Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akiwatuhumu baadhi ya wadau wa sekta ya utalii kwamba wamejipanga kuhakikisha wanamng’oa katika wadhifa wake kupitia sakata la Faru John, wadau wamemtaka asiwe mfamaji.
Akizungumza na JAMHURI hivi karibuni, Prof. Maghembe amesema baada ya Serikali kuongeza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye huduma za utalii kama sehemu ya mkakati wa Serikali kuongeza mapato, wadau wamekereka na sasa wanatafuta ‘kichwa chake.’
“Kuna watu wamewapa waandishi wa habari fedha ili wanichafue mimi Prof. Jumanne Abdallah Maghembe niondolewe kwenye nafasi yangu… wanasema nimefanya maisha yao yawe magumu. Wanapambana kufa na kupona… Watanzania wana uwezo mkubwa wa kupaka matope,” amesema Prof. Maghembe.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii (TATO), Wilbard Chambulo, ambaye ni mmoja wa wadau waliotuhumiwa kutumia sakata za kifo cha Faru John kufukiza upupu Prof. Maghembe aondolewe wizarani, kwa upande wake amesema chama chake hakina ugomvi na Waziri Maghembe.
“Suala la TATO na kupotea kwa Faru John, vina uhusiano gani? Yeye ashughulikie masuala yake na watu wake wa Bonde la Ngorongoro… sisi hatuna tatizo na Prof. Maghembe. Sisi ni nani kushabikia kumtoa Prof. Maghembe ambaye ni mteule wa Rais John Magufuli?
“Sisi siyo mamlaka ya uteuzi wake, lakini pia suala la utendaji wake liko mikononi mwa waliomteua. Kitendo cha kusema kwamba sisi hatumtaki siyo sahihi. Sisi hatuchagui waziri, lakini tunataka kujua majukumu yake kwetu sisi wadau wa utalii ni yapi?” amesema Chambulo.
Kuhusu Faru John, Chambulo anasema kukosekana kwa uwazi ndiyo kunakoendelea kuwatesa wahusika. Amesema kama wangetangaza waziwazi tangu mwanzo kuwa Faru John angehamishwa na alipofariki wakawatangazia Watanzania kuwa amekufa, jambo hilo lisingevuta hisia za watu wengi.
Mwenyekiti huyo amemshauri Prof. Maghembe akutane na wadau wa sekta ya utalii na kujadili changamoto za utalii, huku akisema amekuwa akikaa mbali na wadau hao na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ndiye anayewasikiliza na kuahidi kushughulikia matatizo yao.
“Unapokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, unatakiwa kuangalia maslahi ya Serikali pamoja na sekta binafsi… lakini sasa waziri amekuwa anaangalia zaidi maslahi ya Serikali na kusahau ya sekta binafsi ambao ndiyo wadau katika sekta ya utalii,” amesema Chambulo.
Kuhusu suala la VAT kwenye sekta ya utalii, Chambulo anasema wadau wa utalii hawawezi kupinga mipango ya Serikali, huku akisisitiza kwamba wamekuwa wakilipa kodi zote kama ilivyoelekezwa na Serikali.
Mweyeiti huyo amekwenda mbali zaidi na kusema kwamba sekta ya utalii imekuwa kama yatima, huku wakikosa msaada kutoka kwa waziri mwenye dhamana, mpaka pale Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ameahidi kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kusikiliza kilio chao.
Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Utalii Tanzania, Richard Rugimbana, amesema: “Naomba nisiseme chochote kuhusu suala la hilo la Prof. Maghembe…”
Mtendaji Mkuu wa TATO, Sirili Akko, ameiambia JAMHURI kwamba hoja ya kwamba wamepanga kumtosa kwa sababu ya hoja ya VAT, haina mashiko. Amesema Prof. Maghembe azungumze kuhusu jambo ambalo limewafanya wadau kuwa na uchungu naye.
Akko amesema ni ukweli kwamba suala la kuanzishwa kwa VAT limesababisha matatizo makubwa kwenye sekta ya utalii na suala la Faru John si jambo ambalo linahitaji msukomo wa wadau wa sekta binafsi.
“Sijawahi kumsikia Faru John mpaka juzi baada ya Waziri Mkuu alipoanza kumdai faru huyo… hatuhitaji kuingia kwenye mgogoro na Waziri Maghembe. Sisi tunawaambia watu wetu wafuate sheria,” amesema Akko.
Amesema kuna mambo mawili makubwa aliyofanya Prof. Maghembe, ikiwamo kurejesha misitu ya Tanzania, hivyo kutokana na hilo wanamheshimu. Kuhusu hoja ya VAT, amesema haina mashiko kutokana na ukweli kwamba anayelipa kodi hiyo ni mtalii mwenyewe na si wadau wa utalii.
Wiki iliyopita JAMHURI iliandika kuhusu Faru John, na kufanya mahojiano na Waziri Maghembe, ambaye bila kumung’unya maneno, aliwataja baadhi ya wadau wa sekta ya utalii kuwa wanataka kumwangusha kwa kile alichosema kwamba ni kudhani kwamba yeye binafsi ndiye aliyeshauri suala la VAT.
Akko amesema kutokana na hilo, pengine waziri amegundua kwamba kuna makosa yalifanyika na kwamba imeleta matokeo tofauti na matarajio ya Serikali. Ameongeza kwamba kumekuwapo na kufutwa kwa safari za watalii tangu kuanza kwa matumizi ya VAT.
Bajeti ya mwaka 2016/17 imepitisha tozo ya VAT kwa asilimia 18 kwenye huduma za utalii, hususan katika shughuli za kuongoza watalii, kusafirisha watalii, utalii wa majini, kuangalia wanyama na ndege wa porini, kupiga picha na kutembelea hifadhi.
Baada ya Bunge kupitisha sheria hiyo mpya kuanzia Julai mosi mwaka huu (2016), Serikali imeanza kutoza kodi ya VAT kwenye shughuli za utalii.
Katika hotuba ya bajeti ya mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema miongoni mwa sababu za kuongeza VAT kwenye shughuli za utalii ni kuwa Afrika Kusini wanatoza kodi hiyo na watalii wanaendelea kuingia nchini humo.
Waziri Maghembe amekuwa katika msukosuko baada ya taarifa kuanza kuvuja na kuonesha kuwa aliwasilisha pembe za faru ‘feki’ kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Taarifa za uhalisia wa pembe alizowasilisha zinaacha maswali mengi baada ya JAMHURI kuhojiana na watu zaidi ya 50 wakiwamo wahifadhi.
Baadhi ya waongoza watalii wanasema Faru John ‘wamemnywa’ kwa maana kuwa wamemuua kwa makusudi na kuuza pembe zake, lakini hali ilivyobadilika kutokana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza uchunguzi wa kina, sasa wanahaha kuhalalisha taarifa za uongo walizompa.
“Faru John wamemnywa. Yeye alikuwa na pembe zilizochongoka kiajabu. Pembe zake zilikuwa na ukubwa usiotofautiana. Hizi pembe butu walizomkabidhi Waziri Mkuu ni za Faru Hadija. Hata uzito wa kilo mbili walizosema siyo kweli,” anasema mmoja wa waongoza watalii.
Wakati mtoa taarifa huyo akisema hivyo, wahifadhi katika eneo la Ngorongoro na Grumeti wanasema hajawahi kuwapo faru mwenye jina la Hadija na Prof. Maghembe anasema pembe za Faru John ziliishakatwa kuondoa ncha.
“Pembe za Faru John zilikuwa na uzito wa kilo saba. Waziri Mkuu amepewa zenye uzito wa kilo mbili. Hii ni aibu. Wabanwe na waziri awajibishwe kwa kushiriki uongo huu. Hata kaburi la Faru John halipo, na hapa Grumeti hakuna mbwa mwitu na fisi wa kula mzoga wa faru kama John na kuumaliza. Waseme pembe halisi zimekwenda wapi!” amesema mmoja wa walinzi.
Waziri Maghembe na timu yake wamewasilisha pembe mbili kwa Waziri Mkuu Majaliwa wakidai ndizo za Faru John, lakini baada ya kuwataka wawasilishe vipimo vyenye kujumuisha vinasaba, ghafla wamegeuka na kusema kuwa faru huyo hakuzikwa bali aliachwa akaliwa na wanyama.
Waziri Mkuu Majaliwa akiwa ziarani Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, Desemba 5, 2016 amewataja kwa majina baadhi ya wahifadhi na kusema waliahidiwa Sh milioni 200, na wakapewa fungu la awali la Sh milioni 100 kumhamisha Faru John na kutimiza matakwa yao ya kumuua.
Uchunguzi juu ya alipokwenda Faru John unaendelea, na hiyo ndiyo inayomfanya Waziri Maghembe kutoa kauli tata akidai kuna watu wanashinikiza uchunguzi huo kwa nia ya kumwondoa katika wadhifa anaoushikilia.