Waziri Lukuvi tunaomba utumbue jipu la upimaji viwanja Chasimba

Melekizedeki

New Member
Sep 13, 2016
1
0
Kuna vituko vya upimaji viwanja eneo lililokuwa na mgogoro Chasimba ambapo waziri Lukuvi alifanikiwa kutatua mgogoro huo lakini Lukuvi aliagiza ufanyike upimaji, upimaji huo ulianza march 2016:.

Mpaka sasa hata robo ya kazi haijafikiwa, kwani watendaji wa wizara wanafika kazini saa saba mchana na kuondoka saa Tisa na nusu huku wakitumia muda mwingi kukaa kwenye miti.

Hata hivyo wananchi wamechanga fedha za kugharimia upimaji huo ,ambapo wizara imetoa wataalam tu gharama zote wamebeba wananchi.

Fedha hizo zimekuwa zikitafunwa na wanakamati kwa kukopeshana na kugawana inapotokea sikukuu,wananchi wamegharimia mawe cha kushangaza wataalam hao wanaweka matope mipakani.

Wataalamu wanatumia wanakamati kuchukua hela kwa wananchi ili wasipitiwe na barabara.

Na mpaka sasa zoezi limesimama.
 
Jiongezeni sasa nyie mnafikiri hizo elfu 20 mnazochangishana zitatosha kumaliza hilo zoezi? Ongeeni nao kwa HERUFI KUBWA.
 
Hapo rushwa tu
Sasa wanakuja kufanya nini,hao ndio maana wengie wanakula kichapo
Watambue tu wanatumia mafuta ya Serikali kwenda na kurudi na posho wanapewa.

Wakija watimueni kama hawafanyi kazi
 
Back
Top Bottom