Waziri Magembe azomewa UDSM

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Waziri Magembe azomewa UDSM,jasho zamtoka!
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. J4 Magembe jana alijikuta akitokwa jasho mpaka za miguu kwa aibu baada ya kozomewa na Madenti wenye hasira wa Chuo Kikuu cha Dsm (UDSM),tena mbele ya Rais wa Uganda Mh.Yoweri Museveni.

Magembe, ambaye alihudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii (UDCASS), alikumbwa na
zahma hilo mara tu alipotambulishwa na MC wa shughuli hiyo, Prof Amandina Liambama.

J4 ambaye aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alionekana kushitushwa na jambo hilo na kuanza kunong'onezana mara kwa mara na Membe.

Tofauti na alivyozomewa Magembe, wanafunzi hao ambao walikuwa wamejazana kwenye ukumbi wa mikutano wa Nkrumah, Membe na baadhi ya maprofesa walishangiliwa kwa sauti ya juu na hasa alipotambulishwa makamu mkuu wa chuo hicho, Prof Rwekaza Mkandara.

Hata hivyo, Magembe ambaye alikuwa anatakiwa amkaribishe mgeni rasmi kwa mujibu wa ratiba, alizomewa tena wakati
Mkandara alipoeleza kuwa atamkaribisha mgeni rasmi huku Magembe akiwa ameketi kiti kimoja tu toka alipokuwa
Museveni.
 
Wata zomewa wengi mwaka huu. Mh mwakani wakipanda kwenye majukwa kuomba kura wakazomewa hivi kisha tusikie wameshinda si utakua wizi wa mchana?
 
Aaah wapi,

ni kama kugombana na mpenzi wako. Kugombana sio lazima kuhitimishwe na kubwagana, kuna kupatana pia.

Utashangaa wananchi watakapotulizwa hapo mwakani, utadhani sio wao waliokuwa wakiendesha zomea zomea.
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana kila siku mimi napinga sana kuchanganya suala la SIASA na UTENDAJI hasa kwenye ngazi za juu. Inawezekana ikawa ni haki yake kuzomewa lakini akawa ameonewa kwa kutojua taratibu za uongozi hasa kwenye wizara husika. Ujumbe la kwake: Wizara ya Elimu inautofauti kidogo na Wizara ya Utalii
 
Mnasema ukweli. Tatizo watanzania wengi tume zoea kuongea tu ila vitendo kazi
 
Back
Top Bottom