Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kila wakati Lukuvi anapenda kutoa tishio kwa Watanzania waliopewa viwanja na serikali kuwa watanyang'anywa kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga. Yaani Lukuvi anachosema ni kwamba, hawakustahili kupewa hivyo viwanja kwa kuwa wao hali yao ya kuichumi iko chini na hawana uwezo wa kujenga haraka.
Ugawaji wa viwanja ulikuwa mpango wa serikali na wengi wa waliofaidika na mpango huu walikuwa watu wa kawaida kabisa ambao wanapambana na ugumu wa maisha ya kila siku. Wengi ni wafanyakazi wa serikali au mashirika ya umma wakitarajia watakapopata mafao ya kustaafu watajenga nyumba zao kwenye viwanja hivyo. Hakuna mtu mwenye kiwanja asiyependa kujenga nyumba, hilo liko wazi.
Lakini ajabu ni kwamba Lukuvi hafikirii hilo hata kidogo. Yeye anachojua kila mtu aliyepewa kiwanja ni fisadi mmoja ambaye ana mamilioni ya fedha kaweka mahali na sasa hataki tu kujenga nyumba kwenye kwanja alichopewa na serikali. Kuna wakati hata nafikiria kwamba Lukuvi anafikiri kwamba fedha anazopata kama mshahara na marupurupu kama waziri basi ndivyo ilivyo kwa Watanzania wote - na kwa kuwa yeye ana uwezo wa kujenga nyumba wakati wowote haelewi kwa nini Watanzania waliopewa viwanja washindwe kufanya hivyo.
Msimamo huu wa Lukuvi ni upofu wa hali halisi ya uchumi ya Watanzania kwa kuwa asilmia kubwa sana ya Watanzania, na hata hao waliopewa viwanja wanahangaika kulipa ada za shule za watoto, kulipia kodi ya nyumba, na hata chakula na mavazi. Hali hii imezidi kuwa ngumu katika awamu hii ya tano ambayo Lukuvi ni sehemu yake. Lukuvi haoni hilo, anachotaka ni Watanzania hao waache kuhangaikia ada na chakula ili wajenge hizo nyumba haraka sana. Kwanza tumuulize Lukuvi, je kwa upande wa serikali, imeshapeleka miundo mbinu kama barabara, maji na umeme katika maeneo haya, au bado viwanja hivi viko porini na serikali inachoona ni kibanzi katika macho ya waliogawiwa viwanja!
Ukweli ni kwamba watu wenye hela, huenda wengine ya ufisadi au mambo mengine, au vigogo kama Lukuvi mwenyewe, walishajenga siku nyingi sana. Na sasa labda Lukuvi atuambie, wakati serikali ikitekeleza mradi huu wa kugawa viwanja, nani hasa waliokuwa walengwa wa kupewa viwanja? Je walikuwa ni Watanzania mafisadi au wenye kipato kikubwa kama cha Lukuvi? Je yule mfanyakazi wa kawaida wa serikali anaesubiri mafao ili ajenge, hakustahili kupata kiwanja?
Kama Lukuvi angekuwa na uwezo mzuri wa kuona uhalisi wa mambo kama kiongozi wa wananchi ambao serikali ilitaka kuwasaidia kuwa na nyumba za kisasa, jambo ambalo angefanya badala ya kufoka watu watanyang'anywa viwanja kufikia December 2019, ni kuanzisha mpango wa mikopo nafuu ili watu wajenge. Tena mikopo hiyo isiwe na riba na itolewe kwa kutumia collateral ambayo ni mafao yaliyopo mifuko ya hifadhi. Ikibidi, taasisi hizo za hifadhi ya jamii ndio zitoe mikopo hiyo ya kujengea nyumba isiyo na riba. Benki kwa sasa zinatoza riba hadi 25%, Mtanzania gani wa kipato cha kawaida anaweza kukopa huko ili ajenge?
Lukuvi, asisahau yeye na viongozi wenzake awamu ya tano ni viongozi wa wananchi wote, wenye kipato kikubwa na kidogo. Anapaswa kupima mwenyewe kama ni halali kuwanyanganya viwanja wananchi wasio na uwezo wa kujenga ili kuwapa wananchi wenye uwezo wa kifedha, badala ya kuwawezesha ili waweze kujenga nyumba za kisasa.
Lukuvi hapaswi kuwapigia kelele za kuwanyang'anya wananchi viwanja wakati hujafanya lolote kuwasiaidia kujenga katika hivyo viwanja. Inafanya tutilie shaka lengo lake hasa hapa yeye na viongozi wenzake kuhusu hivyo viwanja. Usikute wanataka kuwanyang'anya wananchi hivyo viwanja ili wagawane kama walivyogawana nyumba za serikali huko nyuma!