Waziri Lukuv,i unalijua hili shamba la hekari zaidi ya 5000 Buhemba - Butiama?

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,187
Tunaona umhimu na juhudi za serikali ya awamu ya tano inavyojitahidi kurejesha ardhi zilizotelekezwa na wawekezezaji kwa wananchi ili waweze kuziendeleza kwa kilimo na makazi bora.
Kituo cha kilimo na ufugaji kilichopo Buhemba wilaya ya Butiama ni Kituo kinachomiliki hekari zaidi ya 5000,,, nikiwa mdogo miaka ya 80 mpaka 90 mwanzoni niliona juhudi za hiki Kituo katika masuala ya kilimo na ufugaji wa ng'ombe wa kisasa japo hawakuzidi 200.
Wananchi walikua wanaweza nunua maziwa maana kilikua na uwezo wa kutoa maziwa japo hakikua na uwezo wa kutoa lita 100 kwa siku

Ilipofikia miaka ya 90 mwishoni Kituo uzalishaji wa kilimo na mifugo ulipungua mpaka sasa tunapoongea Kituo kina ng'ombe wasiozidi 15 japo kinamiliki zaidi ya hekari 5000 huku wananchi hawana maeneo ya kilimo maana eneo kubwa la kilimo walichukua wao na wananchi wakabaki na maeneo ya vilivyo jaa mawe ambako hawawezi zalisha mazao.
Kituo kinamiliki zaidi ya hekari 5000 lakini eneo wanalotumia kulima halifiki hata hekari 10 maana wanalima ni zao la chakula tuu ambapo hata mwananchi mmoja ana uwezo wa kulima eneo dogo kama Hilo huku maelufu ya hekari yakibaki bila kuendelezwa.
Wananchi wanalitamani sana eneo Hilo ili wazalishe mazao Ila hawana wa kuwasaidia maana lipo wazi miaka yote na kituo hakilitumii.

Kuna shida gani serikali iweze kuwasaidia kumiliki hekari 2000 kati ya hizo ili wazalishe mazao zaidi katika wilaya hiyo???
Je Lukuvi unalijua hili eneo???

kama haulijui basi Tunaomba uwasiliane na mbunge wa Butiama Nimrod mkono atakupa maelezo katika na ikibidi utembelee huko utaona hilo jipu ili hiki Kituo kipunguziwe eneo ili wananchi walizalishie mazao maana
limetelekezwa na hawa wawekezaji huku wananchi wanaozunguka eneo hilo hawana ardhi ya kulima.
 
Hata jk ana hekar elfu 8 kule msoga, kati ya hizo anatumia hekar 20 alizojengea nyumba....nazan awagawie na wengine walime
 
Lukuvi bana Jana kadai eti alitema hongo ya bilioni 5 yaani waziri haoni Ata aibu kudanganya duh .
 
Ila hili ni la familia ya nyerere


Ukisikia butiama usidhani kuwa basi butiama kila mahali aliishi Nyerere watu wengine hawapo,,, hilo eneo siyo la nyerere ni la mwekezaji chini ya kanisa la kianglikana lakin hakuna kinachofanyika zaidi ya kuwanyima wananchi maeneo ya kukuza uchumi kupitia kilimo, ufugaji na hata makazi bora maana wananchi wana eneo la vilima vilivyojaa mawe huku eneo la tambarale likiwa chini ya hiki kituo bila shughuli yoyote miaka nenda rudi
 
Back
Top Bottom