Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
Mawaziri wa wizara mbalimbali serikalini, wametakiwa kuiga mfano wa Waziri wa Ujenzi,Dk John Magufuli wa kugawa rasilimali za nchi kwa watu wote.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2013/14.
Filikunjombe ambaye siku zote amekuwa na kigugumizi cha kukubali bajeti kwa urahisi,juzi alikubali kuunga mkono moja kwa moja Makadirio ya Wizara ya Ujenzi akisema kuwa mgawanyo wake umelenga maslahi ya nchi na maslahi ya watu wachache kama ilivyo kwa wizara zingine.
Kutokana na hili, mimi na wananchi wangu wa Ludewa tunakuombea sana ndugu Magufuli na tunasema kuwa ikiwa utakuwa na uhitaji wa nafasi nyingine ya juu zaidi ya hii uliyonayo, usisite kutuambia nasi tutakuunga mkono kwani tuko pamoja na wewe,alisema Filikunjombe.
Mbunge huyo aliwataka mawaziri wajaribu kuiga mfano wa Magufuli ambaye anapeleka miradi kwa nchi nzima na hafanyi kazi ya kurundika miradi katika jimbo lake pekee.
Hata hivyo alimtaka Magufuli kufanya haraka katika kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara katika Wilaya ya Ludewa ambayo haijawahi kupata lami tangu Uhuru hivyo ikijengwa lami wananchi wa huko nao utakuwa mwaka wao wa kwanza kusherehekea uhuru licha ya kuwa Watanzania wengine watakuwa wanasherehekea zaidi ya miaka 53 ya Uhuru.
Kwa hisani ya Mwananchi.