Waziri Lukuvi: Dar es salaam kujengwa miji ya kisasa 25 badala ya watu kurundikana Upanga na Kariakoo. Jiji litaendelezwa kwa kwenda juu ( maghorofa)

Tatizo hatuna wataalamu wala wabunifu wa mipango miji.
waliopo/walio ajiriwa na Serikali wanakula mishahara buree kabisa, hakuna ubunifu wanao ufanya, ujenzi holela kila kukicha!!

Jiji la DSM linapaswa lipanuke maeneo ya pembezoni kama vile Kibamba, kiluvya n.k lkn wapi, wataalamu wa mipango miji wapo wapo tu!
 
Huyu jamaa huwa ana mipango na kauli nzuri kweli, ila tatizo ni utekelezaji!

Mipango ifuatayo alishaieleza mh Lukuvi, sijajua utekelezaji upoje huko ulipo;

1. Kutoa leseni ya makazi kwa TSH 7,000/= tu kwa mwaka nchi nzima. Leseni hizi zilihusu makazi ambayo hayana hati za umiliki. Mpango huu aliusema enzi za jiwe.

2. Kuipima ardhi yote ndani ya nchi, pamoja na kurasimisha makazi nchi nzima. Huu mpango aliusema pia enzi za jiwe.

3. Kumiliki jengo hasa ghorofa moja kwa hati tofauti tofauti. Yaani, kwa mfano, floor namba moja inamilikiwa na Juma na hati yake. Floor namba mbili inamilikiwa na James na hati yake. Huu mpango aliusema pia enzi za jiwe.

4. Mpango ambao ameusema enzi za mama ni huu wa anuani za makazi. Kwamba, kufikia April 2022 makazi yote nchini yawe na anuani, yaani postcode.

Shahidi ni wewe, je huko unapoishi kuna mpango wowote wa Lukuvi umefanikiwa angalau kwa 75%?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Dawa ni kuwezesha mikoa mingine watu wenyewe automatic wataondoka
Na mambo yatabalance, sio leo kila kitu dar au dom huu ni ushamba na uzamani,
Mfano fugua bandari ya tanga uone watu watkavyokimbilia pale, tumia bandari ya mtwara uone kama wamachinga watakuja kusumbua mjini, jenga viwanda vingi pale mwanza uone kama kuna mtu atakimbilia dar nk nk
 
Waziri wa ardhi mh Lukuvi amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla mpango mpya wa ujenzi wa jiji hilo.

Lukuvi amesema ndani ya Dar es salaam itajengwa miji midogo ya kisasa 25 na kwa maana hiyo hakutakuwa na sababu watu kurundikana Upanga na Kariakoo.

Kadhalika Lukuvi amesema Jiji la Dar es salaam sasa litaendelezwa kwa kwenda juu yaani ujenzi wa maghorofa baada ya maeneo kuwa yameshajaa.

Source: ITV habari
Huyo mzee a naishi wapi? Watu wamalundikana mbagala, gongolamboto, mbezi mwisho na si kariakoo wala Upanga
 
Waziri wa ardhi mh Lukuvi amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla mpango mpya wa ujenzi wa jiji hilo.

Lukuvi amesema ndani ya Dar es salaam itajengwa miji midogo ya kisasa 25 na kwa maana hiyo hakutakuwa na sababu watu kurundikana Upanga na Kariakoo.

Kadhalika Lukuvi amesema Jiji la Dar es salaam sasa litaendelezwa kwa kwenda juu yaani ujenzi wa maghorofa baada ya maeneo kuwa yameshajaa.

Source: ITV habari

Aache utapeli wa kijinga, serikali hii imeshindwa hata kutoa vitambulisho vya taifa ndio itakuwa kujenga magorofa?
 
Waziri wa ardhi mh Lukuvi amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla mpango mpya wa ujenzi wa jiji hilo.

Lukuvi amesema ndani ya Dar es salaam itajengwa miji midogo ya kisasa 25 na kwa maana hiyo hakutakuwa na sababu watu kurundikana Upanga na Kariakoo.

Kadhalika Lukuvi amesema Jiji la Dar es salaam sasa litaendelezwa kwa kwenda juu yaani ujenzi wa maghorofa baada ya maeneo kuwa yameshajaa.

Source: ITV habari

1641245843748.png

Angeanza kwanza na uwezekano wa wasafiri kutoka Airport kwenda Mbezi-Louis kwenye kituo cha mabasi ya kwenda mikoani. Watu kutoka mikoani na wale wanao kwenda mikoani kutoka Julius Nyerere Airport ni tatizo. Mtu mwenye akili timamu atapangaje miji namna hii?
 
Back
Top Bottom