Waziri Lukuvi amtumbua Hadharani kigogo wa Ardhi Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,William Lukuvi amemfukuza kazi afisa Ardhi wilaya ya Arumeru,Nicodemus Hillu kwa kosa la kurejesha eneo lenye ukubwa wa hekari 3000 kwa mwekezaji lililokuwa limefutwa umiliki wake na Rais John Magufuli na kuisabahishia serikali hasara ya kulipa fidia ya zaidi ya sh,million 5.

Aidha waziri Lukuvi amempandisha Cheo aliyekuwa afisa Ardhi mteule wa halmashauri ya Arusha,Rehema Jatto kuwa Afisa Ardhi mteule jiji la Arusha baada ya kuridhishwa na utendaji wake wa kazi usio na shaka.

"Huyu mtumishi kuanzia Leo mwambieni nimemfukuza kazi kwa sababu Rais alifuta eneo la mwekezaji la ekari 3000 lakini yeye kwa maksudi aliamua kumrejeshea kinyemela sijui alimlipa ngapi ityabidsi Takukuru wafuatilie alihongwa nini " Alisema Lukuvi

Waziri Lukuvi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizindua ofisi za Ardhi za mkoa wa Arusha na kukabidhi hati za Ardhi kwa wananchi zaidi ya 200 waliokuwa wameomba kwa muda mrefu.

Alisema kuwa serikali imeamua kujeresha huduma ya Ardhi Mikoani zikiwa na hadhi ya wizara ikiwa ni mpango wa kuwarahisishia wananchi kupata hati katika maeneo yao badala ya awali walikuwa wakisotea hati hizo ofisi za kanda.

Aidha aliwataka maofisa Ardhi kufuatilia michoro yote ya Ardhi ambayo wananchi wamepimiwa na kutoa hati miliki ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata mikopo na uhakika wa makazi yao.

Waziri Lukuvi alitoa Siku 90 kwa maofisa Ardhi nchini kuhakikisha wanatoa hati za Ardhi kwa wananchi waliokwisha pimiwa michoro .

Katika hatua nyingine waziri Lukuvi amepiga marufuku matapeli wa Ardhi kuingia katika ofisi za Ardhi kwani katika jiji la Arusha wamewaumiza sana wananchi.

Alisema kuwa amehamisha taarifa zote za Ardhi tangu Uhuru ikiwemo michoro za mkoa wa Arusha zilizokuwa katika ofisi ya kanda mkoani Kilimanjaro ili kurahisisha wananchi kupata taarifa za za Ardhi.

Awali mkuu wa mkoa wa Arusha ,Iddy Kimanta amesema kuwa atahakiisha kero za Ardhi katika ofisi za Ardhi mkoani zinamalizika ndani ya siku saba huku akiahidi kumaliza migogoro ya Ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na kubaki historia

Kimanta amefuta siku mbili za kumwoana Mkuu wa mkoa zilizokuwa akitumia mtangulizi wake ,Mrisho Gambo badala yake amesema kuwa atahakikisha anasikiliza kero za wananchi kila siku kupitia kitengo maalumu atakachokiteua.


Ends....

IMG-20200624-WA0005.jpeg
 
Maswali

Alipewa nafasi ya kujitetea na kusikilizwa kabla ya hukumu?

Je ni afisa ardhi peke yake anauwezo wa kutoa hati ya eneo kubwa hivi?

Kama eneo lilifutiwa umiliki na raisi, alipata wapi ujasiri wa kulirudisha tena
The right to be heard.....sawa kabisa...
 
Lukuvi anafanya kazi Nzuri sana!

Yani kati ya Wizara zenye matatizo sugu ni pamoja na hii lakini walau huyu bwana amerekebisha mambo Mengi kwa manufaa ya wananchi.
 
Back
Top Bottom