Waziri Magufuli ageuka mbogo asusa kupokea barabara ya Kilwa

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, amegeuka mbogo kwa wakandarasi wanaojenga barabara ya Kilwa, huku akisusa kupokea barabara hiyo kutokana na kuwa chini ya kiwango iliyojengwa kwa msaada wa serikali ya Japan.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 10 kuanzia Bendera tatu hadi Zakhiem ilijengwa na Kampuni ya Kajima kutoka Japan, Dk Magufuli alisema kukutokana na kuwa chini ya kiwango, serikali haiwezi kuipokea hata kama ni msaada.

Pia, Dk Magufuli alitoa siku kumi kwa Kampuni ya Chico kutoka China, kuanza kazi ya ujenzi wa kilomita 1.5, kutoka Zakhim hadi Tanita, vinginevyo serikali itafuta zabuni hiyo na kampuni italipa fidia na kufungiwa kufanya kazi nchini.Waziri Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza jana kwenye barabara ya barabara Kilwa, Mandela na Ndundu-Somanga.

“Haiwezekani kupokea kitu kisicho na ubora eti kwa sababu ni msaada, hiyo haiwezekani. Tutaandikia barua Serikali ya Japan kueleza fedha za walipakodi wao zimefanyiwa usanii na mhandisi na mshauri wa Japan tofauti na lengo lililokusudiwa,” alisema Dk Magufuli.

Kuhusu Kampuni ya Chico, Dk Magufuli alisema kinachoonekana ni wizi kutokana na kusaini mkataba tangu mwaka jana na kwamba, tayari imelipa Sh1.27 bilioni kama malipo ya awali.“Huu ni wizi amesaini mkataba tangu Novemba mwaka jana na amelipwa Sh1.27 bilioni za awali, lakini hadi dakika hii hakuna hata kifaa kimoja cha kufanya kazi kilichopo eneo la kazi,” alisema dk Magufuli akionekana kuchukia.

Kwa upande wa barabara ya Ndundu- Somanga, Waziri Magufuli alitoa miezi mitano kwa Kampuni ya Kharafi ya Kuwait, inayojenga barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 60 kukamilisha kazi hiyo, vinginevyo atanyang’anywa kazi hiyo.

Dk Magufuli alisema ucheleweshaji miradi hiyo inasababishwa na Makao Makuu ya Wakala wa barabara nchini (Tanroads), kutaka kusimamia miradi yote nchini.Alimwagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, kuwashirikisha wakandarasi wa mikoa na wilaya kwenye kazi zinazofanyika maeneo yao, ili wakishindwa kuwajibika wafukuzwe kazi sambamba na kufikishwa mahakamani kwa uzembe.

Pia, Dk Magufuli alitoa wiki tatu kwa Kampuni ya Maltauro kutoka Italia, inayojenga barabara ya Mandela, kukamilisha ujenzi huo na kuagiza Tanroads kuhakiki tena ubora wake.
 
Hivi anadhani tatizo ni hao wakandarasi? tatizo lipo tanroads ana ofisini wkake
 
Ndio tunataka viongozi wa aina hii wanafahamu uzembe wa kiutendaji ambao mwisho wa siku inaleta kero na mihangaiko isiyo kuwa ya lazima kwa Wananchi. Kama makubaliano yamefanyika kwanini utekelezaji usiendane na makubaliano? Hata kama kuna ugumu katika kazi Wananchi tuna macho tutaona kuliko kupuuza tu na watendaji wanajifanyia wanavyotaka na kuishia kushinda kwenye mabaa kisa Mkandarasi.

Tena Magufuri kuna tatizo jingine kwa hao wakandarasi hasa wa kichina, wanachimbuachimbua barabara alafu kutwa nzima unawakuta na vijikoti vyao na vijifimbo eti wanapima mwaka nenda rudi huoni mabadiriko, kibaya zaidi maeneo yenye michepuko(diversions) hawaweki alama zozote kitu ambacho kimekua kikisababisha ajari na usumbufu mkubwa kwa watumiaji. Angalia barabara ya Magole-Tuliani(Morogoro) na hata hiyo ya somanga(Mtwara-Lindi)

Nawakilisha zimfikie Magufuri. Diversions jamani muhimu mtatua Wananchi tafadhari ndugu Wakandarasi wa Kichina, acheni ubabe ndani ya Nchi yetu.
 
bold move mh waziri. nadhani tunahitaji kusukumana like this. vinginevyo tunaodharauliwa ni watz wote. bora tuwe tunapata vitu kama hivi. asante mh waziri
 
Kweli kabisa hawa makandarasi wanatuzingua, barabara ikikamilika baada ya muda inaharibika!
 
Magufuli ni crusader wa popularity kwani anajua kinachoendelea serikalini lakini anajitokeza kwenye vyombo vya habari ili aonakane anafanyakazi. Ukweli ni kwamba sekta zote nchini hazipati hela zilizopangwa kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida, Kama serikali inakopa fedha za mishahara ya wafanyakazi wake unafikiri serikali hiyohiyo inaweza kutoa fedha kwa miradi ya mabarabara kwa wakati? Kwenye hili Magufuli hajawatendea haki wakandarasi ma Tanroads
 
Safi sana mheshimiwa waziri,hata kama ni msaada hatutaki vitu below standard.jamani there are some leaders worth supporting.big up magufuli
 
kumi kama Magufuri basi tanzania tutapimana na south africa kimaendeleo..
 
well done magufuli wapiga kura wa jimboni kwako hawajutii kuvote jinalo!!! viongozi ccm igeni mfano huo
 
tunataka vitendo na sio kauli tu za majukwaani
barabara ya kwenda Lindi_Mtwara kuna kipande cha 64 km hakijakamilika kwa miaka miaka minne? na mkandarasi keshalipwa over 60%
Mandela Rd ndo balaa,barabara inatengenezwa kwa mafungu na siku hizi nadhani wameacha kabisa hivyo kuongeza kero ya TRAFFIC JAM
au ndio zile za mgao zinarudi mifukoni halafu contractor anashindwa kuhimili kazi??
 
.................

Dk Magufuli alisema ucheleweshaji miradi hiyo inasababishwa na Makao Makuu ya Wakala wa barabara nchini (Tanroads), kutaka kusimamia miradi yote nchini.Alimwagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, kuwashirikisha wakandarasi wa mikoa na wilaya kwenye kazi zinazofanyika maeneo yao, ili wakishindwa kuwajibika wafukuzwe kazi sambamba na kufikishwa mahakamani kwa uzembe.

Hapa magufuli ni kama anapengekeza tarnropads watumie some sort of sera ya majimbo kwenye operation zao
 
Hivi katika hii serikali inayoongozwa na vasco da gama wa tanzania mchapa kazi wa aina wa magufuli yupo mmoja tu?
Yaani tungekuwa nao watatu na sisi watanzania angalau tungekuwa na kitu cha, kujivunia. Maana huyu jamaa walimpiga stop na vijembe juu, baada ya muda barabara ya kigogo/mburahati kukawa na mgomo wa daladala wakilalamika barabara mbovu, serikali kwa aibu imekaa kimya na kuua issue kimya kimya kwa kuogopa aibu. Kwani wangetekeleza madai ya wagomaji ingeonekana kituko kwa sababu mwisho wa siku mheshimiwa magufuli angeibuka kidedea, sasa hapo nani mwenye maamuzi katika mambo ya msingi! It's a shame guy of magufuli type to be disappointed in execution of his duties, because of fear of being overshadow by his achievement, this is what mr. Vasco da gama of tanzania is avoiding.
 
Magufuli ni crusader wa popularity kwani anajua kinachoendelea serikalini lakini anajitokeza kwenye vyombo vya habari ili aonakane anafanyakazi. Ukweli ni kwamba sekta zote nchini hazipati hela zilizopangwa kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida, Kama serikali inakopa fedha za mishahara ya wafanyakazi wake unafikiri serikali hiyohiyo inaweza kutoa fedha kwa miradi ya mabarabara kwa wakati? Kwenye hili Magufuli hajawatendea haki wakandarasi ma Tanroads

Lakini hawa Chicco tayari wamelipwa 1.27bil TZS!
 
Jamani hicho kipande cha SOmanga kinachosha...we acha tu,km 60 tu lakini gari itatumia masaa 3,sasa kukiwa na mvua ni siku 3.
 
nyimbo ni zile zile tutazisikiliza sana tu
Magufuli aagiza daraja la Kigamboni lijengwe haraka
25 Machi 2011
SERIKALI imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lianze kujenga Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani zao.

Daraja hilo linatarajiwa kutumia zaidi ya Sh bilioni 130 hadi litakapokamilika, NSSF itatoa Sh bilioni 100 na Serikali Sh bilioni 30.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, ametoa agizo hilo leo Dar es Salaam baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni, Dar es Salaam ambako daraja hilo linatarajiwa kujengwa.

"Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni, ifike wakati tuanze, kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo," alisema Magufuli.

Amesema, katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwamo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi, ili kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne kumaliza muda wake ambazo ni sawa na Sh bilioni 100 ambazo zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi ikitafuta zaidi ya Sh bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi

"NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja ... ili likikamilika, litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji, kwani feri zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara," amesisitiza Dk. Magufuli.

Amesema, kimsingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo, hakuwezi kuwafanya wasianze mradi, kwa kuwa katika mradi wowote, mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezwa kulingana na anavyoondelea na mradi.

Dk. Magufuli amesema, ujenzi huo ni muhimu kwa kuwa eneo hilo lina wananchi wengi wanaofanya kazi katikati ya Jiji, hali kadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ukiwamo ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo Mtwara na Lindi na kuwapo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crescentius Magori, alisema, shirika hilo hadi sasa ina Sh bilioni 100 kati ya Sh bilioni 130 zinazohitajika, kukamilisha ujenzi huo haraka.

Alisema, daraja hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili za watembea kwa miguu.

Magori alimhakikishia Magufuli, kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo linalotarajia kuchukua miaka mitatu kukamilika
 
Back
Top Bottom