Antar bin Shaddad
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 202
- 101
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amezomewa na wananchi wa mji mdogo wa Gallapo wilayani Babati wakati wa mkutano wa hadhara baada ya waziri huyo kuktaa kuulizwa maswali na wananchi kuhusu kero ya maji na mgogoro wa muda baina yao na mamlaka ya maji ya mji huo GAWASA.Baada ya maghemmbe kuktaa kuulizwa maswali na wananchi walianza kumzomea pamoja na maafisa wa serikali alioandamana nao na mkutano ulivunjika ambapo waziri huyo aliondoka huku polisi wakiwazuia watu wasimdhuru pamoja na msafara wake.
Kwa muda mrefu mji wa Gallapo umekumbwa na uhaba wa maji kwa kile kinachoelezwa kuwa mamlaka hiyo imeshindwa kuwajibika na kutegemea chanzo kimoja cha ambacho kilianzshwa na wananchi hao miaka karibu ishirini iliyopita huku idadi ya watu ikiwa tayari imeongezeka kwa asilimia 100 katika kipindi hicho.