Waziri Lukuvi, kuna ucheleweshwaji wa makusudi wa hati za umiliki wa ardhi

Mouse3

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
1,421
1,241
Kwako Waziri was ardhi mheshimiwa Lukuvi.

Kumekuwa na ucheleweshwaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa namna ya kimakusudi! Mtu unanunua ardhi , unalipia urasimishaji, mipaka inahakikiwa! Ukitaka hati sasa shughuli inaanzia hapo.

Umeshalipa urasimishaji lakini unaambiwa subiria hati zitatoka ila sio leo! Ukiulizauliza watumishi hao hao wanakwambia tupe milioni kadhaa tulishughulikie ndani ya wiki mbili

Ukikataa wanakwambia hati utaipata baada ya miaka minne. Najiuliza hivi Kama unataka ukope kupitia ardhi yako ili ujenge au ufanye biashara zako inakuwaje?

Tunaomba mfumo wa kupata hati ufanyike online uwe kama Brela ukishalipia ada zako unatumiwa hati online una print na risiti unapewa.
 
Huyo Lukuvi huwa simuelewi kabisa, inashangaza kuona kuwa bado ni Waziri la ardhi wakati nafasi hiyo inampyaya.

Dar es salaam wilaya ya Ilala ulifanyika urasimishaji, wapimaji wakapewa hela yao 200000 kwa kila kiwanja huku Lukuvi akianikiza kuwa bei elekezi ni shs 100000 tu.

Maeneo yamepimwa na kurasimishwa, mawe yamewekwa huu sasa unakwenda mwaka wa pili, hakuna hati na waliopima wametokomea kusikojulikana!. Wananchi wamelipia, hati hazitolewi na Lukuvi yupo tu..... Huu ni wizi wa kitaasisi kama wizi mwingine tu.
 
Wilaya ya Kinondoni pia watu wamelipia upimaji sijui urasimishaji tangu Mwaka juzi/jana lakini hadi leo kimyaaaa.

Watu wa Bunju karibu na Shule ya Fanaka, madale wazo/ kontena na viunga vyake watu wamelipia tangu Mwaka jana lakini hati hakuna.

Inasikitisha sana.
 
Na kule Mbopo mtashugulikia lini?

Ni Mwaka wa ngapi sasa?

Kuna watu wanaendelea kunufaika kwa kutumia maeneo ya watu ambao walikopa bank na bado wanalipa marejesho lakini maeneo yao yanatumiwa na watu wengine.

Fanyeni maamuzi magumu mwenye kustahili apate haki yake.
 
Kule Mbopo muulizeni ex DC Daniel Chongolo anafahamu kiundani kinachoendelea na alifikia pazuri ktk kufanya maamuzi ya kuona haki ikitendeka.

CC: Mbunge Gwajima

DC Godwin Gondwe
 
Kuna makampuni walipewa kandarasi ya kupima maeneo/ viwanja ukanda wote wa wazohill, mivumoni, madale, msigani, mbopo, na mpaka sasa hawana majibu ni lini hati zitatoka, na fedha waliisha kusanya. (Tshs 250,000).

Kwa waombaji 1,000 tu, maana yake kampuni imekusanya Tshs 250,000,000
Kwa waombaji 10,000 , maana yake kampuni imekusanya Tshs 2,500,000,000

Kuna uwezekanao mkubwa makapuni haya yamekusanya mabillion ya pesa, na wizarani hawana taarifa za maombi ya watu hawa. pesa hizi wanawekeza kwenye miradi mingine. hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kukaa kimyaa, ndio uzalendo wenyewe.
 
Aisee hii inashangaza na kusikitisha sana.

Jamaa wamechukua hela halafu hakuna hati .

Halafu kazi imefanyika serikali ya mtaa ikijua na wajumbe wa mashina wakihusika.

Jamani eeeh wananchi wanataka hati zao haraka.
 
Nyakasangwe tu ndio wale wapimaji wamefanya kazi Nzuri sana wakishirikiana na ex DC Chongolo, Manispaa, serikali ya mtaa.

Hati zilitoka kwa wepesi kabisa.

Kama mtu una eneo Nakasangwe fuatilia kalipie upewe hati yako bila utasimu wowote.
 
Ule mgogoro sugu wa ardhi maeneo yale yawezekana ikawa sbb ya hati kutolewa mapema.
 
Aisee hii inashangaza na kusikitisha sana.

Jamaa wamechukua hela halafu hakuna hati .

Halafu kazi imefanyika serikali ya mtaa ikijua na wajumbe wa mashina wakihusika.

Jamani eeeh wananchi wanataka hati zao haraka.
Kupata uhalali ya njia za mkato mkato lazima serikali za mtaa na wajumbe wahusishwe.

NI KAMA HIZI KAMPUNI ZA KUUZA ARDHI NA UNALIPIA KIDOGO KIDOGO , KUNA WATU WATAKUJA KULIA NA KUSAGA MENO
 
Kupata uhalali ya njia za mkato mkato lazima serikali za mtaa na wajumbe wahusishwe.

NI KAMA HIZI KAMPUNI ZA KUUZA ARDHI NA UNALIPIA KIDOGO KIDOGO , KUNA WATU WATAKUJA KULIA NA KUSAGA MENO
Hebu tupatie hizo dondoo za kujihami ili tusije lia kwa wingi,maana wametuchota sana akili kutokana na hizi Hali ngumu za maisha tunayopitia
 
Hakika inasikitisha sana...
Inakatisha tamaa! Ukiwa na maono ya kufanya maendeleo alafu serikali yako haikupi support hata ya kukulindia haki zako hii inafubaza maendeleo! Hakuna watu wanajituma usiku na mchana afrika kama watanzania! Asilimia 98% ya watanzania wamejiajiri! Kwa mataifa mengine tungekuwa watu wakulishwa na kuombaomba serikalini chakula cha misaada! Amka saa tisa usiku kwenye majiji, miji utakutana na wakina mama, vijana na wengineo tayari wako mbiombio na mizigo na biashara zao Lakini wakitaka kujiongeza kufanya makubwa lazima wakutane na kikwazo kutoka wizara za serikali! Yaani mtu anayejifanyia maendeleo bila kuihusisha serikali anafanikiwa haraka na anakuwa huru kuliko kushirikisha serikali! Ukisha jipeleka tu kwenye hizo wizara lazima upate kahasara au hasara taslimu! Hawaelewi ndoto za mtu zinakimbizana na muda pia! Sijui kwanini hatupati watendaji kama wa mataifa ya ughaibuni! Mimi nashauri mameneja wa kila wizara serikali iajiri WAZUNGU/WAHINDI
na hawa ma HR wawe white people watukimbize kwa miaka kadhaa na hakika tuta adopt silka za kiutendaji na kupata kizazi chenye hulka ya utendaji mzuri!
 
Back
Top Bottom