Waziri Lukuvi na Rais Magufuli ingilieni kati unyonyaji wa mradi wa nyumba za PSPF Buyuni Chanika

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
59,506
103,164
Ikumbukwe kwamba miradi ya low cost house scheme inayojengwa na hifadhi ya mifuko ya jamii lengo lake kuu ni kuwasaidia wanyonge, lakini ninachokiona mimi kwenye mradi wa nyumba hizi za PSPF buyuni chanika lengo lake ni kuwatia umaskini hao wanyonge.

Haiwezekani mnyonge huyu umuuzie kanyumba kadogo kwa millioni 75 mpaka 90 kwa riba ya 11% kwa mwaka na rejesho la laki + kila mwezi halafu bado mkasema hapa kuna mnyonge anasaidiwa si kweli.

Ninachokiona mimj robo tatu ya waliochukuwa nyumba zile watanyang'anywa kwa kushindwa kurudisha marejesho kama mkataba wa kinyonyaji unavyotaka.

Hivyo basi ninamshauri Waziri Lukuvi na Mheshimiwa Rais wawanusuru wanyonge hawa kwa kuzifanyia uthamini upya nyumba zile na mikataba iandikwe upya ili watu wauziwe kwa bei ya haki

Vitu kama hivi ndio vya serikali kupata credit kwa wananchi na serikali ikaonekana inawajali watu wake kwa kuingilia kati uhuni huu wa PSPF.

Naishauri serikali hakuna mnyonge yeyote nchi hii anayeweza kulipa rejesho kila mwezi la laki sita na riba kubwa kiasi hicho, kama setikali ni sikivu huu ndio muda wa kuitumbuwa bodi ya PSPF na kwa kuratibu unyonyaji huu na ifanyike tathimini upya na itolewe bei elekezi, kama ujenzi ulifanyika kifisadi gharama wasibebeshwe wananchi wezi wote walioliibia Taifa mahali wanapostahili ni jela tu.
 
Back
Top Bottom