Waziri maghembe,umeligundua hili sasa tufanye kazi ili kuliondoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri maghembe,umeligundua hili sasa tufanye kazi ili kuliondoa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Vitendo, Dec 11, 2009.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Akitangaza matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2009,waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Prof.J Maghembe alisema
  Katika hali nyingine, Profesa Magembe alisema kwamba tatizo sugu la wanafunzi nchini kufanya vibaya katika masomo ya Kiingereza na hisabati, limeendelea kujirudia.

  Katika somo la Kiingereza walifaulu kwa asilimia 35.4 na hisabati asilimia 21 hali ambayo Profesa Magembe alisema imepanda kidogo ikilinganishwa na mwaka jana
  Pamoja na hali hiyo, Profesa Magembe alisema tatizo sugu la wanafunzi wa shule za msingi kutofaulu masomo hayo linatokana na msingi mbovu walio nao walimu wanaofundisha masomo hayo.
  wewe kama waziri mwenye dhamana husika bila shaka wizara yako inatakiwa kuandaa walimu wazuri wa kufundisha masomo husika na si wewe kushangaa mbele ya vyombo vya habari kuhusu kufeli kwa wanafunzi hao.
  Tatizo umelijua wewe kama waziri ,je wizara yako inajipanga vp kuliondoa Tatizo hilo?
  watanzania wanasubiri 2010 kuona takwimu zimebadilika na si kama za mwaka huu.
   
Loading...