Waziri Lukuvi tunajua uko hapa Arumeru!, Pls usimwangushe Rais kwani hii ni wilaya yake aliyotuahidia kuitetea kipekee

amanison

Member
Jul 31, 2015
10
3
Mh.William Lukuvi;tumefarajika kufika Tena Arumeru, ili kuja kubaini na kuondoa "kansa" inayosababisha migogoro sugu na ya muda mrefu ya ardhi ambayo inatishia usalama wa maisha na amani wilayani hapa.

Mh.Lukuvi, kwakuwa siyo Mara ya Kwanza kufika hapa,tunaamini unaijua vema migogoro hiyo na kisababishi chake, na ndo maana uliposimama tu pale madhabahuni St.Theresa,ulitamka bayana unakukuja kuondoa kadhia hiyo.!maneno hayo mazito yametufanya wana-Arumeru tupate Tena tumain jipya la kuona mwaka mpya tukiwa salama. Kwasasa Ni dhahiri mateso,hofu ya kuchomewa nyumba usiku,kutekwa ,kutishwa ,kudhulumiwa,kubambikizwa kesi nk,yamefika kwenye kiti Cha enzi Cha Mungu, na ndo maana yalimgusa mweshimiwa Raisi mwenyewe na akautangazia umma wa Watanzania na ulimwengu ya kuwa atatupigania na kututetea.hivyo kuja kwako na uloyasema madhabahuni Ni ushaidi wa mwisho wa dhiki hi.!

Mh,utakubaliana na Mimi ya kuwa migogoro mingi tulonayo Arumeru haikupaswa kuwa Ni migogoro. Bali imefanywa kuwa hivyo na baadhi ya viongozi kwa maslahi yasojulikana.mfano, Arusha coffee estate ambalo wananchi Wana nyaraka zote na unajua uovu wananchi wametendwa Hadi sasa; na wa hivi karibuni wa "machumba coffee estate"ambapo wananchi wa Kijiji Cha shangarai wanaoishi kandokando na kufanya maendelezo kandokando ya shamba hilo, walifekewa mazao yao yote ya kudumu na yasiyo ya kudumu, makazi na miti yote mikubwa kwa kisingizio Cha kuvamia shamba la mwekezaji,sababu eti mwekezaji huyo ajulikanaye kwa jina la Singa amewapa serikali eneo hilo wajenge shule!!



Wananchi wanajiuliza inawezekanaje serikali itoe mashamba hayo tangu miaka ya 90,yatangazwe kwenye gazeti la serikali, halafu Leo baadhi ya watendaji wakuu wa serikali ya wilaya na mkoa wanasimamia kwa mtutu wananchi kukatiwa mazao na makazi yao kwa kisingizio kuwa shamba Ni la mwekezaji.kama kweli Ni la mwekezaji alikuwa wapi tangu 90, wananchi wanaendeleza maeneo yalopakana na shamba hilo?Sheria inasemaje kuhusu hili?!wako waloishi na kujenga kwa zaidi ya miaka 40.hata kabla halijawa revoked.leo hii,mwaka huu serikali inasema Ni wavamizi.ni nani tuliye mvamia?!Singasinga alipata hati toka kwa Nani na lini tusijue?!
Kiukweli mambo haya yanatia simanzi na huzuni kubwa. Yanafanya mioyo ya watu kuvuja damu.huku nje wakijikunyata kwa hofu ya kutekwa,kuuwawa ukijaribu kutetea ama kuusema ukweli.ama kutetea haki hiyo.bahati mbaya wanapofanya haya wanadhani wananchi Ni wajinga wasiojua lolote.!mh!


Mh,tunaamini unajua mengi kwani mbunge na wananchi wetu wamekuona Mara nyingi.hivyo safari hii tunaamini utatutendea haki!

HAYA NI MATARAJIO YETU.!

1.Utatumia weledi wako na ujasiri wako kumalizia migogoro isiyo ya lazima kabla ya kurudi.hasa Arusha coffee na machumba!

2.Tunaamini kamwe hutokubali Tena kudanganywa!! Baadhi ya Watendaji wetu wamekudanganya wewe na viongozi wakuu wengi vya kutosha.sasa tunaomba usikubali kudanywa Tena!! Na hutamwangusha mh,Raisi!!
3.kwamba kwa taaluma yako, uaweza kuwabaini wahusika,na kuwakwepesha kuwafanya sehemu ya suluhisho kwa kigenzo Cha kuwa kiongozi wa kuchaguliwa.(wakati unajua wazi juu ya figisufigisu za uchaguzi,a hilia maovu yalojificha nyuma yake)."jiulize Mara zote. Kama kweli aliwajibika, kwanini hakuwahi kutetea haki hiyo wazi kwa nafasi yake!?!
4.ingelikuwa Jambo jema kutushirikisha sisi wananchi waathirika na wazalendo katika kupata ukweli pale penye mashaka.kwani ukitumia hao wenye dhamana unajua utakachopata.

Mh,Lukuvi, tunajua ziko changamoto nyuma ya pazia katika kufika maamuzi hayo ya kuwapa wananchi haki.lkn ukikumba maneno ya vitabu vitakatifu,...ya kwamba, ."USIMWOGOPE YEYE AUAE MWILI!!BALI MWOGOPENI YEYE AWEZAE KUUA MWILI NA ROHO..! Tunaamini kwa maneno yako altareni utachagua lililo jema! Nakuhakikishia, ukiwa upande wa haki, MUNGU MKUU ATAKUPIGANIA.wala hatakuacha.,na hata usipokuwepo jina lako litaishi Kama la Nyerere!!kwani mamlaka ulopewa yana nguvu na uwezo wa kumshinda yule mwovu anayeishi juu ya machozi ya masikini wajane na yatima!

Namalizia kwa kukuomba Tena,una nafasi ya kuushanza umma wa Watanzania ya kuwa una maamuzi magumu yatakayoinua shangwe Arumeru, na hivyo utakuwa sii tu umemtendea haki Raisi wetu, Bali Mungu mwenyewe!!
 
Back
Top Bottom