya biashara ya kununua tekinolojia kwa ajili ya ustawi na usalama wa Watanzania. Tekinolojia kwa ajili ya usalama Wa watanzania inatoka kwa vyovyote kwa Mungu. Kuwa na Tekinolijia ya makombora hakujawahi kuwa dhambi na haitakaa iwe dhambi.Kinyume chake ni kutumia tekinolojia kuangamiza watu wasio na hatia na wasio kuwa tishio kwa usalama na ustawi wa dunia.


Dhambi ya tekinolojia ya makombora iko katika kuwa nayo na kisha ukaitumia kutisha tisha wenzio bila sababu zozote zisizoacha shaka yoyote. Na huo ndio uenda wazimu. Panga kila mtu anajua ni silaha.Kuna dhambi gani mimi kununua panga toka kwa mtu anayeyatengeneza (hata kama ana historia ya yeye kutumia baadhi ya mapanga yake kufyekea watu) kwa ajili ya kwenda kufyeka shamba langu ili nilime?


Waziri Mahiga,Tanzania inahitaji kuwa "mwanaume". Sisi hatutakuwa Wa kwanza kuwa hivyo. Ukiachana na NK ziko nchi nyingine kama Iran.,Cuba na nyingine nyingi.Msimamo chanya hulipa mara zote na haujawahi kumuangusha yoyote. Unapoenda UN wala usibabaike na kutafuta maneno ya kujikosha.Kama tumefanya biashara na NK tuiambie dunia kuwa hatukuwa na chaguo jingine isipokuwa kuhakikisha watanzania wanaishi bila hofu ya kuvamiwa na yeyote na wakati wowote.


Waziri Mahiga, unapoenda UN umejipangaje labda? Umejiandaa kwenda kufafanua hicho ulichokisema kuwa kwa sasa mumepunguza mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia baina ya nchi yetu na NK? Ukajijitee kihivyo,kweli? Kama ambavyo sisi tulipoamua kuwabana ACACIA tulifanya hivyo tukiwa na ushahidi kumbakumba ndivyo na hao waliotutaja kuwa tumefanya biashara na NK walivyo na ushahidi wote bila shaka. Kukana kuwa hatujafanya biashara abadani sio utetezi okozi ikiwa wanao ushahidi.Njia pekee ni kueleza bayana kwa nini tulifanya nao biashara kama tumefanya hivyo kweli.Kwa nini tujikunyate kwa tendo jema?


Tuiambie dunia kuwa hatukufanya dhambi yoyote kwa kushirikiana na wanaonekana kuwa "waovu". Dunia ni ya wema na waovu. Tuiambie dunia Tanzania kama ina-deal na NK haifanyi hivyo kuambukizwa ubaya wao bali uwezo na nguvu za kitekinolojia waliojaliwa na Muumba.


Basi nahitimisha kuwa uendapo huko UN uende "kiume" na uwaambie kiume vinginevyo tutaendelea kuwa watu ronyoronyo tu duniani na Wa kujenga uchumi wa watu wetu unaishia kumudu kununua Chips na Bavaria toka Vi-supermarkets uchwara. Natukia safari njema.
 
Back
Top Bottom