Waziri Lukuvi: Kuanzia sasa ukiwa na kiwanja kinatakiwa kiitwe kwa jina lako na la mke wako

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,615
32,722
lukuvi.jpg

Serikali imesema sheria inaruhusu hati ya kumiliki viwanja kuandikwa majina ya familia ikiwemo mume, mke pamoja na watoto hatua ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya mirathi.

Akizungumza leo Jumamosi Desemba 19, mkoani Kilimanjaro. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliamu Lukuvi amesema kwa sasa wizara hiyo inasajili majina hayo na kwamba Watanzania watumie fursa hiyo vema kupunguza migogoro ya mirathi.

“Sisi katika wizara hii na serikalini humu tunapata shida sana ya kushughulikia mambo ya mirathi,wizara inakubali kusajili hati kwa majina zaidi ya mawili hata ukita baba,mama na watoto kusajili hati Moja inaruhusiwa hii inasaidia kuepusha matatizo ya miradhi hapo baadae,” amesema Lukuvi.

Aidha, Waziri Lukuvi ametoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na kwamba keai nyingi za miradhi huwa na changamoto nyingi”alisema

“Kesi nyingi za mirathi wanakuja wajomba ambao hawakujua jasho lenu ambalo mmelichuma wanaandika hati wao wanajimilikisha hiyo ni fursa kwa wananwake…washawishini waume zenu wakati wa kuandika hati mje na majina yenu wote…hata kama umeoa wanawake watatu, sheria ipo wazi,ukija na jina la mtoto chini ya miaka 18 tutasajili jina lake na msimamizi wake.

“Ndoa zote tutaandikisha, akifa mke mmoja inafahamika kwamba haki iliyobaki ni ya wake wawili waliobaki na kwa upande wa mtoto akifikisha miaka 18 kunauwezekano wa kufuta majina ya awali ya wazazi na kumuachi mtoto,” amesema Lukuvi.

Aidha amesema utaratibu huo ikifiatwa hakutakuwa na vikao vya familia vya miradhi na migogoro isiyo ya lazima.

“Sio lazima kwamba mtu alitaka hati aje na mme wake zao Ila ni jukumu langu kuwalemisha kwamba Hilo linawezek,” amesema.

Mtanzania

Pia soma - Waziri Lukuvi, sio lazima kisheria jina la mke na mme kuwa kwenye hati ya kiwanja
 
Sheria hata kama zimekanyagwa lakini hatujafikaia hapa. Sheria za mkataba na sheria ya ndoa mbona jambo la umiliki wa mali huko wazi sana. Hili nimetoka wapi au ni mahaba binafsi. No court of law can entertain such a baseless and unsound political nonsense.
 
Upuuzi mtupu

Hajui kuwa nchi hii ni halali kuwa na ndoa za wake wengi?

Kwa hiyo ukimuoa Fatuma ukanunua kiwanja utamuweka fatuma, kisha baada ya miaka mitano ukamuoa Asha, itabidi ubadili hati umuongeze asha, baada ya miaka miwili ukamuoa Zainabu itabidi ukabadili hati umuweke na Zainabu? .

Je, ukimtaliki Asha akakupekeka mahakamani kudai chake inabidi kiwanja kiuzwe ili mgawane hicho kiwanja licha ya kuwa umeandika majina ya wake zako wengine watatu waliobaki?

Au huyu mdini anataka kutengeneza mazingira ya kutaliki wanawake iwe ngumu kwa kufungamanisha mali na ndoa? - Anataka kuachieve mfano wa ndoa ya Kikanisa kwa watanzania wote kwa mlango wa nyuma?. Katika hilo Lukuvi hutofanikiwa ng'o!
 
Hawa ardhi siwaelewagi kabisa halafu nimenusa kunamazingira ya kuwadhurumu wananchi wa DODOMA kwa yale maeneo yanayoonekana ni fursa kwa kuchukua 30% ya ardhi kama gharama za upimaji na ukiwaambia uwalipe hawako tayari kulipwa.

Na yapo mazingira baadhi ya wakubwa kurukwa katika mpango wa kutengeneza barabara lakini kilicho kibaya mkazi anapimiwa viwanja vitano halafu katika eneo lake anapewa vitatu vingine anaenda kupewa eneo lingine hii sio sawa kabisa na MWENYEZI MUNGU anawaona.

Wamekuwa watu fulani wa double standard hii si sawa
 
Ni matamko mangapi yametolewa mwisho yakafanya kazi kama sheria?
Hayo matamko ni kama yapo? Labda kama yaliamuliwa na vikao vya ukoo. Hamna mahakama (Hata kama zimeoza) itafanyia kazi maneno ya mtaani. ( lazima kuwepo na legal loophole)
 
Back
Top Bottom