Waziri Lukuvi ashiriki zoezi la kuvunja nyumba yake iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi ameshiriki zoezi la uvunjaji wa nyumba kwa kuvunja nyumba yake kwa hiari iliyokuwa imejengwa ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara.

Waziri Lukuvi amevunja nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara kuu iendayo katika hifadhi ya Ruaha katika Kijiji cha Mapogolo, mkoani Iringa.

“Kama kiongozi nimeamua kuonyesha mfano kumuunga mkono Mhe. Magufuli ambaye ameamua kuiboresha barabara hii kuwa kiwango cha lami mpaka Ruaha National Park ili kuongeza mapato ya nchi lakini pia kuongeza vipato kwa wananchi wa barabara hii wanayoitumia”.

“Kwa faida hizo nimeamua mimi mwenyewe kuvunja leo hii nyumba ili wananchi wa eneo hili ambao barabara hii itajengwa lazima wahakikishe wanabomoa wenyewe nyumba zao,” alisema Waziri Lukuvi.

Aidha Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuzivunja wenyewe nyumba zao ili kurahisisha zoezi la upanuzi wa barabara hiyo uwe wa muda mfupi, kwani barabara hiyo inajengwa kwa manufaa yao.

“Lazima tutii sheria bila shuruti. Tuliowekewa alama ya X tuvunje nyumbza zetu ili kazi ya ujenzi wa barabara hii iwe nyepesi, gharama iwe ndogo na iende kwa muda mfupi,” alisema Waziri.

Vilevile aliwakumbusha wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuwa wasitegemee fidia yoyote kutoka serikalini na badala yakee waanze kuzibomoa nyumba zao pasipo kusubiri kuja kubomolewa kwa nguvu.

“Serikali haitolipafidia kabisa kwa watu waliojenga kwenye eneo la barabara kama mimi,” alisema.


Mpekuzi
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
44,473
2,000
Waziri Lukuvi amevunja nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara kuu iendayo katika hifadhi ya Ruaha katika Kijiji cha Mapogolo, mkoani Iringa.

“Kama kiongozi nimeamua kuonyesha mfano kumuunga mkono Mhe. Magufuli ambaye ameamua kuiboresha barabara hii kuwa kiwango cha lami mpaka Ruaha National Park ili kuongeza mapato ya nchi lakini pia kuongeza vipato kwa wananchi wa barabara hii wanayoitumia”.
angeonesha mfano kwa KUTOKUJENGA NDANI YA HIFADHI....na sio sasa hivi!
 

Lapjuu

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
219
250
Nyumba yenyewe ya sent hamsini, hata ingekuwa mimi haingeniuma kuibomoa.
 

20fanaka

Senior Member
Apr 19, 2017
141
250
Hakuna namna maumivu tuyapate wote tu!

Uholela wa zamani ndio uliozaa madhara haya kwenye enzi hizi za sheria ya msumeno inayosimamiwa bila upendeleo.
 

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,452
2,000
Mitaji ya kisiasa hadi unaweza tembea uchi kwa ajili ya kiki za kisiasa tu. Akitoka hapo kwa hasira anaenda kumtishia Ponjoro mmoja tu kuwa anafuta hati ya shamba/kiwanja chake, Mhindi analipa "fidia" ya hiyo nyumba mara tano yake
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,875
2,000
Mnafiki huyooo!! Si ndio aliwabeba mafisadi akawapeleka kwa Magu baada kuapishwa....ili kama ana kazi awape? Si ndio huyu?? Mnafiki huyu baba...ngumbalu!! Aend zake!! Uwezo‎
wake analinganisha na wanakijiji ambao hadi sasa hawajauza mahindi tangu June bei haieleweki?? Msimu umekaribia hajauza mahindi na nyumba wamebomoa!!! Yeye anabomoa nyumba anayofikia mara 1 kwa mwaka na haizidi masaa 5 kufikia humo!!!!‎
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom