Waziri Lukuvi ateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa! Yumo Humphrey Polepole

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Waziri Lukuvi ameteua wajumbe hao 7 wa bodi ya shirika la nyumba la taifa, leo Mei 20, 2019 siku chache baada ya Rais Magufuli kumteua Dr. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Wajumbe walioteuliwa ni,

1. Bi. Immaculate Senye
2. Bi. Sauda Msemu
3. Bw. Abdallah Mwinyimvua
4. Bw. Humphrey Polepole
5. Bw. Martine Madeke
6. Eng. Mwita Rubirya
7. Bw. Charles Singili

IMG_20190520_230013.jpeg
 
Huyo jamaa tangu aliposhiriki kunajisi rasimu ya katiba nikimuona ameingia sehemu huwa naona pameshanajisika...
Labda yuko hapo kama si kwa maslahi mapana binafsi itakuwa kwa chama chake...
Tusubiri matokeo...
 
Ukiona mtu anahangaika kujinyonga kwenye shina la muhogo, ujue ni kiwango cha juu kabisa cha ujinga. Lukuvi hajawahi kuwa serious na kazi yake. Not ethical. Kuke Iringa ana viwanja kibao!! Kila leo anajipimia maeneo yake binafsi. Nadhani ana hati zaidi ya uwezo wa ukoo wake. Leo hii unaweka watu ambao hata hawajui kusoma scale? Watu wa performing arts?

Nchi bado inajaribia watu kuongoza. Ila naona walio wengi ktk mafanikio ni wale ambao hawana aibu. Angalia Mkumbo na wizara ya maji, kweli unaweza kuweka mtu asiyejua kabisa sayansi ktk wizara ya maji? Ataelewa lini? ktk chama hivyo hivyo!
 
Appointment powers za Waziri kuteua mtu yoyote kuwa mjumbe wa bodi fulani iliyopo chini ya wizara yake, ni sawa na presidential appointment powers kuteua wasaidizi wake, ana mamlaka ya kumteua yoyote kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote na teuzi hizi, hazihojiwi popote.

Hivyo nawaombeni tuache kumuingilia waziri katika teuzi zake. Nliwahi pia kushauri humu tuepuke kumuingilia rais katika teuzi zake, kama heshima kwa wakuu wetu, kuna vitu haturuhusiwi kuhoji,
P
 
Hivyo nawaombeni tuache kumuingilia waziri katika teuzi zake. Nliwahi pia kushauri humu tuepuke kumuingilia rais katika teuzi zake, kama heshima kwa wakuu wetu, kuna vitu haturuhusiwi kuhoji,
P
Bila shaka hata hii imo ndani ya Katiba...oops, Katiba, my foot! Samahani sana Pascal Mayalla, naona nimesahau kwamba katika utawala wa kidikteta haturuhusiwi kuhoji na Katiba ni mawazo aliyoamka nayo kiongozi siku hiyo. Ole wako aamke vibaya, idadi ya watakaolimia meno au watakaomiminiwa risasi si haba!
 
Ukiona mtu anahangaika kujinyonga kwenye shina la muhogo, ujue ni kiwango cha juu kabisa cha ujinga. Lukuvi hajawahi kuwa serious na kazi yake. Not ethical. Kuke Iringa ana viwanja kibao!! Kila leo anajipimia maeneo yake binafsi. Nadhani ana hati zaidi ya uwezo wa ukoo wake. Leo hii unaweka watu ambao hata hawajui kusoma scale? Watu wa performing arts?

Nchi bado inajaribia watu kuongoza. Ila naona walio wengi ktk mafanikio ni wale ambao hawana aibu. Angalia Mkumbo na wizara ya maji, kweli unaweza kuweka mtu asiyejua kabisa sayansi ktk wizara ya maji? Ataelewa lini? ktk chama hivyo hivyo!
Sio Iringa tu uliza Dodoma.
 
Huyo jamaa tangu aliposhiriki kunajisi rasimu ya katiba nikimuona ameingia sehemu huwa naona pameshanajisika...
Labda yuko hapo kama si kwa maslahi mapana binafsi itakuwa kwa chama chake...
Tusubiri matokeo...

Ndugu; matokeo gani tena unayoyasubiri? Msimu ukiisha bingwa na alieshuka daraja huwa wameshafahamika pia.
Hakuna kitakachofanikiwa chini ya utawala huu uliofitinika.
 
Back
Top Bottom