Waziri Lukuvi atoa onyo kwa wanaojenga bila kufuata utaratibu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1578890785352.png

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu.

Mhe. Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma wakati akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya ujenzi.

Waziri Lukuvi alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuri zote hadi wafuate utaratibu.

Hata hivyo Mhe. Lukuvi amesema Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha ujenzi.
 
Lakini wajumbe wake wanamuangusha sana, mimi tangu mwaka jana mwezi wa sita nimeomba kibali cha ujenzi wilaya ya temeke ila napigwa dana mpka hii leo. Wanatengeneza mazingira ya rushwa na mimi nimeamua kutowapa
 
Back
Top Bottom