Waziri Lukuvi mpe Rais Magufuli ujumbe wangu

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,159
9,241
Wakuu heri ya mwaka mpya

Naomba nisiwapotezee muda wenu moja kwa moja niende kwenye hoja.

Thread hii sitaiandika kisomi ili angalau kila mtu aweze kuielewa kiurahisi.

Baada ya kukaa na kufanya uchunguzi juu ya namna ya upatikanaji wa nyumba kwenye shirika la nyumba la taifa hatimaye nimeona fursa.

Nafikiri ni wakati sahihi sasa serikali kujikita kwenye kutengeneza nyumba au makazi ya bei rahis ambazo zitapangishwa kwa wananchi wa kawaida bila urasimu kama ilivyo sasa ambapo inaonekana nyumba hizo ni maalum kwa tabaka flani lenye mamlaka.

Mfano pale Manzese pakavunjwa nyumba zote kisha serikali ikatenga eneo hata kule Kiluvya ikajenga makazi ambayo itayapangisha kwa wananchi wa kawaida.

Mfano: Serikali ikajenga majengo ya ghorofa kila jengo moja likawa na floor kumi, ina maana serikali ikijenga majengo ya aina hii ishirini ambayo huenda familiar 5000 zikakaa kwenye mahali hapa palipojengwa kwa viwango na kufuata ushauri wa kitaalamu serikali itakuwa imemsaidia mwananchi wa hali ya chini moja kwa moja.

Pia tutapunguza hatari mbalimbali kama magonjwa ya mlipuko yanayotokana na makazi kujengwa bila mpangilio.

Tutapunguza hatari zinazotokana na mafuriko.

Tutapunguza uhalifu kwa kiasi KIKUBWA.

Lakini pia tukifanya hivi miji yetu itakuwa ya kuvutia sana.

Naamini serikali ikijikita kwenye ujenzi wa namna hi itavuna mabilion ya pesa kutokana na kodi zinazolipwa na wapangaji.

Mahitaji ya makazi ni makubwa sana kwenye miji yetu.

NI wakati sasa Watanzania waache kuishi kwenye maeneo hatarishi kwa kupitia msaada w serikali.

Serikali inawajibika kwa namna yoyote kuhakikisha inawahudumia raia yake wapate makazi bora lakini pia raia hao hao ndio walipa kodi.

Sasa kama serikali haitazingatia maslahi ya raia wake ni kwa namna gani itaweza kukusanya mapato makubwa?

Mambo mengine ndugu zangu tuwe tunaiga hata kwa mataifa mengine vitu kama hivi viko ndani ya uwezo wetu.
 
Miji itavutia?

Wapi uliona Maghorofa yanayoishi kada ya Watu wa kipato cha chini yakawa kwenye hali nzuri, umeshaona maeneoa almaarufu kama kotaz yanavyokuwa.
 
Miji itavutia?

Wapi uliona Maghorofa yanayoishi kada ya Watu wa kipato cha chini yakawa kwenye hali nzuri, umeshaona maeneoa almaarufu kama kotaz yanavyokuwa.
Je tuwaache waendelee kuishi kwenye slams
 
Je tuwaache waendelee kuishi kwenye slams
Hali za Wananchi ziboreshwe kwanza, wakiwa na elimu na vipato vizuri hata ukijenga makazi bora wataweza kutunza na kuthamini.

Kinyume na hapo Mtajenga na hakutakuwa na maintanance za sewerage system, bomba, rangi n.k. maana itageuka mzigo mzito kwa wanaomiliki hizo nyumba.

Mwisho wa siku mtarudi pale pale...hakuna jamii isiyothamini vitu kama kada ya vipato duni...watachora chora kuta wataharibu milango, madirisha, vyoo.
 
Duuuuh mkuu watu wa vipato duni walikukosea nini

Je nyinyi mnaoishi masaki ndio pekee mnapswa kupata huduma za namna hi ?

Au nyinyi ndio mmestarabika ZAIDI?
 
Duuuuh mkuu watu wa vipato duni walikukosea nini

Je nyinyi mnaoishi masaki ndio pekee mnapswa kupata huduma za namna hi ?

Au nyinyi ndio mmestarabika ZAIDI?
Wewe shida yako ni zijengwe tu basi ufurahi, mwisho wa siku yanageuka magofu.

Hivi umeshayaona yale mabasi ya Mwendokasi yalivyo kwa sasa, pamoja na vituo vyake...vituo vile vimekuwa kama dampo za takataka.

Mimi ninachosema tufute/tupunguze kwanza watu wenye vipato duni ndio italeta maana kuwajengea hivyo...sasa nadhani hofu yako ni kuona kuimarisha uchumi wa Watu ni ngumu kuliko kujenga hayo maghorofa.
 
Back
Top Bottom