Waziri Magufuli, sheria sio kama "menu" katika migahawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Magufuli, sheria sio kama "menu" katika migahawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Mar 2, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  TOKEA MBUNGE WETU MHE JOHN MNYIKA AANZE KUTUTETEA WANANCHI WAKE WANAONYANYASWA NA MAMALAKA ZA BARABARA, WATUMIAJI WENGI WA BARABARA HIYO YA KLA SIKU WAMEKUWA NA MAONI TOFAUTI KUHUSU UAMUZI WAKE HUO. HII NI KUTOKANA NA KUFANIKIWA KWA PROPAGANDA ZA MHE JOHN MAGUFULI KUWAFANYA WATU WENGI KUAMINI KUWA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA BARABARA YA MOROGORO KATI YA UBUNGO HADI KIBAHA NI MATOKEO YA WATU KUJENGA KATIKA HIFADHI ZA BARABARA, JAMBO AMBALO SIO KWELI HATA KIDOGO.

  WENGI WALIOJENGA KATIKA HUFADHI ZA BARABARA WAMEJENGA MAJENGO YA BIASHARA YA MUDA KWA KIBALI CHA TANROAD KUWA ENDAPO HIFADHI ITAHITAJIKA MAJENGO YAO YATABOMOLEWA BILA FIDIA YOYOTE.

  LAKINI MHE JOHN MAGUFULI ANATUMIA KIGEZO HICHO HICHO KUVAMIA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI WALIYOYAPATA KIHALALI NA KUDAI NI HIFADHI YA BARABARA ENDELEA ................


  BOMOA BOMOA UBUNGO HADI KIRUVIA

  Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

  Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

  Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

  Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

  Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

  Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.

  IMETOLEWA NA WANAHARAKATI WANAOPINGA WANANCHI KUNYANYASWA NA WIZARA YA MIUNDO MBINU NA TANROAD
   
Loading...