Waziri Lukuvi ashiriki zoezi la kuvunja nyumba yake iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara

Mbona nyumba yenyewe ni kama gofu, inaonekana aliitelekeza!
Isitoshe yeye siyo mlala hoi, anazo nyumba nyingi tu so hawazi yeye na familia yake watalala wapi!
Kilichoniacha hoi zaidi, kwenye hiyo video anaonekana akivunja bila kuchukua tahadhari yoyote, anagongagonga tu kwa nyundo!
Ana bahati tofali halijamgusa...
Mambo mengine ni kiki tu...
 
Huu ndo ule unafiki ambao siupendi, eti amevunja nyumba,? Aache kuadaa watu huo
 
Duuuuuuuuuuuuuu! aliyenacho kweli anacho. maneno rahisi rahisi kweli. Hivi ningekuwa mimi ninavunja nyumba ninakwenda kukaa wapi na familia yangu. Huo ni mfano wa kibeberu.


"HEBU CHEKI WATU WALIVYOJAA ROHO MBAYA"

Jamaa mmoja alishukiwa na Malaika toka mbinguni akaambiwa omba chochote unachotaka lakini Jirani yako yeye ndiye atapata mara mbili

.....Kwa Mfano ukitaka MTOTO 1 jirani yako atapata WATOTO 2, ukitaka GARI 1 jirani yako atapata MAGARI 2

Huyu jamaa akafikiria sana kwa muda halafu akamwambia Malaika

....NITOE JICHO MOJA" ili jirani yake yatoke yote mawili na asiweze kuona kabisa.

MSICHEKE BINADAMU NDIVYO TULIVYO
 
Kwa muono Wang, wazir alitakiwa ajiuzulu cheo chake na ikiwezekana hata ubunge km VP. Kwa sabab nafac aliyonayo na kosa alilolifanya tayar inamuondolea heshima ya kubaki ndani ya baraza la mawazir
 
Awadanganye wajinga wake huko, huku kuna wasomi wanaweza wakatafakari mambo. Na kweli nadhani wanashangilia wakati alicho kibomoa anaweza akakijenga bila kutoa hela mfukoni.....
 
Mimi nina swali la msingi sana kwa wataalamu, naomba kujua,.
Kuna nyumba zimewekewa alama ya X na tanroad wamevunja ikiwa zina hati miliki halali, watu hawa serikali inawaangaliaje ikiwa serikali yenyewe ndio ilitoa hati hizo,? Na hati hizo zimetoka miaka mingi tu, hususani Barbara ya morogoro maeneo ya kimara.
Naombeni mnijuze ni hatua gani ya kuchukua.
 
Nyumba mbovu hii, na sasa kama si kutafuta sifa ameita hadi waandishi wa habari wamuhoji usanii mtupu. Maigizo at its best.
 
Back
Top Bottom