jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,264
Siku moja baada ya Serikali kuwataka watumishi waliohamia Dodoma kutokea Dar kuuona mji huo kuwa ni kituo chao cha kazi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji ndugu Gerson Lwenge amesema kuwa hakuna makazi ya kutosha na wafanyakazi wengi wanaishi kwenye nyumba za wageni (Guest House).
Siku ya alhamisi Katibu mkuu Kiongozi ndugu John Kijazi alisema kuwa njozi ya Serikali kuhamia Dodoma inaelekea kutimia baada ya idara nyingi kutoka Wizara 18 kuhamia na kuanza kazi Dodoma.
Lakini akiongea mkoani hapa jana Waziri Lwenge amesema kuwa kupata nyumba(makazi) mkoani hapa ni changamoto kwa watumishi waliohamia.
Wizara anayoongoza imeshahamisha wafanyakazi waandamizi 102 katika hatua za kwanza za kuhamia Dodoma.
Alisema kwamba wizara yake ina jumla ya wafanyakazi 422 ambao wanatarajiwa kuhamia Dodoma. Kwa sasa wizara hiyo imepanga ofisi kwenye jengo la Benki wakati Serikali ikijipanga kujenga jengo kwa ajili ya wizara hiyo.
Awali Katibu mkuu alinukuliwa akisema kuwa "tutakutana na changamoto nyingi mwanzoni ila tuwe tayari kuzikabili."
The Guardian 3rd March 2017